Monday, September 04, 2006

Crocodile Hunter Steve Irwin Kafa


Loh! Leo asubuhi nimeamka nakufungua TV na kuona habari kuwa Steve Irwin au kwa jina lingine Crocodile Hunter (mlinda mamba) kafa. Wanasema kauliwa na samaki aina ya Sting Ray. Hicho kichomi chake chenye sumu kilimchoma kwenye moyo.

Nilisikitika sana kuwa kafa lakini huko najiuliza je ansingekuwa anacheza na wanyama hatari si angekuwa bado yu hai? Siku zote nilisema ngoja tutasikia kuwa kaumwa na nyoka na kafa. Hata siku moja sikudhania kuwa hatima yake ingekuwa samaki Sting Ray.

Nilipokuwa nakaa Chuo Kikuu cha Dar es Salaaam, jirani yetu mzungu akawa anatulaumu kwa kuua majoka. Na kama kulikuwa na nyoka nyumbani kwake, analazimisha houseboy wake amkamate na kumpelea idara ya Zoology pale UDSM. Mzungu mwenyewe alikuwa mshenzi, anamfuata na gari yake kuhakikisha kuwa anampeleka kweli!

Ilikuwa sisi wengine tukiona nyoka, tunatafuta fimbo, mawe na kuua! Kwanza ukiumwa na huyo nyoka, kutakuwa na dawa kweli dispensary ya kukukutibu. Au unaweza kuchelewa kupata usafiri wa kwenda hospitalini na kufa. Na mara nyingi tulisikia mtu kafa kwa kuumwa na nyoka, hivyo kwa nini tusiwaue! Ua au uliwe!

Lakini wazungu sijui wakoje, wakiona mnyama hatari wanataka awe pet. Lakini mnyama pori ni mnyama pori tu! Mnakumbuka yule tiger alivyomtafuna Roy, huko Las Vegas kwenye Seigfried & Roy Show. Yule tiger alifugwa nao taokea azaliwe. Je, mnakumbuka yule kijana wa kizungu mwenye miaka 17 aliyekufa baada ya kuumwa na pet kifutu (viper) wake huko Kenya? Alikuwa anafuga majoka wa kila aina nyumbani kwake, macobra, chatu, nk. na alishumwa nao, lakini huyo kifutu ndo kamwuma na kumwua.

Haya nirudi kwa marehemu Steve Irwin. Ilikuwa wakati mwingine nikitazama show zake nasema anajiona mungu wa wanyama na hawatadhuru. Utamwona yuko Afrika anakamata black mamba na cobra mwenye hasira. Mara anacheza ma mamba mkubwa kweli kweli huko kashika mtoto wake, tena mdogo mwenye umri miezi michache tu. Tena anamtembeza mbele ya mamba kama kitoweo vile. Halafu alidiriki kusema, alijua kuwa mamba hawezi kumdhuru mwanae. Bora angesema ilikuwa bahati mamba hakumdhuru.

Na leo tunasikia alikuwa anaogelea na sting rays huko Australia kwa ajili ya show yake, ndo alikuwa anaogelea juu ya sting ray na stingray kanyanyua kichomi chake na kumchoma kifuani kwenye moyo! Naona huyo sting ray alikuwa si rafiki yake, au alichoka naye.

Mungu amlaze kaka Steve Irwin mahali pema mbinguni. Amen. Na kifo chake iwe fundisho kwa wengine, mnayama pori ni mnyama pori.

2 comments:

AfroFeminista said...

Umenichekesha sana! Kweli mtu anapozoea kucheza na wanyama wa pori au majoka (siku yangu ya kwanza kulisikia hilo neno!!!), ni muda tu, kabla hajakufa kutokana na hayo majoka na wanyama!!!

Na huyo muzungu jirani wako, ni mwenda azimu kweli kweli!

Naomba radhi, Kiswahili changu ni kibaya sana!

Anonymous said...

Chemi,
unajua hawa wazungu hawajozea kuona hawa wananyama katika mazingira yao halisi (natural), kwa hiyo wanaona kama ni big deal mtu kuchezea hawa wanyama.

sisi kule nyumbani tuna matatizo mengi sana, hatujafikia muda wa kuaanza kujali mambo ya wanyama (wawe pet au wa polini), labda tunajali mbwa (guard dog) kwa sababu anaweza kuwa mlinzi na kufukuza wezi, au paka kwa sabau anaweza kusaidia kuua panya. Swala la urafiki na wanyama bado halipo nasi. au nyie wengine mnasemaje???