Saturday, September 30, 2006

TUUNGEJUA!!!!

Mwaka juzi mimi na rafiki yangu Alina tulikuwa tunaongea habari za kuweka pesa za kuishi na za kutosha tukiwa tumestaafu kazi. Miezi mitatu baada ya hayo maongezi Alina alifariki kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu. Siku hiyo tuyliyovyo kuwa tunaongea hakujua kuwa anaumwa. Kazini kwangu kuna mama fulani alienda lunch, hakurudi maana alipata massive heart attack na kufa barabarani kwenye sidewalk. Kijana mwingine aliaga kuwa tutaona wiki ijayo lakini alipata ajali ya gari na kufa kesho yake.

Mnafahamu wimbo wa maiti? “Nimekufa leo, kesho ni zamu yako!” Ukweli, watu wanakufa kila siku. Wengine wanakufa shauri ya uzee, wengine kwa ajali, wengine kwa kuuliwa na binadamu wenzao au wanyama wa porini, wengine kwa ugonjwa. Hakuna mtu anayajua atakufaje. Nadhani watu wangejua wangekaa kwa woga, wangeshinda wanalia na kutetemeka ovyo.

Nadhani ni vizuri kuwa sisi bindamu hatujui siku ambayo tumepangiwa kifo. Fikiria kama tungejua. Dunia ingekuaje?

Tuseme fulani anajua kuwa atakufa leo jioni saa mbili usiku. Basi ingekuwa hekaheka kuomba kupiga simu kwa watu na kuomba msamaha kwa watu aliyowakosea. Au angesema mi nakufa kleo ngoja nilipize kisasi kwa kumwua fulani na fulani. Mtu angeenda kuichoma moto nyumba ya mtu akijua kuwa hata akifungwa jela siku yake ya kufa ni karibu. Mtu asingehangaika na shule akisema haina faida maana atakufa siku fulani hivyo hiyo shule haitamsaidia na anapoteza muda. Asingeenda kazini, maana angesema nakufa siku fulani ngoja nifanye shughuli zangu binafsi.

Haya tuseme fulani anajua kuwa atakufa wiki ijayo Ijumaa saa tatu asubuhi. Basi anamaliza pesa kwenye credit card kwa kula laifu, na kuachia familia yake madeni tele. Huko anafanya ngono ovyo bila kujali magonjwa wala nini. Huenda angekunywa pombe kupita kiasi na kumaliza siku zake akiwa kwenye coma hospitalini! Wengine wangeenda kutapeli watu wakijua kuwa kifo kiko karibu hivyo hawana shida.

Wengine wangejua siku yao, basi ndo wangemaliza vitu walivyoanza halafu hawakumaliza kama vile kuandika vitabu, kushona gauni, wangemaliza kujenga nyumba zao, wangekazania kumpachika mtu mimba, wangeenda kwao kuona wazee na ndugu zao ambao hawajaona miaka mingi. Mtu angekaa na watoto wakae anawaambia kuwa anawapenda badala ya kushinda baa anakunywa pombe. Wangekuwa kanisani, miskitini, temple na sehemu zingine za dini wakitubu madhambi zao. Mtu kwenye foleni angeomba apishwe maana ni karibu saa yake ya kufa. Kwa kweli kama watu wangejua siku yao ya kufa ingekuwa pilika pilika.

Mungu aliumba kila kitu na sababu. Kwa kweli tunapita tu katika hii dunia. Mabibi na mababu zetu walitangulia na vizazi vijavyo vinafuata. Na ni maksudi alituumba kusudi tusijue siku ya kuondoka duniani. Hivyo kaeni mfikirie je, ningejua nitakufa lini ningefanya nini.

4 comments:

Anonymous said...

Hi Chemi,
umeongea point-lakini kwa kuzunguka sana. ushauri kwa wanandugu ni kuwa kwa sababu hujui utakufa lini-hakikisha kila kitu kipo sawa ili ukifa usiwaache ndugu zako wakitapa tapa. Mfano ni watu wangapi (wale waishio ughaibuni) ambao wana bima ya maisha (life insurance??). Je mnajua kuwa ukifa hii inaweza kukusafirisha kukupeleka nyumbani kwenu, na pia kulipa madeni yako yote (mfano mortgage)??
Ahsante sana kwa kuanzisha hii topic, labda watu wengi wataisoma na kuchangia maoni yao.

luihamu said...

The issue is not the day you or i die,but what good have you and i do to others?death is naturally and has to happen one day.It is very sad that we wait until so and so is dead that is the time we talk of his/her good things.Life is just a trip even death as a reason.who knows it feels it who jah bless no man curse.one one love.check for my blong and you will find topic to discuss.
www.luihamu-rastafarian.blogspot.com

Anonymous said...

Dada Chemi,
Asante sana kwa kutufanya tufikirie. Leo hii nimekata Globe Life Insurance na kuandika will. Nilikuwa naogopa lakini ni kweli kila mtu tumeandikiwa siku ya kufa.

Anonymous said...

ningejua ntakufa lini, ningejiua wiki moja kabla!