Scene from AftershockHabari zenu wapendwa wasomaji? Leo nawajulisha kuhusu sinema inaitwa
Aftershock. Film iko sponosred na History Channel na itaonyeshwa kwenye
History Channel. Niliwajulisha kuwa nilifanya audition kupata nafasi ya kuigiza kwenye hiyo sinema. Sikupata pati niliyofanyia audition lakini nilipata part nyingine.
Basi juzi nilienda kwenye filming huko Sutton, Massachusetts. Ni kama maili 50 kutoka Boston. Eneo enyewe ni shamba kabisa. Yaani niliposhuka kwenye gari nilifurahi kuona miti mingi, majani, sungura, kuku wanatembea wanavyotaka! Upepo ulikuwa freshi kabisa safi mno! Ama kweli kukaa mjini kunachosha.
Haya kufika kwenye seti ya film, walikuwa wameweka matenti. Moja ya chakula, moja ya make-up, nyingine ya vifaa. Gereji ya nyumba iligeuzwa 'wardobe' (nguo). Nilenda sign-in halafu moja kwa moja nilipelekwa wardrobe kuvalishwa costume. Role yangu ni 'farm hand ' yaani ni 1867 Utumwa umeisha lakini weusi wanaajiriwa kwa hela ndogo sana, na bado kuteswa na kuuliwa ovyo. Walinivalisha sketi nyeusi ndefu, apron, sharti ya dume! Sikuvaa viatu. Baada ya hapo nikaenda make-up. Kwenda huko walinipaka make-up ya uchafu! Kwa kweli ukiona picha zangu kwenye hiyo seti mini na wenzangu ni wachafu kweli kweli! Tulikuwa wachafu mpaka watu walituogopa! Tulikuwa wachafu maana tulikuwa tunalima shamba, na ilikuwa na matope shauri ya mvua! Udongo ulikuwa umejaa wadudu na minyoo wale wakubwa wakubwa (earthworms).
Halafu kulikuwa na farasi mkubwa kweli kweli! Alikuwa anaitwa Barney! Basi alikuwa anapita karibu sana kwangu lakini ali-behave. Tukaanza kuwa marafiki mpaka hapo walipoanza kufyatua marisasi na kaanza kushutuka! Ikabidi wamwondoe kwenye seti. Kaanza kutoka mapovu mdomoni kwa woga!
Niliumwa na mdudu kwenye mguu walimeta EMT (paramedic)! Fikiria walikujwa na huduma ya 911 hapo hapo! EMT’s wawili walikuwa assigned kule kwa shoot yote, pamoja na zimamoto na polisi!
Nitawajulisha zaidi...