Tuesday, January 16, 2007

Ndoto inaweza kutokea Kweli!




Mimi nimewahi kuota kuwa natuzwa Oscar. Nilivyoamka ilibidi nicheke. Nikasema haiwezekani nituzwe hiyo Oscar, kwanza weusi huwa hawatuzwi, na pili nani atanipa nafasi ya kuigiza kwenye sinema itakayonipa nafasi hiyo.

Lakini jana nimeamini kuwa ndoto huwa inaweza kutokea kweli. Baada ya kuona, Jennifer Hudson, kashinda Golden Globe Award kama Best Supporting Actress. Ijumaa alishinda Critics Choice Awards na sasa watu wanasema anastahili Oscar. Mwaka jana saa hizi nani alitegemea kuwa leo, Jennifer angekuwa Superstar? Ni sinema yake ya kwanza kuigiza, na pia mwaka 2004, alishindwa kwenye mashindano ya American Idol….kama utakumbuka Fantasia Barrino alishinda mwaka ule. Jaji Simon Cowell, alimwambia kuwa hata fika mbali na uimbaji. Kwa kweli nilisikitika sana siku hiyo alivyotolewa kwena AI, maana nilijua Jennifer ana kipaji.

Mungu ni mwema. Akifunga dirisha anafungua mlango. Jennifer kapata nafasi ya kuwa kwenye sinema ya Dreamgirls. Jennifer alichaguliwa kutoka kwenye waigizaji 781 waliofanya audition. Kama hujaiona Dreamgirls nakushauri ukaione. Nilienda kuiona juzi na kwa kweli ni sinema nzuri mno, yaani mno. Sijawahi kuona sinema nzuri kiasi hicho miaka mingi, tena waigizaji wakuu ni weusi. Na waMarekani wametokea kuipenda hiyo sinema. Soundtrack ya sinema ni namba one sasa hivi! Na kila mtu anamsifia Jennifer Hudson na kuigiza na kuimba kwake.

Kwa ufupi, Jennifer anaigiza kama Effie White, ambaye ni mwimbaji mkuu wa Kikundi cha The Dreams. Meneja wa Kikundi (Jamie Foxx) anamshusha na kumweka, Deena Jones, (Beyonce) kuwa mwimbaji mkuu kwa vile ni mzuri wa sura kuliko Effie. Effie anatupwa na kikundi cha chake na anasota na maisha. Sitaki kuwaeleza mengi lakini kuna mapenzi mle. Beyonce naye aliteuliwa kwa ajili ya tuzo ya Best Actress, lakini hakupata.

Eddie Murphy anaigiza kama James ‘Thunder’ Early, ambaye ni mwimbaji mwenye staili ya pekee ya kuimba. Anatokea kupendana na moja wa hao Dreams. Naye alituzwa Golden Globe kama Best Supporting actor. Kama hamkuona show, walivyomtangaza mshindi, alionekana kuwa na mshangao. Sishangai maana alishateuliwa mara kadhaa kwa ajili ya sinema kana The Nutty Professor, na hajashinda hata siku moja. Na huko kwenye Oscars ndo hawajamjua kabisa.

Kwa hiyo ndoto huwa zinatokea kweli. Jennifer Hudson, ametuonyesha kuwa inawezakana.

3 comments:

shamim a.k.a Zeze said...

jamani kumbe ni nzuri hivyo mwenyewe niko na hamu nayooo....hope edie marph atanifurahisha kama kwenye coming to america.....na nina hamu ya kuona uigizaji wa lady B.

wacha tuisibiri ije new world cinema......nawe endelea kuota one day tutakuandika humu umepewa tuzo lol

MICHUZI BLOG said...

Chemi

naungana na mchangiaji wa juu yangu. kwa jinsi ulivyo mpiganaji tena mwenye kipaji (nimeona tulipocheza ile sinema ya khanga n.k.)sioni kwa nini na wewe ndoto yako isitimie. iko siku utapata channel na mambo yatajipa. usikate tamaa dear.one day yes, utakuja nambia...

Kibunango said...

Ni sinema nzuri,Hasa unapojaribu kuona jinsi gani muziki unavyoweza kubadili maisha ya watu!