Showing posts with label Askofu Kakobe. Show all posts
Showing posts with label Askofu Kakobe. Show all posts

Friday, June 28, 2013

Mama Aliyetembea Baada ya Miaka 18 Kwenye Wheelchair



Huyo Mama alikuwa kwenye wheelchair miaka 18. Utaona  anatembea na lazima atahitaa mazoezi zaidi ili aweze kutembea vizuri. Iliktokea kwenye Bishop Kakobe's Toronto Miracle Healing Crusade, Saturday 6/22/13/

Watu Wangapi Walihudhuria Mkutano wa Askofu Kakobe Toronto?

Naona kumekuwa na maswali mengi kuhusu watu wangapi walihudhuria Mkutano wa Askofu Kakobe mjini Toronto. Idadi ya kweli ni maelfu, lakini wengine eti kwa kutizama picha wananipinga wanasema mamia.  Kwanza, hamkumwepo, mimi nilikuwepo.

Ile Rexall Tennis Center ina chukua watu 10,000 (capacity). Ni kweli aikujaa.  Lakini kila siku watu 2,000-3,000 walihudhuria. Parking lot zilijaa, kulikuwa na polisi wa kuongoza trafiki.  Pia Paramedics (kuhudumia Wagonjwa walikuwepo wanne kila siku).  Picha nilipiga lakini hazikutoka vizuri za hao Paramedics. Pia sikuona mtu aliyeenda kupata huduma yao, walienda kwa kwa Askofu.

Wakati Askofu alivyoomba watu waende kumpokea Bwana Yesu ni mamia walioenda kwa vile wengine wengi walikuwa wamekwishampokea.

Watu walikuwa wanakaa sections fulani, ndo maan zingine zilikuwa tupu. Niliona watu wa kila rangi pale, na hata waislamu. Ile stadium ni kubwa. Labda mwaka wataijaza. Pia hakuna fujo iliyotokea pale. Mambo yalienda vizuri sana.

Roho ya Bwana Yesu ilikuwepo pale Rexall.  Amen.   Askofu aliwaombea wafanyakazi wa pale Rexall na mji wa Toronto kwa ujumla. 

Monday, June 24, 2013

Askofu Kakobe Amaliza Ziara Yake Toronto, Canada

Wadau, nimekuwa hapa Toronto, Canada kwenye mkutano wa Askofu Kakobe. Maelfu ya watu wa kila rangi na hata waislamu walitokea. Kulikuwa na wahindi, wachina, wakorea, wazungu pamoja na waafrika wengi. Tumeshuhudia miujiza!  Jana kijana wa kiChina aliyekuwa kwenye wheelchair aliweza kutembea. Bibi ambaye alikuwa kwenye wheelchair miaka 18 aliweza kutembea, viziw walisikia!  Watu waliolewa mapepo! Hapa Toronto, Askofu Kakobe amefanya mengi! Mkuanta huo ulikuwa  June 20-23, 2013 Rexall Centre, York University.  Kweli Mungu anamtumia Askofu Kakobe!

Nimepiga picha hizi kwenye mkutano jana na juzi.





Askofu Kakobe Jukwaani

Walioamua kuokoka

Tuesday, January 05, 2010

TANESCO Mwogopeni Mungu!!!!

(Pichani: Askofu Zakaria Kakobe Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam)

KAZI IPO!!!! Naona hii miaka ya karibuni wanazidi kumsumbua Askofu Kakobe!

****************************************************

Kutoka ippmedia.com:

Na Joseph Mwendapole

5th January 2010

Waumini wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship, lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam, wameanza kulinda mabango yao kwa saa 24 na wameapa kuwa iwapo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) litajaribu kuyaondoa patachimbika.

Akizungumza jana na Nipashe kwenye Kanisa hilo, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Zacharia Kakobe, alisema vijana wake wamehamasika na wameamua kulinda kanisa lao kwa saa 24 hivyo Tanesco wasijidanganye kuwa wanaweza kuyaondoa mabango hayo.

"Vijana kama unavyowaona wako hapa kwa saa 24 kuhakikisha tingatinga likija kutaka kuyaondoa halifanikiwi maana huu ni uonevu dhidi ya Kanisa, na wamevaa sare ili iwe rahisi kutambulika kuwa ni waumini wa hapa," alisema Kakobe.

Fulana walizovaa waumini hao zilikuwa zimeandikwa “Tanesco mwogopeni Mungu, baada ya Richmond sasa mmeligeukia kanisa”.

Askofu Kakobe alisema mabango hayo yametengenezwa kwa Sh. milioni 120.

Alisema Tanesco ilijaribu kupitisha nyaya hizo upande wa pili lakini baada ya kujadiliana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilikataa baada ya kubaini hatari ya kupitisha umeme huo mkubwa karibu na makazi ya watu.

"Wasomi walikataa maana wanaujua umeme na madhara yake, sasa walipoona wameshtukiwa kule wakaona waje wapitishe huku kwetu ambako walidhani waumini ni watu wasiojua kitu, cha kushangaza walianza kwa kutwambia kuwa umeme huo hauna madhara baadaye wakasema wakishaweka nyaya zao itabidi mabango haya yaondoke maana ni hatari yakiendelea kuwepo sasa wanajichanganya wenyewe," alisema na kuongeza kuwa yeye ni msomi wa sayansi na anaufahamu vilivyo umeme.

Alisema shirika hilo limekuwa likitoa fidia tangu Ubungo zitakazopita nyaya hizo lakini walipofika kwenye Kanisa hilo hawakuona hata umuhimu wa kuzungumza na waumini ili kufikia muafaka.

Tanesco imeshasema kuwa itatekeleza mpango huo mapema mwaka huu, baada ya utafiti wa wataalamu na ushauri wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kwamba hauna madhara kwa wakazi wa eneo hilo.

CHANZO: NIPASHE