Tuesday, December 26, 2006

Marehemu James Brown







REST IN PEACE JAMES BROWN

1933 - 2006

Jamani nilisikitika kusikia habari ya kifo cha Godfather of Soul, James Brown! Alifariki jana asubuhi, Krismasi, akiwa anaumwa Pneumonia. Lakini jamani Ijumaa mbona alionekana mzima, ana-sign autographs na kutoa zawadi za Krismasi kwa watoto!

Ukweli, mimi ni mmoja wa washabiki wake wakuu. Yaani kila nikisimikia animba 'funk' lazima niinuke na kucheza! Nyimbo zake, 'Say it Loud, I'm Black and Proud!', 'Hot Pants, 'Sex Machine', Get Up, na zingine nyingi haziwezi kusahaulika. Sasa kwa vile ni marehemu bei ya CD's zake zitaongezeka bei.

Nisiseme habari ya jinsi nilivyokuwa nashangalia akicheza na kutia madoido ya 'splits'! Nina mpaka mDoli wa James Brown, una bonyeza mahala na anaanza kucheza na kuimba ule waimbo wake wa 'I Feel Good!' (Najisikia vizuri). Tangu mdogo yaani miaka minne hivi nakumbuka kucheza na kupiga kelele kila nikisikia anaimba, eti najaribu kumwiga!

Mungu amlaze mahali pema mbinguni. Amen.


1 comment:

Anonymous said...

Ingawa ni muda mrefu umepita tangu kifo chake najiunga nawe kumtakia maisha mema peponi. Namkumbuka sana Marehemu James Brown wakati huo tukiwa shule miaka ya 70, ilikuwa ni soul music fever, enzi za akina Aretha Franklin na wengineo weusi waliotingisha. Huku nyumbani tulizipata habari za kifo cha James Brown lakini zilikubikwa na habari za kifo cha aliyekuwa Rais wa Marekani Marehemu Gerald Ford. Endelea kutuhabarisha.