Saturday, March 27, 2021

Concussion Awareness - Habari Zaidi - Ubongo ukiumia




Wangapi mmeanguka na kupoteza fahamu kwa muda?  Au baada ya kuanguka unajiona unazimia zimia

Ni kutokana na kitu kinaitwa Concusssion. Yaani ubongo  unapata shot vile.  Mara nyingi wana michezo waanaathirika, na wanaopata ajali wanaathirika.

Mnaweza kusoma kuhusu Concussion  KWA KUBOFYA HAPA:

Snowboarding Concussion (Everything You Need to Know) (snowboardhow.com)



Kumbuka msanii Steven Kanumba alikufa kwa Concussion baada ya kuanguka na kugonga kichwa nyumbani kwake.  Mnaweza kusoma kuhusu kifo cha Kanumba  KWA KUBOFYA HAPA:

http://swahilitime.blogspot.com/2012/04/kanumba-alikufa-kwa-brain-concussion.html


Saturday, March 20, 2021

Mh. Samia Suluhu Hassan Aapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania

Kutoka BBC SWAHILI

Samia Suluhu Hassan aapishwa kuwa Rais wa Tanzania na Jaji Ibrahim Juma katika Ikulu ya Jijini Dar es Salaam.

Mama Samia ameapishwa katika hafla ndogo iliyofanyika katika Ikulu ya Magogoni na kuhudhuriwa na marais wastaafu wa Tanzania na Zanzibar.

Mara baada ya kuapishwa alipigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride maalumu kwa mara ya kwanza akiwa kama amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Mama Samia mwenye miaka 61, ndio mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huu nchini Tanzania na wa pili Afrika Mashariki.




Wednesday, March 17, 2021

Rais John Pombe Magufuli Afariki Dunia!



KUTOKA GAZETI LA MWANANCHI 

 Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo cha Rais Magufuli, zilitangazwa jana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo akisema Magufuli alifariki dunia saa 12 jioni kwa maradhi ya moyo baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Machi 6.

Amesema awali, Rais Magufuli alifikishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Machi 6 akisumbuliwa na tatizo la moyo la mfumo wa umeme ambalo alikuwa nalo kwa zaidi ya miaka 10.

“Machi 14 mwaka huu, alijisikia vibaya akakimbizwa hospitali ya Mzena ambako aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete hadi umauti ulipomkuta,” amesema Mama Samia.

Amesema Tanzania itakuwa katika kipindi cha maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti. Alisema wananchi watajulishwa juu ya taratibu za mazishi za kiongozi huyo mkuu wa nchi.