Wednesday, October 04, 2006

Ngoma ya 'Tap'



Najifunza kucheza ngoma ya Tap Dance. Hii picha nilipiga baada ya Show niliyofanya na Studio yetu hivi karibuni.

Tap Dance ni ngoma inayochezwa ukiwa umevaa viatu maalum vyenye vyuma chini. Kuna kuwa na chuma mbele na nyingine nyuma kwenye kisigino. Unacheza heel-toe, heel-toe na kila kikigonga chini kinaitwa tap. Na hivyo viatu vinatoa sauti kama muziki ukiweza kuvimudu.

Tap Dance ulianzishwa na waMarekani weusi na baadaye kudakwa na wazungu. Miaka ya nyuma watu wengi sana Marekani walijua kucheza lakini siku hizi 'interest' nayo inafifia. Watoto walikuwa wanacheza tangia wadogo. Marehemu Gregory Hines alijitahidi sana kufufua. Bila shaka mmeona watu wanacheza kwenye sinema kadhaa hasa zile sinema za zamani na musicals.

Kwa kweli inahitaji kazi na mazoezi na moyo. Ukiona wakina Savion Glover wanacheza ujue wamejifunza miaka na miaka. Ajabu ni mchezo wa mahesabu, maana lazima uwe na taps kadhaa katika sehemu ndogo ya muziki na zifuate muundo maalum. Huwa inategemea na muziki unayaotumia. Kwa sasa vijana wengi wanapenda Jazz Tap na Hoofing. Hizo staili kidogo una uhuru wa kwenda nje ya muundo wa ku-tap kwa mahesabu.

Kuna mama fulani marehemu sasa alikuwa anaitwa Ann Miller, alikuwa anaweza kupiga tap zaidi ya 500 kwa dakika moja. Ndo mwenye rekodi ya kutap haraka. Wandugu sitafika huko! Sitini kwa dakika moja ni kazi.

Si ajabu unauliza sababu iliyonifanya nianze kujifunza. Ni hivi, nilienda kwenye audition ya show fulani na kuulizwa na nina dance experience. Nikasema najua kucheza ngoma za East Africa. Wao walisema wanataka watu wanaojua ngoma za hapa USA kama ballet na tap. Basi ikabidi ninunue viatu na nitafute darasa! Mwanzo ulikuwa mgumu lakini sasa sioni kitu cha ajabu sana. Na naona raha kuwa naweza kucheza wimbo mpaka mwisho bila kukosea. Na next time nafanya audition wakisema wanataka nicheze dance niko tayari kuwa 'tapia'!

Kama uko Marekani au Ulaya bila shaka kuna studio karibu na wewe inayofundisha tap dance.

6 comments:

Anonymous said...

Haya ndio mambo tunayotaka kuyasikia!. Chemi please endelea kuweka hizi positive pictures na more developments zina impact kubwa sana kwa watu wengi kuliko unavyofikiri. I am so proud of you!.
During the day nilikuwa napenda kucheza mziki na ili kuonekana kama unafanya kitu ni lazima ujue kucheza Chacha, Reggae, funk, soca na of course Robot. Nilikwenda Club Jumamosi kukumbushia walipiga a lot of oldies nilicheza sio kawaida. Tap inataka a lot flexibilty, control na good frame of mind. I am sure Tap na Ballet zina hitaji skills nyingi zaidi na long practices.
GO CHEMI YOU GOT WHAT IT TAKES!

luihamu said...

WAKATI MIMI NATAFAKARI AFRIKA INAELEKEA WAPI,WEWE UNATAKA KUCHEZA(ROCK)WAKATI WA AFRIKA WANASHIDA KIBAO WEWE UNATAKA KUCHEZA(ROCK)WEWE NI MWAFRIKA KWELI?JAH LIVE.PEACE.

MICHUZI BLOG said...

Chemi!
Naku-admire sana kwa vipaji lukuki ulivyonavyo na unavyozidi kuvumbua. Keep it up! Natumai sie utakuja kutufundisha pia

John Mwaipopo said...

Nakufagilia wawa! Unabidii sana ya kujifunza mambo mageni kila uchao. Kila la heri. Kama alivyosema kaka michuzi natumai utakuja kutufundisha siku moja.

Anonymous said...

Haya Chemi,
ujumbe niliouchukua ni mmoja tu, kuwa kama ukikwama sehemu kwa sababu huna ujuzi au elimu fulani basi usisite kurudi shule. huu ni mfano wa kuigwa na wote watafutao maisha bora.

Anonymous said...

Chemi,
Mimi nilikuwa naona dansi ya kugonga sakafuni na viatu (tap dance) kwenye sinema. Miezi miwili iliyopita ndio niliiona moja kwa moja hadharani (live).

Hongera kwa kuingilia dansi hii. Pia namuunga mkono Michuzi alichosema kuhusu vipaji vyako.