Showing posts with label Jamaica. Show all posts
Showing posts with label Jamaica. Show all posts

Wednesday, December 23, 2009

Ajali ya American Airlines Jamaica



Wadau, ndege ya American Airlines imepata ajali mara baada ya kutua huko Norman Manley International airport, Kingston, Jamaica. Kwa waliowahi kufika huko wanaelewa kuwa huo uwanja uko mwambao mwa bahari ya Caribbean. Habari zinasema kuwa ndege hiyo iliyokuwa na abiria 154 karibu iingie kwenye bahari! Ilisimama futi 10 (mita 3) kabla ya ufukwe! Ni miujiza hakuna aliyekufa ingawa watu 90 waliumia. Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia leo.
Habari zinasema kuwa ndege ilielekea kutua salama, abiria walikuwa wanapiga makofi, lakini wakati wa 'taxi' ndege haikusimama na badala yake ikaanza kuteleza, na kugonga vitu na zile oxygen masks zilishuka na zile overhead compartment za carryon baggage zilifunguka. Watu walikuwa wanapiga mayowe na kumwomba Mungu! Walisikia ndege inakatika vipande vipande.
Ndege hiyo aina ya 737, ilikuwa imetoka Washington, D.C.

Sunday, September 13, 2009

Caribbean Festival Kwetu Cambridge Leo!

Wadau, leo hapa Cambridge, Massachusetts, tulivamiwa na watu wa Boston. Walikuwa hapa kwa ajili ya Caribbean Carnival ambayo infanyika kila mwaka. Mwaka huu walichelewa kuifanya, kawaida wanafanya August na ndo tunaaga summer (kipindi cha joto). Nimepiga picha kadhaa kwa ajili yenu.














Sunday, August 17, 2008

Bendera yetu Iraq - Part II

Mwanajeshi wa Tanzania (?) aliyeumia huko kwenye Vita vya Iraq
Jamaica Flag

Tanzania Flag
********************************************
Wadau, kuna watu ambao wanadai kuwa huyo mwanajeshi kavaa bendera ya Jamaica begani. Wala haifanani na bendera ya Jamaica. Ila inaonekana kabisa kama ya Tanzania, au ni macho yangu?