Showing posts with label Divorce. Show all posts
Showing posts with label Divorce. Show all posts

Sunday, December 06, 2015

Kesi ya Rufaa ya Talaka ya Thadei Mtembei Imeahirishwa

wooden gavel and books on wooden table,on brown background

Na Mwandishi wetu

KESI ya rufaa ya madai ya talaka dhidi ya mfanyabiashara na Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya St Mathew, Thadei Mtembei imeahirishwa baada ya wakili wa Mtembei, Mussa Kyoboya kudai mrufaniwa yuko India kwa matibabu.

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Tarimo.

Katika kesi hiyo, mpeleka rufaa, Magreth Mwangu anawakilishwa na wakili Chacha Mrungu. Kesi hiyo ilikuja mahakamani juzi ambapo mrufaniwa alitakiwa kupeleka majibu ya rufaa.

Hata hivyo, wakili wake alisema majibu hayako tayari kwani kuna vipengele ambavyo alitakiwa kusaini, lakini ilishindikana kutokana na kuwa nchini India kwa matibabu. Kesi hiyo imepangwa kuendelea Desemba 16 mwaka huu.

Awali, kesi hiyo ilisikilizwa katika Mahakama ya Mwanzo Kizuiani mbele ya hakimu Rajab Tamaambele, ambapo Mwangu na watoto wake walionekana hawana haki, kwa madai sio mke halali na watoto hao ni wa zinaa kutokana na kuzaliwa nje ya ndoa.

Katika madai ya msingi, Mwangu anataka talaka, mgawanyo wa mali na matunzo ya watoto.

Katika sababu za rufaa, mrufani alieleza kusikitishwa na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Mwanzo Kizuiani Septemba Mosi mwaka huu, kwa hakimu kukosea kisheria kwa kutosaini nakala ya hukumu ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa saini za wazee wa baraza.

Sababu nyingine ni Mahakama kukosea kisheria kwa kunyang’anya haki ya watoto kwa kutotoa matunzo ya watoto kwa mama, ambaye anaishi na mrufaniwa kwa miaka 20 na kuvunja Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009. Maamuzi ya Mahakama ya Kizuiani yalishindwa kufuata sheria kwa wazee wa baraza kushindwa kutoa maoni yao.

Saturday, September 18, 2010

Morgan Freeman na Mke Wake Waachana Rasmi

Mcheza sinema maarufu Morgan Freeman na mke wake wameachana. Walikuwa wametengana tangu Mzee Morgan alivyopata ajali ya gari akiwa na mwanamke mwingine. Pia iligundulika kuwa alikuwa anatembea na mjukuu wake tangu ana miaka 16. E'dena Hines ana miaka 27 sasa na atategema kuwa Mrs.Morgan Freeman mtarajiwa. Nataka kutapika! Hata haya hawana.
Mnaweza kusoma habari zaidi kwa kubofya HAPA:

***********************************************************************

Morgan Freeman, Missus Finalize Divorce

Look out, ladies, Morgan Freeman is officially a free man.

A Mississippi judge has finalized the divorce of the Academy Award-winning actor from his second wife of 26 years, Myrna Colley-Lee.

Freeman's Jackson-based lawyer, William R. Wright, tells E! News that a divorce decree was issued on Wednesday, though terms were kept under seal.

"There's no waiting period, there was no trial and they reached an amicable settlement settlement," said the legal eagle. "He is just happy that they can both move on."

The Dark Knight star married Colley-Lee, a theater and film costume designer, on June 16, 1984, and the couple were together during Freeman's rise to the top of the film world as one of Hollywood's most durable and acclaimed actors.

In August 2008, however, the thesp's business manager announced the pair had filed for divorce after separating the previous December. No reason was given for the split, but the divorce petition came just days after Freeman was involved in a scary car crash with a female friend of the family's.

Freeman, 73, was previously hitched to Jeanette Adair Bradshaw from 1967 to 1979.

Read more: http://www.eonline.com/uberblog/b200951_morgan_freeman_missus_finalize_divorce.html?utm_source=eonline&utm_medium=rssfeeds&utm_campaign=imdb_tv-movies#ixzz0zssxgbaJ

Thursday, August 13, 2009

Divorce Cakes - Keki za Kuachana

Wadau, mapenzi ni matamu lakini wakati mwingine yanakwisha. Waliokuwa wanapendana wanajikuta wanachukiana. Kama walikuwa wamefunga ndoa basi wanaachana (divorce). Sasa imeanza biashara ya kufanya party za kusherekea kuachana. Hebu mcheki hizi dizaini za keki!

******************************************







Thursday, April 24, 2008

Ndoa ya Star Jones na Al Reynolds yavunjika!

Star Jones kabla hajapunguza uzito na baada ya kupunguza
Arusi ya Star Jones na Al Reynolds 2004


Star Jones na Al Reynolds wakiwa kwenye Honeymoon

Star Jones na Al Reynolds baada ya Star kupunguza uzito


BEFORE AND AFTER


Haya leo nimekuwa umbea. Nimesikia habari kuwa Star Jones na mume wake Al Reynolds wanaachana. Kwa kweli mambo ya kuachana ni mambo ya kawaida hapa Marekani, lakini hii imekuwa habari kubwa.

Kama mnakumbuka walivyofunga ndoa ilikuwa habari kubwa kweli. Yaani Star Jones wakati huo alikuwa ni moja wa wanawake wa ile show, THE VIEW. Alikuwa anapendwa kweli na watazamaji.. Watu walivyosikia anaolewa kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 42 walifurahi kweli ingawa walisema huyo mume wake anacheza upande mwingine (anapenda wanaume wenzake). Sasa baada ya kutangaza ndoa, alikuwa anatangaza details mpaka chupi atakayovaa mpaka watu wakaona kinyaa.

Mara baada ya kuolewa kwake alianza kupungua uzito, kawa mbaya wengine walisema kawa kama kinyago, halafu alitolewa kwenye THE VIEW. Alikataa kusema alipunguza uzito kwa njia gani. Kumbe alifanyiwa opresheni ya kupunguza tumbo. Watu walimchukia kwa vile alificha siri yake kwa miaka mitatu.

Sasa wanaachana. Nikitazama picha za Star kabla hajaolewa na sasa namwona mtu mwingine na alivyo sasa.
Hivi ni kwa nini mara nyingi watu wakifunga ndoa ya kifahari ndoa haidumu? Utakuwa watu walifunga ndoa simple lakini zinadumu miaka na miaka na wanapendana hasa.

Wadau mnasemaje?
Kwa habari zaidi someni: