Friday, June 28, 2013

Watu Wangapi Walihudhuria Mkutano wa Askofu Kakobe Toronto?

Naona kumekuwa na maswali mengi kuhusu watu wangapi walihudhuria Mkutano wa Askofu Kakobe mjini Toronto. Idadi ya kweli ni maelfu, lakini wengine eti kwa kutizama picha wananipinga wanasema mamia.  Kwanza, hamkumwepo, mimi nilikuwepo.

Ile Rexall Tennis Center ina chukua watu 10,000 (capacity). Ni kweli aikujaa.  Lakini kila siku watu 2,000-3,000 walihudhuria. Parking lot zilijaa, kulikuwa na polisi wa kuongoza trafiki.  Pia Paramedics (kuhudumia Wagonjwa walikuwepo wanne kila siku).  Picha nilipiga lakini hazikutoka vizuri za hao Paramedics. Pia sikuona mtu aliyeenda kupata huduma yao, walienda kwa kwa Askofu.

Wakati Askofu alivyoomba watu waende kumpokea Bwana Yesu ni mamia walioenda kwa vile wengine wengi walikuwa wamekwishampokea.

Watu walikuwa wanakaa sections fulani, ndo maan zingine zilikuwa tupu. Niliona watu wa kila rangi pale, na hata waislamu. Ile stadium ni kubwa. Labda mwaka wataijaza. Pia hakuna fujo iliyotokea pale. Mambo yalienda vizuri sana.

Roho ya Bwana Yesu ilikuwepo pale Rexall.  Amen.   Askofu aliwaombea wafanyakazi wa pale Rexall na mji wa Toronto kwa ujumla. 

16 comments:

Anonymous said...

Asante sana kwa kazi nzuri Dada Chemi. Mungu akubariki sana. Achana na Doubting Thomas Bwana Yesu anajua ukweli.

Anonymous said...

Tatizo la wabongo ni wivu na fitina. Ndo maana nchi yetu haiwezi kuendelea. Mwache mtumishi wa Mungu Askofu Kakobe afanye kazi yake. Kama Tanzania hatuwezi kumthamini wenzetu nje ya nchi watamthamini!

Agano said...

Nchi yetu itaendelea kwa kuamini upumbavu wa mtu kupona ulemavu kwa jina la yesu? Tatizo lenu ni kwamba hamna uhakika wa mnachokiamini na ndiyo maana mpo "desperate" kuona miujiza ili muweze kuamini mnachotaka kuamini. Na kwa kuwa miujiza haitokei, basi mnaitengeneza miujiza akilini mwenu na mnaamini uongo wenu wenyewe. Huyo Chemi aliyekuwepo hapo kwa kakobe anaelewa fika kwamba hakuna kiwete wala kipofu aliyepona hapo, lakini hatosema ukweli kwa sababu ameshamuweka kakobe katika "pedestal" na anamuona kakobe ni muwakilishi wa mungu hapa duniani.
Ukweli ni kwamba hii ni Loliondo ya kiingereza tuu.

Agano said...

Wandugu; kuweni makini na huyu dada yenu Chemi. Simtukani, lakini Chemi hajatulia akilini. Natoa ushahidi ufuatao.

Kwenye blog yake hii tarehe 31 Machi 2011 aliandika yafuatayo.

"Wadau, Nimepigiwa simu na rafiki yangu Tanzania kuwa Babu wa Loliondo amekubali kufika Dar na kutibu wagonjwa. Huduma itakuwa kwenye viwanja wa Jangwani. Tarehe bado haijatangazwa lakini utaratibu wa kugawa vikombe itakuwepo. (Natumaini siyo utani wa April Fools) "

Wadau, kama hii haitoshi kujua akili za chemi, basi angalia hapa chini.

Thursday machi 24, 2011 aliandika kwenye blog yake haya yafuatayo.

"Wadau, naona vigogo wanakimbilia Loliondo kupata 'kikombe cha dawa'. Je, walipanga foleni na wengine au walipata 'bump'? Pia, eti kuna uvumi (au huenda ni kweli) kuwa Mzee Mandela wa Afrika Kusini naye alienda huko kisirisiri kupata kikombe. Kama hiyo dawa kweli inafanya kazi basi huyo babu apatiwe ulinzi mkali hata wa FFU 24/7. Maana wazungu wakipata fununu watamwua. Kisa makampuni ya madawa (Pharmacueticals) watafilisika kwa kukosa wateja.

Dawa ya babu OYEEEEE!"

Haya sasa iliyobaki mtajaza wenyewe.

Chemi hata usipotundika maoni haya, lakini nadhani yatakusaidia kuweza kufikiri.

Chemi Che-Mponda said...

Mdau Agano, asante kwa mchango wako. Bado namheshimu Babu wa Loliondo na Mungu akinibariki nitaenda kupata kikombe.

Lakini leo namzungumzia Askofu Kakobe ambaye nilimshuhudia mwenyewe akimponyesha baba MNigeria aliyekuwa ameumia mgongo mwaka 1999 alipokuja Boston. Yule baba ni mzima hadi leo, na kila akiniona lazima aniuliza habari za The Man of God Askofu Kakobe. Imani ni kitu kikubwa sana, kama huna basi waache wenzako wakae na imani zao. Kuhusu yule MNigeria nilikuwa namfahamu kabla hajapata ajali na nilimshauri aende kwa Kakobe atakapokuwa Boston. Alienda na kapona. Alitupa magongo yake hapo hapo. Mungu yu Mwema!

