Saturday, October 28, 2006
Washindi wa 2006 ni Cardinals!
Ukikaa Marekani lazima utasikia habari ya mchezo BASEBALL! Zamani sikuwa na habari na huo mchezo na wala sikuujali lakini siku hizi mimi nimekuwa mshabaki! Kila mji Marekani una timu yake. Miji mikuu ina timu kubwa na wachezaji wanalipwa donge nono. Naona kama watu wana mapenzi na Baseball zaidi ya watu wanavyokuwa na mapenzi ya mpira wa miguu Tanzania.
Jana jioni timu kutoka St. Louis, Missouri iitwayo, Cardinals, walishinda timu kutoka Detroit, Michigan iitwayo, Tigers. Cardinals ni aina ya ndege na Tiger ni aina ya paka kubwa, sasa ungetemea Tigers washinde. Lakini Cardinals walinyakuwa ushindi wa World Series, yaani kuwa timu bora ya baseball ya mwaka 2006. Hongera kwao.
Ukweli nilikuwa nashabikia Tigers. Sijui kwa nini, lakini napenda sana wakicheza kwenye uwanja wao Detroit. Kila wakipata bao (score), na kukanyaga Homeplate basi unasikia mlio wa Tiger halafu macho ya sanamu ya Tiger wao yana waka na kucheza cheza! Kama wangefanikiwa kushinda World series sijui huyo Tiger wao angefanyeje.
Safari ya wacheza baseball ni ndefu kila mwaka. Wanaanza msimu wao April na kucheza na timu mbalimbali na kupunguzwa mpaka wanapata timu bora kwenye mchezo wa World Series. Tofauti na michezo mingine kama Football, wachezaji wa baseball wanacheza karibu kila siku na siku zingine hata game mbili kwa siku! Na kuna washabiki ambao hawakosi hata game moja ya timu wao.
Baseball ni mchezo uliyoanza marekani. Zamani weusi walibaguliwa na hawakurusiwa kucheza japo kwenye timu za weusi tupu. Miaka ya 1950's walianza kuruhusu weusi kucheza. Siku hizi kuna wachezaji wengi kutoka nchi za Amerika ya Kusini kama Dominican Republic, Cuba na Colombia. Na pia waJapani na waChina wapo. Wacehzaji wa kizungu katika Major Leagues wamekuwa wachache lakini bado watu wanashabikia.
Watoto wadogo wanacheza kwenye timu za Little League. Uwongo mbaya game zingine ni kama vile game za wakubwa Major Leagues. Watoto na wazazi wa wachezaji wanakuwa tayari kushikana masharti. Mwaka huu kocha wa timu fulani ya Little League alifungwa jela baada ya kumlipa mtoto wa miaka minane kumpiga na kumjeruhi mtoto mwingine kwenye timu yake na mpira kwa vile aliona kama yule mtoto atafanya washindwe.
Navyoona mchezo ni mgumu na lazima uwe na roho kuucheza maana ukipigwa na kale kampira (baseball) utaumia! Mchezaji anajitahidi kuupiga mpira unaoenda spidi kali mno na kamti (bat). Kusudi watu wasivunje mikono wakiudaka wanavaa gloves maalum. Batter ambaye ni zamu yake kujaribu kuupiga anavaa kofia kubwa na ngumu kichwani maana ukipgwa nayo unaweza kufa. Hapa Boston kwenye timu yetu, Red Sox, kuna jamaa, Matt Clement ambaye ni fundi wa kutupa mpira (pitcher) kapigwa kichwani na mpira mwaka jana na hajawa mzima tokea hapo!
Hapa Boston, timu yetu ni Red Sox na walishinda World Series, mwaka 2004. Japo ni timu ya mji wetu mimi siwapendi sana. Ni ghali mno kwenda kwenye game zao halafu tiketi zinauzwa magendo mpaka dola $3,000! Kukaa bleacher ni dola $70 na huoni kitu bila kuwa na binoculaurs!Waachie wenyewe tutazama kwenye TV! Au nitaenda Baltimore na New York kuangalia game huko maana tiketi ni dola $40 tu.
Haya nawaachia nafasi mtoe stori zenu za baseball.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Mie sio mshabiki wa baseball, lakini wamerakani wananiuzi wanapotumia maneno kama "world series" , "world champion" etc.
Mfano Kwenye basketball siku hizi Marekani wanapigwa bao na nchi nyingine duniani.
Pole chemi kewa timu yako kushindwa kwenye fainali
Kweli Annoy umenenena,wamarekani kila kitu wakishakijua wanasema kuwa ni cha dunia.Kweli kwa basketball wanatisha sana lakini huwezi kuwaita ni World champion sababu mashindano yaliomalizika kule Japan walitupiliwa mbali na nchi zilizokaa kimya ambazo haziijiti ma world champion.
Kwa Baseball nimechemsha sijui kitu hapo
Post a Comment