Rais wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA), Dkt.Serafina Mkuwa (kulia), akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi na matibabu ya Saratani ya Matiti na mlango wa kizazi mkoani Mwanza.
Kampeni hiyo itazinduliwa kesho katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan na baadaye kufanyika kwa siku mbili bure.
Na BMG
Kutoka kushoto ni Dkt.Mary Charles ambaye ni Makamu wa Rais MEWATA, Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald Subi, Rais wa MEWATI, Dkt.Serafina Mkuwa, Mwenyekiti Kamati ya Kampeni na Mjumbe kamati tendaji MEWATA, Dkt.Magdalena Lyimo pamoja na Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Mwanza, Secilia Mrema.
Pia watumishi wa afya mkoani Mwanza wamepatiwa mafunzo kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi
Na George Binagi-GB Pazzo
Makamu wa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu, kesho
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kampeni ya uchunguzi na
matibabu ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi bila malipo mkaoni Mwanza.
Rais wa
Chama cha Madaktari Wanawake nchini MEWATA, Dkt.Serafina Mkuwa, ameyasema hayo
hii leo Jijini Mwanza wakati akitoa taarifa ya kampeni hiyo kwa wanahabari.
Amesema
baada ya ufunguzi wa kampeni hiyo, akinamama na wasichana mkoani Mwanza,
watapata fursa ya kufanya uchunguzi na matibabu ya Saratani ya matiti na mlango
wa kizazi kwa muda wa siku mbili ambazo ni kesho na kesho kutwa katika vituo
vinne ambavyo ni Uwanja wa Furahisha, Vituo vya Afya Makongoro, Karume pamoja
na Igoma Jijini Mwanza ambapo huduma zitakuwa zikitolewa kuanzia majira ya saa
moja asubuhi.
Tatizo la
saratani ya matiti na mlango wa kizazi bado ni changamoto kubwa mkoani Mwanza ambapo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald Subi, anabainisha kwamba takwimu zilizopatikana katika halmashauri za Ukerewe, Buchosa pamoja na
Kwimba, zinaonesha kwamba kati ya wanawake 1,294 waliochunguzwa, 58 wanamabadiliko ya awali ya saratani na 18 wanamabadiliko makubwa ya saratani na wamepewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hata hivyo
Dkt.Subi amewahimiza wananchi kuepuka matumizi ya tumbaku, sigara pamoja na
pombe kali ambayo huchangia ongezeko la magonjwa ya saratani ya matiti na
mlango wa uzazi kwa akinamama huku akiwahimiza kufanya uchunguzi angalau mara
moja kwa mwaka ili kubaini tatizo mapema kwani tiba ya mapema husaidia
kupambana na magonjwa hayo.
Chama cha Madaktari Wanawake nchini kimeshirikiana na Wizara
ya Afya, Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza pamoja na wadau wengine wakiwemo
Gender Health, PSI pamoja na Tayoa katika kufanikisha huduma hiyo ya uchunguzi
na matibabu ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi bila malipo mkoani
Mwanza.
No comments:
Post a Comment