Thursday, December 07, 2006

Dar es Salaam kuna Joto!


Jamani Dar kuna joto! Loh! Unapigwa nayo ukishuka tu kwenye ndege. Siku mbili za mwanzo nilivyokuwa huko niliona joto kweli. Ni kweli kuwa Novemba/Desemba joto unazidi Dar, lakini kwa kweli nilikipata. Kwa siku nilikuwa na kunywa maji mengi kweli, na vinywaji vingine. Jamani nilitoka jasho zile siku za mwanzo.

Halafu mara nyingi umeme ulikatika kwa hiyo feni na Air Conditioning hazifanyi kazi, kwa hiyo unaendelea kuchemka. Unakwenda ofisini mwa mtu halafu unabakia kujipepea na gazeti shauri ya joto. Asubuhi, umeme ulikuwa unakatika saa 12 kamili. Basi unaamka kwa sababu feni chumbani unazimika na joto unaanza kuzidi. Hata hivyo siku zilivyopita nilianza kuzoea joto.

Haya nilivyondoka nilianza kusikia baridi kwenye ndege. Nilitamani ningebaki Bongo nifaidi joto. Na kufika Boston nilikaribishwa na snow (theluji)! Unatoka kwenye joto kuingia kwenye snow.

Basi nimerudi Boston na ka-tan. Nilikuwa navaa sleveless Dar, basi unaona kabisa mikono umekuwa Dark. Sehemu zilizokuwa zimefunikwa zilikuwa light. Wazungu kazini waliniuliza kama nimepata 'sunburn'. Nikawaambia hapana ni tan, na sisi weusi tunapata tan pia. Lakini wacha nifaidi hiyo Vitamin E ya jua, maana kipindi hiki cha winter jua unaliona tu. Mambo ya kukaa nje na mwili kuganda shauri ya baridi hatutaki.

13 comments:

Anonymous said...

I'm Kortny,
from Sri Lanka,
and I'm 18 y.o

Hi, Everybody
I've studied English sinse Spring .
It's so hard Language!
I would like like to meet peple and practisice My English with them.

Kiss!!

John Mwaipopo said...

Hiyo ndio Bongo Dar es Salaam. Ndo maana miye najikalia Mbeya. Unitoe unipeleke wapi.

Anonymous said...

Business: The Economy Housing boom continues

UK mortgage lending rose to its highest level in six years - further evidence of the strength of the housing market.
Mortgage lending in June totalled ?11bn, up 21% compared to the previous month and 31% higher than the level one year ago.
--------------





MICHUZI BLOG said...

chemi!

nyumbani ni nyumbani tu...

MICHUZI BLOG said...

nasikitika sana hatukuonana ulipokuja. hata hivyo, i salute you, my dear sister kwa yote unayotupa...

MICHUZI BLOG said...

mwaipopo umenisusa? nitembelee tu nkamu gwangu. siku hizi na-moderate for obvious reasons!

Chemi Che-Mponda said...

Michuzi,

No problem, I will be back soon! I realize how much I missed Bongo! Will send you an e-mail!

mloyi said...

Ndiyo Dar tulivyo, joto letu, mbu wetu, Kunguni, viroboto, chawa, ng'e wote tunaishi mnavyo. Mvua ikinyesha kidogo tuu, tabu! huendi dukani bila kuvua viatu, ukizubaa utakuta maji yameingia mpaka chumbani kwako, na bahati mbaya jirani yako ikiwa siku yake ya kuzibua choo, unalo.
Simu ni nyingi sana, hata mwenye kipato cha USD3.00 kwa siku anamiliki simu na ana uwezo wa kuweka credit kila siku! mambo hayo. Usafiri ni kilekile mabasi yamekuwa mengi kwa idadi,unavijua vipanya, lakini uwezo wake wa kubeba abiria ni uleule iliyokuwa nao UDA miaka ya kati ya themanini huku Dar imekuwa mara tatu yake!.
Jiji nalo halitaki kutanuka, zinakua townships tuu, lakini CBD ni ileile aliyoiacha mwingereza miaka 45 iliyopita, fikiria msongamano usio wa lazima ukiingia CBD! Hata masoko hayakui, bado watu wa maeneo yate ya Dar wanapendelea kununua bidhaa zao Kariakoo shimoni!. Machinga, kama unawajua, sasa kidogo wamepewa red card hawazagai sana kariakoo tumeonja mji usio na shughuli nyingi zisizo za lazima mjini.
fikiria ukitembea barabara ya kibiashara hapo NY, barabara yenyewe ni kubwa na shughuli ni chache sana hata wachomoaji mifukoni,kama wapo, hawananafasi ya kukuchomolea. lakini huku kila uendapo unajihatarisha kuchomolewa au kupanguswa mdudu.
Haya hayatoshi kuielezea Dar, lakini tulikuwa tayari kula majani ili raisi wetu apate ndege binafsi ya kisasa, ambayo tuliishia kubambikiwa, hatukujua kama kuna matumizi ya muhimu kama kununua mitambo ya kisasa ya kutengeneza umeme, ambayo sasa inatugharimu kiasi kikubwa kuliko tulichokataa miaka yote na bado hiyo mitambo siyo yetu!!!!. yote haya yanaendelea kwenye jiji liitwalo Dar ya wajanja wa kujanjiwa.... ............../

Innocent Kasyate said...

Kweli Bongo joto ndio hali halisi lakini ungekaa zaidi hata tusherehekee Christmas.
Naomba ukija tena tuwasiliane: I want to know more about your film activities.
Thanks.

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

Sawubona

I'm glad!

Hur star det till?

Fiance Lawyer Visa
Prepaid Credit Card
Writing Desk
Pole Saw
Batch Concrete Mixer
Bad Credit Home Loan Mobile Mortgage
Demolition Equipment Heavy Rental
Air Bed Cigar
Belly Button Outie
Aegis Mortgage
Used Car Dealer Miami
169k

Catch-you-later

Anonymous said...

Bad Side Effects Of Quitting Lexapro

Can Lexapro Cause Side Effects In Pregnacy

Lexapro And Add

Dreams Side Lexapro Effects

Lexapro And Insomnia

Effects Lexapro Medication Side

Antidepressant Lexapro For Depression In Elderly Patients

Anonymous said...

Chao

I'm glad!

How are you?

Auto Air Condition Repair Agent California Estate Lake Real Tahoe
Sub Contractor Agreement
Utah Motorcycle Accident Attorney
New Bankruptcy Law 2005 Air Conditioning Installation Precast Concrete Balusters
Alexandrite New York Car Insurance
Eddi