Thursday, October 26, 2006

David Banda Madonna



Huyo mtoto mweusi ni mtoto wa miezi kumi na tatu, David Banda ambaye baada ya miezi kumi na nane atakuwa mtoto wa mwimbaji maarufu Madonna na mume wake, Guy Ritchie. David yuko Uingereza sasa na familia yake mpya.

Juu, ni picha ya Madonna na watoto wake wote, chini ni picha ya David na baba yake mpya Guy Ritchie. Yaani wiki mbili tu, mtoto kanawiri na kuonekana mwenye furaha!

Madonna alimpata David kutoka kwenye nyumba ya watoto yatima huko Malawi. Mama yake alikufa katika uzazi na pia wakubwa zake walifariki shauri ya malaria. Baba yake mzazi Yohane Banda, alishindwa kumtunza mwanae na kumpeleka huko kwa watoto yatima. Baba yake anasema ni bora amchukuea maana angebakia Malawi angekufa.

Huyo mtoto atalelewa katika nyumba ya fahari na atakuwa na mahitaji yake yote na atasoma digrii zote anazotaka kusoma. Pia mama yake Madonna lazima atamwachia mamilioni ya dola za kurithi. Si uwongo kulelewa katika familia ni tofauti na kulelewa kwenye nyumba ya yatima.

David Banda kazaliwa katika umaskini, lakini leo anaishi katika utajiri. Na lazima kuna watu wanamwonea wivu!

2 comments:

Anonymous said...

me nafikiri hawa wanasheria/watetezi wa haki za binadamu wanatafuta ulaji tu. Kama baba ya mtoto ametoa ruksa, wao ni nani kuanza kuzuia zuia??

Anonymous said...

natumaini madona anajua analofanya na kwa faida ya david kwa kuwa kuna watu wengi siku hizi wamegeuza matatizo ya watu kuwa maarufu wanapowasaidia,kujenga majina yao
siku hizi mtu anakusaidia kwa kuwa anataka kuwa maarufu ,kujenga jina lake....