Showing posts with label Accident. Show all posts
Showing posts with label Accident. Show all posts

Saturday, August 10, 2019

Uchu wa Mafuta yaua watu zaidi ya 70 Morogoro - Ajali ya Lori la Mafuta

Jamani wadau, mkiona  mafuta yanavuja kutoka kwenye gari kimbia, siyo mnakimbilia kupata mafuta dezo!  Yanawaka kwa kirahisi mno. Umaskini kitu kibaya sana, maana si ajabu wengine waldihani watuuza hayo mafuta wapate hela ya ugali!   Ona sasa watu zaidi ya  sabini wamepoteza maisha baada yakuungunguzwa! 

Wengine waliokufa ni madereva wa bodaboda na mama nitilie!  Walizoa mafuta hata kwenye ndoo! Na wanasema, mafuta yalilipuka baada ya mtu kuchomoa  betri 
ya lori  na mtu mwingine alikuwa anavuta sigara!   Nasikia huyo mvuta sigara aliambiwa asivute karibu na mafuta.  Alijibu mafuta ya kisasa hayawezi kuwaka moto! Nadhani watakuwemo kwenye watu waliokufa!
Mungu alaze roho za waliokufa mahala pema mbinguni. Amen.


Kutoka Associated Press
DAR ES SALAAM, Tanzania (AP) — A damaged tanker truck exploded in eastern Tanzania as people were trying to siphon fuel out of it Saturday, killing at least 62 in one of the worst incidents of its kind in the East African country.
Tanzanian state broadcaster TBC, citing police figures, said at least 70 more people were injured during the explosion in the town of Morogoro, located about 120 miles (200 kilometers) from the economic hub of Dar es Salaam.
Regional police commissioner Steven Kabwe told the local Azam TV that many suffered serious burns.
Witnesses told The Associated Press that a crowd had gathered around the fuel tanker after it was involved in an accident early Saturday and some people were trying to siphon away fuel when the truck burst into flames.
Video footage posted on social media showed people collecting fuel into jerry cans before the fire incident.
In a statement expressing condolences, Tanzanian President John Magufuli said he was dismayed people attacked vehicles involved in accidents instead of offering help.
Residents are routinely killed by explosions while stealing fuel from incapacitated tankers in East Africa. Those who steal the fuel usually hope to be able to sell it cheaply to motorists.
In 2013, at least 29 people were killed on the outskirts of the Ugandan capital, Kampala, as scores swarmed around the scene of an accident.
There is limited awareness about the danger of explosions of damaged fuel tankers, said Henry Bantu, a road safety expert who runs the Tanzania-based Safe Speed Foundation. Local leaders need to do more to educate people on the risks, he said.



Watazamaji kwenye shemu ya mlipuko Morogoro

Monday, September 07, 2015

Rais Kikwete Awapa Pole Majeruhi wa Msongamano

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Hassan BAntu alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
 Mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi Flora Maduka akiwa kitandani pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika msongamano huo
 Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi. Jalia Mohamed akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete akiendelea kutoa pole kwa majeruhi
 "Pole sana...." Rais Kikwete akimfariji mmoja wa majeruhi

 Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyeungua kwa moto
  Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyevunjika mguu wakati akicheza kwenye mti
Rais Kikwete akimpa pole mvulana ambaye aligongwa na gari wakati akielekea kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana 
Rais Kikwete alipata fursa ya kutembelea wodi ya watoto na kuwapa pole kwa kuumwa kwao
Rais Kikwete akiongea na wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo kumtembelea mgonjwa
Rais Kikwete alizongwa na wananchi waliokuwa na hamu ya kuongea naye 
Rais Kikwete akitoa mapendekezo ya kupanua hospitali hiyo ambayo ina eneo kubwa lakini majengo machache ya chini. Alipendekeza uongozi wa hospitali na mkoa ubuni namna ya kuipanua kwa kujenga majengo ya ghorofa ili kuwepo na wodi na sehemu nyingi zaidi za huduma.
Mwishoni Rais Kikwete aliongea na wanahabari wa kutoka vyombo mbalimbali na kueleza masikitiko yake kwa yaliyotokea jana Uwanja wa Jamhuri baada ya mkutano wa kampeni kumalizika.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya baada ya kuwajulia hali majeruhi wa msongamano baada ya mkutano wa kampeni uwanja wa Jamhuri Morogoro jana. PICHA NA IKULU