Wednesday, December 13, 2006

Nilitolewa Ushamba Dar - Text Messaging


Haya nimezungumza habari ya watu wengi kuwa na cell phone Dar. Sasa kuna hiyo kitu 'text messaging'. Naona ndo mawasiliano ya bei rahisi kuliko voice call. Kila mtu anajua kutuma text message, isipokuwa mimi!

Niliazima simu ya mama yangu. Watu walikuwa wananitumia text message. Doh, niliweza kuzisoma, lakini nilishindwa kutuma jibu! Niliona aibu kweli. Dada moja kanipigia na kusema, 'Nilivyona hujajibu niijua hujui kutumia texting!"

Ni kweli nilikuwa najibu watu kwa kuwapigia simu na of course ni ghali. Japo nina cell phone miaka mingi na nimeona hiyo text feature, huwa nasoma message na kuinua phone na kupiga kama inabidi nijibu. Nimeona vijana na watoto wadogo wanajua kutumia lakini haikuniingia kuwa nami nitumie. Na mara nyingi kwenye TV utasikia, send a Text message to halafu wanakupa namba. Lakini hata siku moja sijajaribu! Jamani USHAMBA! Ni kama vile compyuta. Mtu unaona lakini unaogopa kutumia! Ukianza kutumia unasema, Kumbe ni rahisi hivyo!

Sasa nimerudi Boston, na natazama cell phone yangu. Na ndo nimekuwa na-explore jinsi ya kutumia hiyo text message. Nimeanza kupatia. Lakini naomba mnieleza jinsi ya kuweka space kati ya maneno! Kwa sasa naweka period kati ya maneno.

Kumbe ni simple na mawasiliano rahisi. Nimeanza kupenda text messaging. Ushamba wa text messaging umenitoka.

13 comments:

Unknown said...

pole na mchakamchaka wa text messanging Chemi.kwa bahati mbaya itakuwa vigumu kwa wanablog kukuelekeza moja kwa moja jinsi ya kuweka space kwenye simu yako kwa sababu inategemea na aina ya simu unayotumia na mode of texting.kama hint jaribu kwenye namba 1,o,* au #.one of those should work.

Chemi Che-Mponda said...

Thanks for the tip.

Anonymous said...

We Dada wa ze sixties,hivyo kujua kuandika ki-blog usione you know all.
Why thanking for the trip?It was your money mom.Ooops wabongo ambao hamja enda bongo siku nyingi mna matatizo sana,it`s not your problem.

Anonymous said...

Anononymous wa 10:24 hebu jifunza kuandika English. La sivyo andika Swahili. Mambo ya kuandika broken aibu kweli ndo maana ukajiita anony.

Anonymous said...

Duh,we mwanamama acha kutuzuga!!!.Unajua sana ku-text ila unatafuta mijisifa tu.Loh wabongo bwana!!

Anonymous said...

Ulikuwa kwa mama yako. Wewe ni binti ya Dr. Chem-Mponda wa UD? Kama ndio wewe dada yao Jesca, na Malaika, basi nawafahamu. Mliishi ule mtaa ambao kuna UDASA club, nyumba ya pili from Udasa CLUB.

Chemi Che-Mponda said...

anonymous wa 6:56PM, ndo sisi. Tulikuwa tunakaa 13 Simba Road, karibu na Hall 3. Nitumie e-mail chemiche3@yahoo.com

Anonymous said...

Chemi nimekuandikia e-mail. Fungua uisome. Utakumbuka mambo mengi ya Tanzania.

Anonymous said...

Sister Chemi. This may sound weird, but can someone start a campaign to convince the prosecutor not to send brother Mike Tyson to prison. You the brother has been to prison several times before but that doesn't make it right, even though he was found under influence of drugs, and possession this past Friday. The brother has kids to take care of, and sisters seem not to be around him. If Mike goes to the pen, his kids will miss their dad, and the brother will be depressed so badly. I think the judge should give him probation, so he can be monitored while outside. Pretty much a house arrest. You know we all mess up at some point because we are not perfect.

Anonymous said...

mike tyson committed a crime, he should go to prison if found guilty. i am sorry for mike but this has happened a lot to make him learn something. He is lucky that his kids are in americans, they will be looked after by someone. I got no sympathy with mike , he is the role model to a lot of people in the world. let him learn

Anonymous said...

hey u ms/mr whoever mbona mna tia aibu bongo land namna hiyo mana kanma haujuai saving's naomba uenda chuo cha uhasibu labda wata kusaidia maana cell phone zilikuwepo toka zamani bongo kabla ya mshimdi wa mobiele!!!!!!!!!!(buzz) kulikuwa na kitu kinaitwa cetlitephone kama haukuwa nayo basi muulize michuzi labda anaweza kuku saidia maana wadau wa dar hamjui chochote ndugu zenu wa tabora (nyamwezi) walikuwa tayari wapewa maisha ya cable ahhhhhhhhhhhhhhhh u dont belive ask (TRA tabora) je ? TBC ya tabora imeanza lini ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa pole sana. bongo maisha safi toka enzi hizo. jgrafia kama ime lala utanelewa pole sana. from the williamson mine AAUUUUUUUUUUUUUUUUUUU?

Anonymous said...

read instruction when u buy a phone? wake up usi lale wewe unatia aibu wab ongo tafadhali ms/mr pls think before u write or comment in blog wabongo tupu kila mahali kama wahindi vili chukua safari mexico, jionee peso its like pesa do the math. tafathali naomba tuandike mambo yatakayo wasaidia wadogo zetu sio nyinyi vituko kwa sababu vipimo vinaonysha jinsi gani tulivyo nyuma lps u need 2 wake up!!!!!!!!!!

Anonymous said...

na wewe che-ponda je unajua kwamba posta bongo wana leta arua pamka kwako kama una add! au unafikiri ukiwa na P.O.Box watu leta tafathali soma maelezo kabla hauja chukua kifunguo cha posta!!!!!!!!!!!!tatizo lako ni kuhonga sana ndio maan mna fikiri mambo mengine hayapo bongo yapo toka 1927 by the law chapter!!!! angalia nyuma ya karatasi ya maelezo soma mpaka chini labda utaelewa unafikiri kumlipa !!!!!!!!!!wa daraja la kwanza ndio deal basi kumbe aneumia ndio wewe pole sana kijana wa 80'''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''s