Kutoka kwa Taji Liundi
TAHADHARI:
Inanisikitisha sana kuandika tahadhari hii kwenu rafiki
zangu. Haistahili kuwa tahadhari. Lakini SASA HIVI katika mitaa
mbalimbali jamaa zetu wa TANROADS wanapita kukamata na kupiga FINE
magari yaliyoegeshwa "vibaya". Fine ni Tsh 220.000.
Hili ni
tatizo kubwa sana na RUSHWA inafukuta kwenye zoezi hili. Mtanzania wa
kawaida HAWEZI kulipa kiasi hicho kama ameegesha KANDO YA BARABARA zetu
za kawaida, mfano pale Sinza Palestina.
Hao jamaa wanadai inabidi uwe umewasha TAA ZA TAHADHARI NA UWEKE TRIANGLE.
Sawa. Lakini si kawaida kabisa na zoazoa yao leo ni hatari. Wanatembea na Noah kubeba madereva/abiria waliokamatwa.
MAONI YANGU: Tusinyanyasane! Sio uungwana. Wananchi tunasota ile mbaya. Huko mitaani tunahangaika kujikwamua kiuchumi.
TANROADS kama Wakala wa Serikali inatakiwa ITOE MATANGAZO YA ELIMU KWA
UMMA KABLA YA KUCHUKUA HATUA ZA KISUMBUFU NA KIHALIFU KWA KUCHOCHEA
RUSHWA(wanakubali hadi Tsh 60/70elfu ukiongea nao).
Kwa kawaida,
wangetakiwa wapite hata na PA watangaze: "Ndg wananchi katika eneo hili,
mnaombwa kuegesha magari yenu kwa utaratibu huu kandokando ya barabara
kuu. Hakikisha umewasha taa za dharura na weka Triangle mita...nyuma ya
gari".
Hii ingeondoa usumbufu wa KUMWELEKEZA kila mkosaji.
Tumieni TBC!! RADIO Uhuru nk. Ombeni Matangazo ya kijamii kwenye Radio binafsi.
Kinachotokea ni shambulio la kihalifu kwa WaTanzania wasio na hatia.
Kwa mara nyingine tena naandika kuhusu uendeshaji mambo KIHOLELA.
Uholela huu unanyanyasa waTanzania.
Marafiki zangu humu mlio na wadhifa na uwezo wa kufwatilia hili..fanyeni hivyo. Mtagundua nazungumza UKWELI!!
Sijapendezwa!
Eneza TAHADHARI hii.
Showing posts with label TANROADS. Show all posts
Showing posts with label TANROADS. Show all posts
Saturday, June 28, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)

