Thursday, December 27, 2007

Tiger Tatiana aua!

Bad Tatiana, Dead Tatiana!


Wazungu wanapenda sana kufuga wanyama pori kwenye maeneo wanayoita 'Zoo' hapa Marekani. Huko San Francisco, California wametengeneza zoo inayofanana na pori ambao wanakaa hao wanyama huko kwao mfano Afrika, India.

Afrika hatuna huyo mnyama, Tiger. Ni aina ya paka mkubwa kama simba. Ana rangi ya orange na mistari meusi.

Sasa juzi siku ya Krismamisi vijana fulani watatu walienda kutembea kwenye Zoo huko San Franciso. Saa ya kufunga hiyo zoo walikuwa bado wanazura huko. Kwa bahati mbaya kijana moja aliuliwa na huyo tiger, Tatiana (pichani), na aliwajeruhu wengine wawili.

Polisi walimwua Tatiana aliyekutwa ameketi karibu na mtu aliyemjurehi. Ajabu kuna wazungu wanalalamika kwa nini polisi walimwua. Wanamlilia huyo Tiger kama vile binadamu kafa.

Watu wanauliza huyo Tiger alitorokaje, maana alivuko 'moat' (maji yanayozunguka eneo) na kuruka ukuta mrefu ambayo wanasema haiwezekani. Hawajui kama mtu alimwachia huru au vipi. Tutajua ilikuaje siku zijazo. Msicheze na mnyama pori mwenye hasira!

Familia ya marehemu Carlos Souza Jr. (17) wanapanga mazishi yake. Bila shaka hiyo Zoo watalipa gharama zote za mazishi na kulipa fidia ya mamilioni ya dola kwa familia yake!

Ajabu mwaka jana huyo huyo Tatiana alikula mkono wa mama moja (Ndiyo, aliula) aliyekuwa anamlisha chakula. Huyo mama alikuwa ni mfanyakazi na alitenda maovu yake mbele ya umati wa watu waliolipa hela kushushudia tiger analishwa chakula.

Mwaka 2003 hapa Boston kuna Sokwe 'Little Joe' aliwahi kutoroka Zoo. Baada ya kupiga watu watatu akiwemo mtoto mdogo mwenye miaka mitatu, alikutwa ameketi kwenye kituo cha basi cha kwenda mjini Boston. (Ni kweli kabisa) Kuna watangazaji wa redio walifukuzwa kazi kwa kumfananisha na mtu mweusi wa ghetto.

Kwa habari zaidi za muaji Tatiana soma:

http://www.sfgate.com/cgi-bin/article.cgi?f=/c/a/2007/12/27/MN39U4TQ5.DTL

http://www.timesonline.co.uk/tol/news/world/us_and_americas/article3098742.ece

http://edition.cnn.com/2007/US/12/27/tiger.attack/?imw=Y&iref=mpstoryemail

1 comment:

Anonymous said...

Warudishe hao wanyama waliotoka! Kuwafuga katika zoo ni mateso kwao.