Saturday, June 28, 2014

Tahadhari kwa Waegeshao Magari Jijini Dar

Kutoka kwa Taji Liundi

TAHADHARI:

Inanisikitisha sana kuandika tahadhari hii kwenu rafiki zangu. Haistahili kuwa tahadhari. Lakini SASA HIVI katika mitaa mbalimbali jamaa zetu wa TANROADS wanapita kukamata na kupiga FINE magari yaliyoegeshwa "vibaya". Fine ni Tsh 220.000.

Hili ni tatizo kubwa sana na RUSHWA inafukuta kwenye zoezi hili. Mtanzania wa kawaida HAWEZI kulipa kiasi hicho kama ameegesha KANDO YA BARABARA zetu za kawaida, mfano pale Sinza Palestina.

Hao jamaa wanadai inabidi uwe umewasha TAA ZA TAHADHARI NA UWEKE TRIANGLE.
Sawa. Lakini si kawaida kabisa na zoazoa yao leo ni hatari. Wanatembea na Noah kubeba madereva/abiria waliokamatwa.

MAONI YANGU: Tusinyanyasane! Sio uungwana. Wananchi tunasota ile mbaya. Huko mitaani tunahangaika kujikwamua kiuchumi.

TANROADS kama Wakala wa Serikali inatakiwa ITOE MATANGAZO YA ELIMU KWA UMMA KABLA YA KUCHUKUA HATUA ZA KISUMBUFU NA KIHALIFU KWA KUCHOCHEA RUSHWA(wanakubali hadi Tsh 60/70elfu ukiongea nao).

Kwa kawaida, wangetakiwa wapite hata na PA watangaze: "Ndg wananchi katika eneo hili, mnaombwa kuegesha magari yenu kwa utaratibu huu kandokando ya barabara kuu. Hakikisha umewasha taa za dharura na weka Triangle mita...nyuma ya gari".

Hii ingeondoa usumbufu wa KUMWELEKEZA kila mkosaji.

Tumieni TBC!! RADIO Uhuru nk. Ombeni Matangazo ya kijamii kwenye Radio binafsi.
Kinachotokea ni shambulio la kihalifu kwa WaTanzania wasio na hatia. Kwa mara nyingine tena naandika kuhusu uendeshaji mambo KIHOLELA. Uholela huu unanyanyasa waTanzania.
Marafiki zangu humu mlio na wadhifa na uwezo wa kufwatilia hili..fanyeni hivyo. Mtagundua nazungumza UKWELI!!

Sijapendezwa!

Eneza TAHADHARI hii.

6 comments:

Anonymous said...

Ninasikitika sana kwa vitendo hivyo. Siyo watoe taarifa, bali wabandike mandiko ya NO Parking sehemu wanazoona hazistahili kuegesha magari. Ni kwa vile watanzania pia hatujui sheria. Akishika gari ambapo hapajawekwa hiyo alama wanatakiwa kushtakiwa. Amkeni Watanzania. Pili,wanapokataza kupaki gari, waonyeshe ni wapi wametenga parking ya magari yaliyoongezeka. Hii ndiyo adha iliyo katika jiji hili. Mfano, makusanyo ya Parking ambayo yamekuwa yakikusanywa kila siku, yamefanya kazi gani, yameboresha nini, yameongeza vipi sehemu za kupaki magari. Watanzania tuko kimya.Tunashindana na wale wanaokusanya, lakini halifiki panapohusika.Lakini panapohusika ni wapi!!! Tanzania inayokwenda bila sheria. Leo utampeleka wapi mtu. Kila mtu akiamua anaanzisha mradi na kuwachomoa watanzania. Watanzania tudai sehemu za kupaki, watuonyeshe. Mbona gari za serikali hazitiliwi kashkash!! Je! Ni sheria gani inayosema wasifuate sheria. Hii inanikumbusha tukio la askari aliyeiweka gari pembeni kule karibu na makumbusho kwa kutanua. Akaingia matatani.Jamani!! Vyombo vya utekelezaji wa majukumu kuweni na roho za kibinadamu!!!!

Anonymous said...

Naomba wanajamii tushirikishane uzoefu wa kuchachamaa na uelewa wa sheria. Tukifanya hivyo tutarekebisha uonevu unaotokea kila siku, asilimia kubwa ikiwa ni woga tu, au eti siwezi kupoteza muda. Hili ndilo linalotuponza. kumbuka, muda utakaopeteza kupigania haki, ni Muda unaowakoa watanzania wengi, wanyonge, ambao sauti zao zimedidimizwa. Ni sisi ndio tutakobadilisha au kukomesha uovu tunaofanyiwa kwa kinga ya pesa. Pesa uliyovuna kwa jadsho ni tamu, ni kwa ajili ya familia. kwa nini tuendelee kuwajazia vibaba visivyojaa hata ukiwahamishia utajiri wote wa Tanzania. Asante!! Naomba Tupambane, ila tufuate sheria!

Anonymous said...

Sijawahi kusikia duniani kwamba mtu anayeegesha gari kandokando ya barabara mahali ambapo haijakatazwa rasmi anatakiwa kuwasha taa za tahadhari na kuweka pembetatu. Naamini hii ni kinyume cha sheria. Naomba wanasheria watoe ufafanuzi.

Anonymous said...

Hii ya kuwasha taa na triangle ni kali kuliko zote mwaka. Sasa kama watoza ushuru wamegeuka walimu wa alama za barabarani walimu watafanya kazi gani?

Anonymous said...


Sisi si watoto yatima bali tulisha kata tamaa na mfumo wetu wa sheria na mahakama na ndio maana tunaona bora kutoa rushwa yaishe.

Hivi iweje nikamatwe kwa kosa la kupark mahali ambapo hakuna alama ya kunizuia kupark pale halafu nikubali kulipa faini?

Maana ukiamua mpelekane mahakamani sidhani kama mshitaki wako watapata ushahidi wa kukutia hatiani.

Hili ni taifa la waoga, wanaojua kuongea sana, na wasio tayari kutoa jasho kuleta mabadiliko - HAPO TU!

Anonymous said...

jana nilinusuruka mitaa ya mori...ni hatari sana na sijui kwanini operation kama hizi zinakuja hadi mtaani Wamekosa za mjini au hazijawatosha.