Friday, September 22, 2006

Tanzanian Model Tausi Likokola - International Star



Huenda mmesikia jina la Tausi Likokola. Tausi ni model wakiTanzania anayejulikana kimataifa. Amekuwa kwenye maonyesho ya Urembo ya Gucci, Christian Dior, Tommy Hilfinger, Issey Miyake, na Escada. Mambo yake si mchezo. Huenda amepishana na Naomi Campbell na Tyra Banks kwenye Catwalk (jukwaa inayotumika kwenye maonyesho ya urembo).

Zaidi ya kazi za urembo Tausi amekuwa akifanya kazi ya kusaidia wagonjwa wa UKIMWI kupitia NGO yake iitwayo Tausi AIDS FUND . Aliaanzisha baada ya ndugu na marafiki wengi kuaathirika na huo ugonjwa hatari.

Akina Dada watapenda site yake. Anatoa tips za urembo kama kutunza ngozi, nywele, vyakula bora na mengine. Pia ametunga vitabu na kuna muhtasari za vitabu vyake.

Website ya Dada Tausi Likokola:

http://www.tausidreams.com

Ama kweli WaTanzania tunaweza kujivunia kuwa nasi tuko kwenye jukwaa la fesheni ya kimataifa. Hongera Tausi, mfano wako ni wa kuigwa.

6 comments:

Anonymous said...

Chemi asante kwa kuposti hii article ya Tausi. Mafanikio ya ma Models wengi ni kuwa marketable kuitwa mara kwa mara na kuweza kuadvertise Products mostly wanakwendaga kwenya mavazi na mengineyo.
Kuna a lot of frustrated souls ambao wanataka kujiendeleza na wanatafuta "a leaning shoulder to tell them you can do it go for it" aidha kwa Big Brother au Big Sister ambaye ana upeo mkubwa na positive attitude.
Chemi you are a good example you are there now.labda kwenye Blogu yako ungeongeza Kipengele cha HINTS jinsi ya kubreak through, mikataba ambayo itakuletea matatizo mbeleni, web sites zipi za kutembelea. Nini cha Kufanya kama vitu haviendi.Na kadhalika
Hustahili kubeba huu mzigo, Najua una shughuli, lakini kuna matatizo ya watu wengi hawajui waanzie wapi kuendeleza vipaji vyao.
Haya ni maoni yangu tuu

Chemi Che-Mponda said...

Hi Kaka Peter,

Ku-breakthrough unahitaji moyo na uvumilivu na bahati.

Kuna watu wamechukua njia ya mkato wakidhania wameukata, kumbe huko baadaye nafasi nzuri ilipotokea mambo waliofanya nyuma uliwazuia kwenda mbele. Pia kuna watu ambao wanajua kuwa kuna akina dada na akina kaka wanaotaka kuwa models na kuwaonea. Mtindo moja ni 'Casting Couch' yaani kutembea na huyo anayekuahidi kitu. Kumbe hakuna lolote.

Naona nitakusanya tips na kuandika kwenye blogu. Wazo zuri.

Tip Moja - Cheki Craigslist kwa eneo unapokaa. Na ukienda kwenye audition au booking usiende peke yako.

Na halahala matangazo mengine yanadanganya, wanasema wanataka model kumbe wanataka mpige picha uchi. Nitatafuta mifano na kuweka kwenye blog.

Anonymous said...

Chemi,
kwa kweli tunashukuru kuendelea kutujulisha juu ya wabongo wenzetu ambao ni maarufu "celebrity", huyu modo sijawahi kumsikia-lakini sasa najua kuwa wabongo nao hawapo nyuma sana katika ukumbi wa kimataifa. Naona anatumia urembo wake kufanya vitu vingi tu vya maana. Kama mtu anataka habari zaidi anaweza kutembelea tovuti za hao watu maarufu na anaweza kuwatumia barua pepe moja kwa moja.
Ahsante sana.

Jaduong Metty said...

Chemi,

Asante kwa hii post. Najua vile vile umempigia debe Cynthia, lakini mh.."video girls" bado kwangu ni no. Kwa upande mwingine, dada Tausi amedhihirisha kwamba unaweza kufanikiwa kwa kuwa "classy" badala ya kujishushia hadhi. Kama unaongelea, kupiga kona nyuzi 180, basi dada Tausi ameweka kiwango ambacho nadhani hata Cynthia angekitafuta.

Shida kama alivyoelezea Peter Kapanga ni kwamba waTanzania wengi hawajajua namna ya kutafuta ushauri (mentoring), kwa hiyo watu wengi wanaishia kwenye njia potofu.

Jaduong Metty said...

Trio Kaka,

Naomba unitafute ukibahatika kupitia humu. mettyn@hotmail.com.

Anonymous said...

Aisee ni vizuri kusikia tausi is still doing googd.Juzi nilisikia spain au sijui italy wanataka kupiga marafuku sick looking girls on the catwalks, kwavile there are a bad example to other young girls. Sijui kama gazellle looking models like tausi will be affected, but i hope she has a healthy looking figure. Mi nafikiri cynthia is head for the same sature that tausi has---being an international model, alhtough what she is doing aint bad either. What there are both doing tausi and cynthia is very encoraging, showing that anyone can achieve their dreams if they really want to and they can actually benefit from them. Hongera sana tausi and cynthia for doing what your hearts desire and profiting from it, you both are an ecouragement for those of us who are too scared to pursue ours.