Saturday, January 06, 2007

Hongera Dada Asha Rose Mtengeti-Migiro



Nachukua nafasi hii kumpongeza Dada Asha Rose Mtengeti-Migiro, kwa kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (United Nations). Kwa kweli ni jambo sisi WaTanzania lazima tujivunie.

Namfahamu Dada Asha Rose, tangu alivyokuwa anasoma UDSM. Mimi wakati huo bado nilikuwa nasoma Secondary School. Kwa kweli huwezi kujua Mungu amempangia mtu nini. Nikikumbuka enzi zile, yaani tusingeweza kutegemea kuwa atakuwa kiongozi anayeheshimika dunia nzima. Alikuwa hana makuu. Lakini miaka ilivyoenda tuliona alivyoonyesha meno kuwa anaweza kuongoza na kuongoza vizuri.

Pia kuteuliwa kwake unaonyesha jinsi Tanzania inavyoheshimika duniani. Hatujawa na migogoro mingi ya kisiasa kama nchi zingine barani Afrika. Na nasikia ilikuwa kila mkutano wa kimataifa akienda anapata washabiki kwa uongozi wake mzuri. Watu wengine wamekuwa wakishangaa alipataje kuteuliwa katika nafasi nzito hivyo. Nawambia ameteuliwa kwa sababu ameonyesha watu wengi Tanzania na nje ya Tanzania kuwa ni mtu mzuri mwenye moyo na kipaji cha uongozi.

Jambo lingine ni kuwa mwanamke kutoka Third World amekababidhiwa uongozi mzito. Lazima Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Ban Ki-Moon, kamwona Dada Asha Rose ni mwanamke jasiri atakayeweza hiyo kazi.

Dada Asha Rose amekuwa ni mfano mzuri kwa wasichana wote wa Tanzania na Afrika kwa ujumla!

Akina Mama Oyee!

5 comments:

Baragumu said...

Ndugu habari zenu,ninaandika hii msg,sio comment ya "Hongera Dada Asha Rose......",bali nimeandika msg hii kuuliza kama nataka kujiunga na hii BLOG,lakini sioni sehemu ya kuji-rejist ili niwe member,ninayo google account,Pls help.

Chemi Che-Mponda said...

Unaweza kunitumia e-mail address yako. Tuma chemiche3@yahoo.com

Anonymous said...

Chemi

Na wewe nikupe hongera kwa kushiriki katika sinema tamu na ya kusisimua kiasi hico...The After Shock...
Nimetazama trailer na kuifurahia sana. Itanipasa kutafuta DVD yake.
Hongera sana mwanamama(dada).

MICHUZI BLOG said...

CHEMI!!

HAPPY NEW (belated) NEW YEAR!

Asante kwa yote unayotupatia humu barazani mwako, nategemea mengi zaidi 2007.

Pia nakutaia afya njema wewe na familia yako, na naomba tena unisamehe kwa kutoonana ulipokuja bongo. Hiyo haikuwa kwa makusudi ila mipango ya Muumba wa yote.

Chemi Che-Mponda said...

simbadeo,

Asante sana. Nina projects zingine mwaka huu pia.

Michuzi,

Asante, Happy New Year to you all well. Usiwe na wasiwasi, nategemea kufika huko tena hivi karibuni.