Na kuhusu picha za Before and After Toronto, zipo, wapiga picha walikuwa wengi.

Anonymous said...

Damu ya Yesu Kristo ni nzito. Hata Agano atasemehewa. Amina.

Anonymous said...

Dada Chemi umefanya kazi yako nzuri ya kumhubiri Yesu kwa kushuhudia matendo yake aliyofanya huko Toronto. Kutokuamini kwa baadhi ya watu kusikusumbue kwasababu wengine wamejaa wivu kama mafarisayo. Ipo siku watajua kuwa Yesu ni Bwana.

Anonymous said...

Agano!!! , wewe ulikuwepo Toronto? Tuambie basi yaliyojiri huko Toronto, maana unatoka mapovu sana au ndo shetani amekasirika kwasababu kazi zake mbovu zimeharibiwa vibaya? Angalia usijekuwa unatumiwa na shetani pasipo wewe mwenyewe kujijua.

Agano said...

Chemi, kuna neno wazungu wanalitumia linaitwa "anecdote". Juzi uliweka picha ya mchina kwamba amepona ukiwete, na leo unaleta ya mnijeria kupona mgongo. Hizi zote ni "anecdotes". Kama ni kweli tuwekee ushahidi hapa.

Kwa wale mnaosema natoka povu; mimi sikuwepo toronto, lakini nimeshawahi kuhudhuria mkutano wa kakobe viwanya vya jangwani mwaka 1995 nikiwa form 3. Wazungu wana msemo wao wanasema "fool me once shame on you, fool me twice shame on me". Kakobe will fool some people all the times but not all the people.

Agano said...

Chemi, nenda tuu ukapate kikombe cha babu yako. Ninachoelewa ni kwamba babu hagawi kikombe siku hizi; Sasa labda kama wewe unataka kumpelekea babu kikombe akakijaze dawa yake.

The truth is desperation won't turn fantasy into reality. If indeed visiting a scammer who put together a monumental deception to the detriment of innocent lives is something to be proud of, then goodluck to you.

Anonymous said...

Agano,

Povu linakutoka la nini, kutokuamini kwako hakubadilishi ukweli kuwa , Askofu Kakobe ni mtumishi wa Mungu, na wapo wanaopona kwa jina la YESU, sio tu miili yao lakini muhimu zaidi watu wanapona roho zao kwa kuokoka na kubadilishwa maisha kuwa mbali na dhambi. Mtu yeyote anayepinga kazi hii ya kuwatoa watu katika hatari ya kutupwa jehanam ya moto na kubadilishwa maisha kumuelekea Mungu aliye hai katika YESU, atakuwa ni ajenti wa ibilisi. Ni kama wale wanaokataa kwamba baada ya kufa watenda dhambi hawataenda motoni, unaweza ukakataa leo, lakini baada ya kufa utakapokuwa unachemka motoni ndio utajua kama moto upo au la.

Anonymous said...

Watu wenye roho za wivu za kaa kama ndugu Agano, hawawezi kuzuia kazi ya Mungu kusonga mbele. Kwa nini roho inakuuma hivi mtumishi wa Mungu akienda kufanya kazi ya Mungu? wewe umeamua kuwa mpagani na kutokuamini kazi za Mungu, na kumuona Mungu ni kama wewe mwanadamu kwamba hawezi kufanya mambo makuu,basi waache wanaoamini waendelee na imani yao.

Anonymous said...

Woiiiii!!! Da Chemi tumeshampoteza jamani. Siamini kama ni yeye ameandika hivi:

Lakini leo namzungumzia Askofu Kakobe ambaye nilimshuhudia mwenyewe akimponyesha baba MNigeria aliyekuwa ameumia mgongo mwaka 1999 alipokuja Boston. Yule baba ni mzima hadi leo, na kila akiniona lazima aniuliza habari za The Man of God Askofu Kakobe. Imani ni kitu kikubwa sana, kama huna basi waache wenzako wakae na imani zao. Kuhusu yule MNigeria nilikuwa namfahamu kabla hajapata ajali na nilimshauri aende kwa Kakobe atakapokuwa Boston. Alienda na kapona. Alitupa magongo yake hapo hapo. Mungu yu Mwema!

Anonymous said...

Anony wa June 30, 2013 1:17 AM,

Ni kweli hujakosea dada Chemi mmempoteza katika vijiwe vyenu vya majungu fitina na chuki dhidi ya jina kuu kuliko majina yote jina la YESU KRISTO linalohubiriwa na Mtumishi wa Mungu Askofu Kakobe, Ndio maana mashetani wote mnapiga makelele. mlitaka awe katika njia pana mliyopo nyinyi ya kwenda upotevuni, lakini Dada Chemi ameigundua siri ndio maana ametoka huko, Mungu akufungue na wewe macho pia ili ujue kwamba hakuna neno gumu la kumshinda Mungu ikiwa watu wataamini kazi iliyofanywa na YESU KRISTO msalabani.

Anonymous said...

Anony June 30, 2013 8:11 AM
BRAINWASHED

Anonymous said...

brainwashed for the name above all names and the only way to heaven JESUS CHRIST. while by your word it's obvious that you have been brainwashed by the father of lies, the devil.