Showing posts with label Tiger. Show all posts
Showing posts with label Tiger. Show all posts

Saturday, November 28, 2009

Tiger Woods Apigwa na Mke Wake na Kupata Ajali ya Gari!



Duh! Tiger Woods ana mke mzuri, lakini inasemekana ameanza kutembea na mama fulani (bimbo) huko New York. Na ndo chanzo cha mke wake kumpiga na yeye kukimbia saa 8 za usiku na kupata ajali ya gari jana! Kwanza kama hii habari ni kweli namsifu mke wake kwa kumtwanga! Wanaume hawana dogo! Na si ajabu huyo mwanamke ni mbaya kuliko mke wake! Tiger na mke wake wana watoto wawili wadogo.





**************************************************************************


Police in Florida hope to talk to golfing great Tiger Woods today about the circumstances surrounding his SUV accident early Friday.

The 33-year-old was treated and released from a hospital after his vehicle struck a fire hydrant at his estate near Orlando and then and hit a tree on a neighbor's property in the early morning hours.

Police say they attempted to talk to Woods yesterday, but his wife said he was sleeping. One key question is where he was headed at that hour.

The accident came two days after the National Enquirer published a story alleging that Woods had been seeing a New York night club hostess, and that they recently were together in Melbourne, where Woods competed in the Australian Masters.

Kwa habari zaidi someni:

http://abcnews.go.com/Entertainment/cops-questions-tiger-woods-car-accident/story?id=9195444

http://www.orlandosentinel.com/news/local/breakingnews/os-bk-tiger-woods-accident,0,1369881.story

Thursday, December 27, 2007

Tiger Tatiana aua!

Bad Tatiana, Dead Tatiana!


Wazungu wanapenda sana kufuga wanyama pori kwenye maeneo wanayoita 'Zoo' hapa Marekani. Huko San Francisco, California wametengeneza zoo inayofanana na pori ambao wanakaa hao wanyama huko kwao mfano Afrika, India.

Afrika hatuna huyo mnyama, Tiger. Ni aina ya paka mkubwa kama simba. Ana rangi ya orange na mistari meusi.

Sasa juzi siku ya Krismamisi vijana fulani watatu walienda kutembea kwenye Zoo huko San Franciso. Saa ya kufunga hiyo zoo walikuwa bado wanazura huko. Kwa bahati mbaya kijana moja aliuliwa na huyo tiger, Tatiana (pichani), na aliwajeruhu wengine wawili.

Polisi walimwua Tatiana aliyekutwa ameketi karibu na mtu aliyemjurehi. Ajabu kuna wazungu wanalalamika kwa nini polisi walimwua. Wanamlilia huyo Tiger kama vile binadamu kafa.

Watu wanauliza huyo Tiger alitorokaje, maana alivuko 'moat' (maji yanayozunguka eneo) na kuruka ukuta mrefu ambayo wanasema haiwezekani. Hawajui kama mtu alimwachia huru au vipi. Tutajua ilikuaje siku zijazo. Msicheze na mnyama pori mwenye hasira!

Familia ya marehemu Carlos Souza Jr. (17) wanapanga mazishi yake. Bila shaka hiyo Zoo watalipa gharama zote za mazishi na kulipa fidia ya mamilioni ya dola kwa familia yake!

Ajabu mwaka jana huyo huyo Tatiana alikula mkono wa mama moja (Ndiyo, aliula) aliyekuwa anamlisha chakula. Huyo mama alikuwa ni mfanyakazi na alitenda maovu yake mbele ya umati wa watu waliolipa hela kushushudia tiger analishwa chakula.

Mwaka 2003 hapa Boston kuna Sokwe 'Little Joe' aliwahi kutoroka Zoo. Baada ya kupiga watu watatu akiwemo mtoto mdogo mwenye miaka mitatu, alikutwa ameketi kwenye kituo cha basi cha kwenda mjini Boston. (Ni kweli kabisa) Kuna watangazaji wa redio walifukuzwa kazi kwa kumfananisha na mtu mweusi wa ghetto.

Kwa habari zaidi za muaji Tatiana soma:

http://www.sfgate.com/cgi-bin/article.cgi?f=/c/a/2007/12/27/MN39U4TQ5.DTL

http://www.timesonline.co.uk/tol/news/world/us_and_americas/article3098742.ece

http://edition.cnn.com/2007/US/12/27/tiger.attack/?imw=Y&iref=mpstoryemail