Saturday, April 17, 2021

Buriani Prince Philip (1921-2021) - Mume wa Malkia wa Uingereza

 Leo  mume wa Malkia wa Uingereza, Prince Philip, amezikwa katika kanisa la Mt.George huko Windsor Castle, Uingereza.  Prince Philip alifaikri tarehe 9 Aprili akiwa na miaka 99.  Alikuwa mume wa Malkia Elizabteh kwa miaka 73. 

Niliwahi kuongea na Prince Philip. Mwaka 1979, nikiwa mwanafunzi wa  shule ya sekondari Zanaki,  tulikuwa Ikulu, kuwapokea.  Enzi zile, kama anakuja kiongozi wa nchi ya nje, wanafunzi walikuwa wanatumiwa kupanga  njia kumlaki   

Basi, malkia na familia yake walishuka kwenye gari, na walitembea kwa miguu kwenye  kapeti nyekundu kuingia Ikulu.  Prince Philip alisimama, na kutangalia sisi wanafunzi.  Akauliza,  nyie ni wanafunzi wa shule gani, kwa Kiingereza,  Wanafunzi waliokuwa karibu na mimi walikimibia.  Nikamjibu,  " We are students from Zanaki Girls Secondary School.  (sisi ni wanafunzi kutoka shule ya sokndari Zanaki".  Akauliza  shule ilikuwa inaitwa nini zamani, nikamwambia, Aga Khan Girls.  Alisema  asante, na kuendelea kuingia Ikulu.  Doh!  Niliongea na Royalty!  nilirudi yumbani kwa furaha na kuwasimulia wazazi wangu na marafaiki jinis nilivyoongea na Prince Philip.

Kwenye ziara ile ya mwaka 1979, Malikia alisali na sisi, katika Kanisa la Mt. Albano, Dar es Salaam.  

Mungu ailaze roho ya marehemu Prince Philip.  

Kuona video fupi ya ziara ya Malkia Elizabeth II na familia yake East Africa mwaka 1979  BOFYA HAPA:

 Wanafunzi na wakazi wa Dar es Salaam, wakiwashangalia Malkia Elizabeth na familia yake wakielekea Ikulu alipotembelea Tanzania mwaka 1979,


Malkia Elizabeth II na hayati Prince Philip wakiwapungia waTanzania baada ya ziara yao mwaka 1979.


Maisha ya Prince Philip

No comments: