Showing posts with label Msiba Kifo. Show all posts
Showing posts with label Msiba Kifo. Show all posts

Saturday, February 26, 2022

Agnes Trip Killing Brings Awareness to Domestic Violence and Sexual Abuse in Kenya



                       AGNES TIROP 1995-2021

By MUTWIRI MUTUOTA and GERALD IMRAY

Associated Press ELDORET, Kenya (AP) -  The brutal killing of Olympic runner Agnes Tirop last year shows signs of being a turning point for Kenya in finally confronting a scourge of abuse and violence against female athletes. It hasn't been spoken about or even acknowledged until now. The 25-year-old Tirop was stabbed to death at her home last October. Her partner has been charged with murder in her killing. Her death provoked a deep reckoning in Kenya and prompted current and former athletes to finally speak out and put pressure on authorities. They say young female athletes have been abused by partners, coaches and others for years and their stories have gone untold or been ignored.


Thursday, January 02, 2020

Tanzia - Bibi Jeredina Paulo Suka Haule

Ninasikitika kutangaza kifo cha ndugu yangu, Bibi Jeredina Paulo Suka Haule, kilichotekea, Janauri 1, 2020, huko kijijini, Ilela, Manda, Tanzania. Alikuwa mama Mzazi wa Stephen Challe na Burton Challe.

Bibi Suka amekwisha lazwa katika nyumba yake ya milele. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.





Bibi Jeredina Paulo Suka Haule
October 28, 1928 to January 1, 2020

Mimi na Bibi Suka (mwenye ndoo)  kijijini Ilela mwaka 2009

Bibi Suka na baadhi ya wajukuu wake mwaka 2014

Misa ya Kumwombea Bibi Suka Kanisa Anglikana Ilela



Saturday, May 13, 2017

Tanzia - Mh, Said Thabith Mwambungu

 
The late Regional Commissioner Said Thabith Mwambungu
 
Kutoka kwa mwandishi mahili  Nickson Mkilanya 
 
 KWAHERI YA KUONANA RC SAID THABITH MWAMBUNGU
 
Amefariki leo katika hospitali ya taifa ya muhimbili,hatunaye tena, Said Thabith Mwambungu mkuu wa mkoa mstaaf na miongoni mwa wanasiasa wabobezi na wakongwe katika zama hizi.
Ameripotiwa kusumbuliwa na ugonjwa wa figo kwa siku kadhaa hata akapelekwa kutibiwa nchini India na kurejea na nafuu ambayo pia haikupata kumrejesha katika majukwaa ya siasa na hata hadharani.
 
Kuugua huko pasipo kutajwa kuwa ndiyo sababu iliyopelekea rais Magufuli kumhamishia ofisi ya waziri mkuu na kuahidi kumpangia kazi zingine toka juni 26 mwaka jana lakini nafsi yangu yakiri kuwa pengine hiyo ndiyo sababu kuu.
 
Alilitamka kwa ufasaha jina lake la said said thabith mwangu enzi za uhai wake hasa pale nilipofanyakazi naye mimi nikiwa kama mwanahabari wa luninga,radio na hata magazeti, ni mzaliwa wa Malinyi mkoani Morogoro ambaye kwangu mimi ni miongoni mwa wanasiasa bora,baba Bora na kielelezo cha watu wema na wastaarabu niliopata kukutana nao.

Miongoni mwa mambo aliyoyaacha km funzo kwangu ni uvumilivu na upendo. Wakati mmoja akiwa mkuu wa wilaya kuna kiongozi mmoja alimfanyia figisu figisu nyingi ambazo hata wanahabari tuliona na kugundua akionewa dhahiri! Lakini tulipoongea naye jibu lake alijibu kuwa mwacheni tu huyo, hayo ni yakupita, hajui siasa, vumilieni yataisha na kweli huyo mtu alikuja ondolewa ktk nafasi na kumwacha mwambungu akitamba na siku chache baadae kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa ruvuma.
 
Jambo lingine alijua kuthamini watu na kuwaonesha upendo wa dhati hata wale ambao kwa tabia za kibaguzi wasingepaswa kumsogelea lkn bado aliwapa nafasi sawa na wale ambao kimtazamo walikuwa na sifa ya kumsogelea. Nakumbuka wakati mmoja aliniambia nick mwanangu fanya mpango uoe nikufanyie sherehe kabla sijaondoka na hapa alimaanisha kabla hajahamishwa kituo cha kazi nami nilicheka na kuahidi kufanya hivyo lkn leo hatunae tena ameondoka mwambungu pasipo kushughudia harusi yangu.
 
Amini mungu ni mwema wanae wakiongozwa na hamidu mwambungu watashughudia harusi yangu kwa niaba yake inshallah.
 
Wakati wa uhai wake alipata kuwa kada mwandamizi katika ccm, katibu wa chama cha mampinduzi mkoa,  mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa achilia mbali nafasi zingine nyeti ndani ya nchi hii, Na ameacha watoto watatu, hamidu said said thabith mwambungu, Khalid na Abiba S. S Thabith mwambungu na mjane.
 
 Mtoto mkubwa wa marehemu  aitwae Hamidu Mwambungu anasema haijaamuliwa bado kama baba yao atazikwa morogoro au kwingineko.
 
Tangulia mtu mwema Said Said Thabith Mwambungu.

Saturday, May 06, 2017

Buriani Mwanahabari Revocatus Bulizya

Marehemu Revocatus Bulizya enzi za uhai wake
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Revocatus Bulizya wakati ukiingizwa katika Kanisa la Katoliki Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya ibada ya kuuaga kabla ya kwenda kwenye mazishi yaliyofanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.

Saturday, July 18, 2015

Mwimbaji Banza Stone Afariki Dunia

The Late Ramadhani Masanja aka Banza Stone
Mwimbaji maarufu Banza, Stone (42). amefariki dunia leo hii nyumbani kwake Sinza, mjini Dar es Salaam.  Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema poponi. Amen.



Kutoka THE CITIZEN


Dar es Salaam. Veteran dance musician Ramadhan Masanja aka Banza Stone, 42 (pictured) was yesterday afternoon pronounced dead at his family home in Sinza Dar es Salaam after a long illness.
After several false alarms about his death, the news was confirmed by his elder brother, Mr Jabir Masanja, who said the singer had been admitted to Mwananyamala Referral Hospital in Dar es Salaam.
The real cause of his death was not clear at the time we went to press, but in an earlier interview, Banza, who had been restricted to his bed, complained of a severe headache.
The ailment rendered the singer unable to walk or even feed himself properly without support.
News of the singer’s demise hit the social media at about 2.00pm with his legion of fans sending condolence messages to his family.
Radio DJ Fetty and presenter Anna Peter wrote on their Twitter accounts: RIP Banza Stone.
More condolence messages were from Mwana FA, Izo Bizzo and many others who expressed the loss of Banza Stone who many considered as dance music icon.
The singer whose career took off in the early 1990s was famed for hits such as ‘Mtu Pesa’, ‘Angurumapo Simba’,’Mtaji wa Maskini’ and ‘Elimu ya Mjinga’.
In a career that spanned over 20 years, Banza Stone ventured into music at an early age just after he had completed his elementary education in 1987 despite his parents’ disapproval  .
But his real debut into music was in 1990 after his earlier attempts to do hip hop proved futile.
Though many know him for his efforts that catapulted him to fame while at TOT Plus, before he made a career move to The African Stars ‘Twnga Pepeta and later Extra Bongo, he had worked with smaller bands before.
His struggles to make it took him to bands such as  The Heart Strings, Twiga Band, Achigo Band as a drummer and Afri-Swez.


Sunday, May 24, 2015

Mama Bishanga Afiwa na Kaka Yake - Casim Jaffer Manji

MAMA BISHANGA AMLILIA KAKA YAKE CASIM JAFFER MANJI

Leo hii tarehe 23/05/2015 asubuhi ya Tanzania nimefiwa na kaka yangu mkubwa Bw Casim Jaffer Manji (Jalejale) Kongowe kwa binti yetu Anna Kepha mtoto wa marehemu dada Mwl Cecilia Hatia.
Napenda kutumia nafasi hii kumjulisha Abasi Manji na akina Manji wa DSM. Familia ya Jaffer Manji wa Bombey, wadogo zangu Dr Geofrey Hatia Nambira wa Namibia, Isaya Hatia wa Finland, na aunt Eva Mack Hatia wa Finland. Familia ya marehemu mzee Abdruhaman Bellim, familia ya mzee Abdala, mzee Jalabi, na shangazi Anna Mchauru wa Masasi ya zamani na Mkuti, ukoo wa che Mbungo wa Lukuledi Masasi, na ukoo wa Hatia wa Ndanda. Na Deo mwalujua na familia yake wa Columbus Ohio.

Kwa taarifa za mipango na ratiba ya mazishi wasiliana na

Mwl Mack Hatia wa Azania sekondari 225 0754 290 013
Kilian kamota 225 653 0763 200
Constancia Hatia (Mrs Solmon) 225 0712 555 966
Musa Kamota 225 075 609 370 
Fidelis Mrope 225 0713 410 321 
Hendrich Nambira (Kenny) 225 0715 965 321
Joseph Hatia (Ndugu) 225 0713 987 173

Mungu amempenda Zaidi kaka yetu. Tushukuru kwa yote.

Mama Bishanga / Mrs Marolen

Ohio / USA

Saturday, February 21, 2015

Bongo Fleva Staa Mez B Afariki Dunia!

Kutoka Facebook 

Msanii wa Bongo fleva  Moses Bushagama  aka. 'Mez B'  amefariki Dunia Ijumaa, February 20, mkoani Dodoma kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu. 

Mez B alikuwa ni mtoto wa pekee kwa mama yake kwani alizaliwa peke yake. Rest in Peace.


The Late Mez B