Marehemu Revocatus Bulizya enzi za uhai wake
Jeneza likiingizwa kanisani.
Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili huo.
Wanahabari wa Sahara Media alikokuwa akifanya kazi marehemu katika Kituo cha Televisheni cha Star TV na ndugu jamaa wa marehemu wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wanahabari wakiandika wasifu wa marehemu Revocatus Bulizya.
Wanahabari Kibwana Dachi (kulia) na Ben Mwanantala
wakiwa kwenye ibada hiyo.
Katekista wa Parokia ya Muhimbili akiongoza ibada hiyo.
Ni huzuni katika ibada hiyo.
Na Dotto Mwaibale
VILIO na majonzi vilitawala wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari Revocatus Bulizya wa Kituo cha Televisheni cha Star TV wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Kanisa Katoliki la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam leo asubuhi.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali akiwepo aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam toka mwaka 2010/2015, Shelymar Kweygia ambaye ni ndugu ya mke wa Bulizya.
Akitoa mahubiri wakati wa ibada hiyo Katekista wa Paroko ya Kanisa Katoliki MNH, alisema ni wakati wa kila mmoja wetu kutafakari juu ya maisha yake ya kimungu.
Alisema hakuna njia ya kukutana na mungu bila ya kifo na ndio maana wakati wote tunatakiwa kujiandaa kwa sababu hatui ni lina tutatoweka duniani kama alivyotuacha ndugu yetu Revocatus Bulizya.
Recocatus Bulizya alzaliwa tarehe 29-10-1979 na kufariki dunia tarehe 2-5-2017 kwa kugongwa na pikipiki 'bodaboda' maeneo ya Pugu jijini Dar es Salaam wakati akirejea nyumbani kwake akiwa ameongoza na mke wake.
Mazishi ya marehemu yamefanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa nje kidogo ya jijini Dar es Salaam na mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.
No comments:
Post a Comment