Mjumbe wa halmashauri Kuu (CCM) Mkoa wa Iringa, Leah Mwamoto akiongea na wazazi wa shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakicheza nyimbo mbele ya mgeni Rasmi
NA FREDY MGUNDA,KILOLO
Mjumbe wa halmashauri Kuu (CCM) Mkoa
wa Iringa, Leah Mwamoto amewaonya wazazi wanaokatisha masomo watoto kuwa
serikali itawachukulia hatua kali pindi watakapobainika kufanya kosa hilo.
Mwamoto ameongea hayo katika mahafali
ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika kijiji cha
Mlafu wilayani Kilolo alipomuwakilisha mbunge wa jimbo la Kilolo Venance
Mwamoto.
Akiwaonya wazazi katika mahafali hayo
Mwamoto amewaeleza wazazi juu ya mazingira mabaya wanayoyakuta watoto
wanaokwenda kufanya kazi za ndani katika miji mikubwa.
Hata hivyo amewaomba watendaji wa
kata kuendelea kuwafutilia watoto ili kuwaepusha kujiingiza katika mazingira
hatarishi yatakayoharibu ndoto zao.
Aidha Mwamoto amepongeza uongozi wa
shule ya sekondari Mlafu kwa matokeo mazuri pamoja na mbunge wa jimbo la
Kilolo, Mhe Venance Mwamoto kuchangia bati 180 na mifuko 100 ya saruji kwa
ujenzi wa zahanati kijiji cha Mlafu.
Awali akisoma taarifa fupi ya shule
mwalimu mkuu wa shule hiyo Emmanuel Mbangwa ameomba wadau kujitokeza kuboresha
mazingira katika shule hiyo hususani kujenga nyumba za walimu na mabweni.
Nae diwani Mlafu Isidory Kiyenge
amewataka wazazi wa kata hiyo pamoja na wadau kuwa tayari kuchangia katika
sekta ya elimu ili kuongeza mazingira ya ufaulu.
Kayenge amewataka wanafunzi kujiandaa
kwa mitihani ya kidato cha nne huku alito ahadi ya kuwaandalia chakula wakati
wa mitihani.
No comments:
Post a Comment