Arusi ya Star Jones na Al Reynolds 2004
Star Jones na Al Reynolds wakiwa kwenye Honeymoon
Star Jones na Al Reynolds wakiwa kwenye Honeymoon
Star Jones na Al Reynolds baada ya Star kupunguza uzito
BEFORE AND AFTER
Haya leo nimekuwa umbea. Nimesikia habari kuwa Star Jones na mume wake Al Reynolds wanaachana. Kwa kweli mambo ya kuachana ni mambo ya kawaida hapa Marekani, lakini hii imekuwa habari kubwa.
Kama mnakumbuka walivyofunga ndoa ilikuwa habari kubwa kweli. Yaani Star Jones wakati huo alikuwa ni moja wa wanawake wa ile show, THE VIEW. Alikuwa anapendwa kweli na watazamaji.. Watu walivyosikia anaolewa kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 42 walifurahi kweli ingawa walisema huyo mume wake anacheza upande mwingine (anapenda wanaume wenzake). Sasa baada ya kutangaza ndoa, alikuwa anatangaza details mpaka chupi atakayovaa mpaka watu wakaona kinyaa.
Mara baada ya kuolewa kwake alianza kupungua uzito, kawa mbaya wengine walisema kawa kama kinyago, halafu alitolewa kwenye THE VIEW. Alikataa kusema alipunguza uzito kwa njia gani. Kumbe alifanyiwa opresheni ya kupunguza tumbo. Watu walimchukia kwa vile alificha siri yake kwa miaka mitatu.
Mara baada ya kuolewa kwake alianza kupungua uzito, kawa mbaya wengine walisema kawa kama kinyago, halafu alitolewa kwenye THE VIEW. Alikataa kusema alipunguza uzito kwa njia gani. Kumbe alifanyiwa opresheni ya kupunguza tumbo. Watu walimchukia kwa vile alificha siri yake kwa miaka mitatu.
Sasa wanaachana. Nikitazama picha za Star kabla hajaolewa na sasa namwona mtu mwingine na alivyo sasa.
Hivi ni kwa nini mara nyingi watu wakifunga ndoa ya kifahari ndoa haidumu? Utakuwa watu walifunga ndoa simple lakini zinadumu miaka na miaka na wanapendana hasa.
Wadau mnasemaje?
Kwa habari zaidi someni:
9 comments:
dada chemi hamna cha ndoa za kifahari au ndoa simple,matatizo ya kutoelewana na kuachana yapo haijalishi ilikuwa ndoa simple au ya kifahari.kwa upande fani naweza sema kwa upande waafrika tunaweza ona ndoa zina muda mrefu lkn watu wanaona moto kwenye hizo ndoa,na wanaamua kuvumilia hasa wanawake,ukizingatia akifikiria kuachika anaona kama anaiabisha familia yake etc,dada chemi wenzetu waliodunia ya kwanza huwa hawapendi kuona wananyanyasika kwenye mahusiano na kwenye ndoa zao.sisi huku tunaodumisha mila kwa kuona aibu hasa mwanamke kuachika.
mimi nadhani mila zetu na tamaduni zinatufanya hasa waafrika tuwe na uvumilivu na sio kwamba watu wanafurahia ndoa,ukilinganisha na wenzetu wa mataifa ya magharibi mtu akileta za kuleta anaomba divorce mfano kama hapa kwetu Tanzania mwanamke wa kikurya akipigwa na mumewe anaona ndo anapendwa na wala hashitaki hata kuomba talaka.
ndoa za kifahari na simple zote zina matatizo,hata hapa TZ ila tofauti kubwa ipo kwa mataifa ya wenzetu,mwanandoa akifanya ndivyo sivyo mwenzake anaomba talaka fasta.dada chemi mfano hapa bongo tatizo la wanaume wanandoa kuwa na nyumba ndogo a.k.a vimada ni kama fashion siku hizi,yani mfano msichana anaolewa utasikia watu wanasema asubiri kuibiwa na mume wake yani mumewe kuwa na mwanamke wa pembeni.hii imekuwa common sana hapa bongo,utakuta hata kama mke wa jamaa akishtukia lijamaa linafanya kuomba msamaha kwa kusema shetani alimpitia,na anaweza rudia hivyo hata mara 5basi mwanamke anasamehe tu story imekwisha na hamna mambo ya talaka hapo.
by mkereketwa
WOOW MI NIMEPENDA SHELA LAKE LIPO BOMBA SANA,NDO FASHION YA MASHELA YA SIKU HIZI BONGO DARESALAMA.
kwa kweli shela nyeupe huwa inapendeza haswa kwenye harusi,walipendeza kweli ingawa ndo hivyo tena.
kwahiyo nawewe hutaki kukonda ehhh
SASA NA WEWE PUNGUZA UZITO SIO UNASEMA ANATISHA KWASABABU YA KUCOVER UZITO WAKO FANYA HIMA UTAPENDAZA SANA
Dada Chemi you are beautiful! Achana na hao wapuuzi.
Kuhusu Star Jones alivyokonda kawa mbayaaa!
Now Al Reynolds married a beautiful heavyset sista. Then she turned into a skinny and ugly hag. No wonder he lost interest.
Post a Comment