Tuesday, January 09, 2007

Oprah ajenga shule ya kifahari ya Wasichana Afrika Kusini

Bila shaka mmesikia habari ya Oprah Winfrey kufungua shule ya wasichana huko Afrika Kusini. Shule enyewe inaitwa ‘The Oprah Winfrey Leadership Academy’. Kwa kweli nampongeza kwa kitendo chake cha kukumbuka Afrika na kusaidia wasichana huko. Wanafunzi waliochaguliwa wanatoka kwenye familia zenye kipato cha chini. Na walichaguliwa kutoka kwa maelfu ya wasichana walioomba nafasi ya kuingia huko.

Oprah alijenga shule hiyo kwa gharama ya dola za kimarekani $40 milioni. Kwa sasa ina wanafunzi 145. Bila shaka tutasikia waliosoma hapo watapata mafanikio mazuri kimasomo na kwenda kusoma vyuo vikuu maarufu duniani kama Harvard, Stanford, Cambridge, Oxford etc.

Shule enyewe ni ya kifahari hasa. Hata wanaosoma shule za Ivy League na ma Prep school duniani wanaweza kuwaonea wivu has wasichana. Nikisema ni ya kifahari, nina maana ni ya kifahari hasa. Oprah mwenyewe ni bilionea na kazoea maisha ya kifahari na alitaka hao wasichana wajue ufahari manake nini. Mfano, shule ina saloni kwa ajili ya kutengeneza wasichana nywele, wanalalia mashuka enye nyuzi 200 count (Duh…kama wanalala hoteli ya Waldorf Astoria) sahani zilichaguliwa na Oprah na si ajabu sahani moja ina gharama ya dola mia, ina theatre za ndani na nje, ina ma fireplace tele (Afrika unahitaji fireplace ya nini?) na mengine mengi. Walimu wameletwa kutoka nchi za nje.

Je, wakirudi majumbani mwao kwa ajili ya likizo wataishi namna gani? Si wamezoea ufahari. Si uwongo kuna watu ambao baada ya kukosa maisha ya kifahari waliozoea, walirukwa na akili na wengine kujiua. Natumaini Oprah ana mpango wa kuhakikiisha hao wasichana wanaendelea kuishi maisha ya kifahari wakimaliza masomo yao.

Lakini najiuliza kama hizo pesa katumia vizuri kweli? Nakubali kuwa ni hela yake na anaweza kufanya anachoaka nazo. Lakini jamani hiyo hela ingeweza kusomesha maelfu ya wasichana huko Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla. Kuna faida gani ya mtu kula chakula kwenye sahani enye thamani ya dola mia, wakati huko nyumbani kwake huenda hakuna chakula. Pia watoto wengi Afrika wanashindwa kusoma vizuri shauri ya kukosa mlo wa kutosha. Na kisa cha kulalia shuka enye 200 thread count wakati huko majumbani mwao wanashukuru kuwa na sehemu safi ya kulala. Au wanalala wane kwenye Kitanda kimoja. Kuhusu hiyo saloni si bora wangekuwa wanasukana wenyewe kwa wenyewe, ili wajue sanaa ya kutengeneza nywele.

Samahani lakini navyoona kuna watoto Afrika ambao wangeshukuru kuwa na unifomu na viatu vya kuvaa kwenda shule. Wangeshukuru kuwa na vitabu, na madaftari. Wangeshukuru kama wanakuwa na uhakika wakulipwa ada ya shule, na kuwa na njia ya kufika shule bila bugudha, kama vile school buses. Yaani hiyo dola milioni $40 zingeweza kutumiwa kujenga hata shule kumi bora Afrika na kusaidia wengi zaidi.Hayo ni maoni yangu tu. Wapendwa wasomaji, mnaonaje?

14 comments:

Simon Kitururu said...

Mimi nafikiria kuwa sehemu kubwa ya uamuzi wake kujenga shule hii ni kujipatia therapy mwenyewe.Ukimsikia anavyoiongelea utagundua shule hiyo its not only about the students, its about Oprah herself.Ni njia moja ya kujiponyesha mwenyewe kutokana na yote yaliyomkumba

Chemi Che-Mponda said...

Kaka Simon,

Kwa kweli naweza kukubaliana na wewe. Ni therapy project yake. Lakini navyoona, kama hataendelea kuwapa maisha ya ufahari wakimaliza hao wasichana watapata shida sana. Hata huko SA wanauliza huo ufahari utafikisha hao wasichana wapi japo si vibaya kujua ufahari ni nini.

Anonymous said...

Dada Chemi,
Naona kasomo kajiografia kidogo mwezetu mmh. Kumbuka tu Afrika Kusini kuna winter kama ilivyo boston na Ulaya. Inawezekana baridi isiwe kali kiasi hicho lakini kuna baridi kali kipindi hicho. Ikiwa winter kaskazini kusini ni summer na kinyume chake ni sahihi. Hivyo fire places ni muhimu.
Wachina wanasema ukitaka kumsaidia maskini ale samaki mfundishe kuvua. Ndicho alichofanya kwa hao Wasauzi. Kulisha wenye njaa inakuwa ngumu kidogo maana bado watatka kula maisha yote mwishowe ataishiwa. Bora hivyo mwenye uchungu na maisha atakazana na kutoka. Ukiweka kwenye usafiri wa wanafunzi yatakuwa yaleyale ya mabasi ya wanafunzi Dar:wajanja watakula.

John Mwaipopo said...

Eeh kumbe ndo maana wakati fulani aliwahi kujihusisha kuwa yeye ana asili ya Afrika Kusini. Kumbe ana lake jambo. Hata hivyo ni jambo jemba isipokuwa tumshke sikio watoto hao wasizoeshe raha sana.

Chemi Che-Mponda said...

Skip Gates alimfanyia DNA test, na waligundua hana asili ya South Africa. Oprah alikuwa andai yeye ana asili ya Uzulu. Kabila lake liko huko Liberia, West Africa wanaita Kpelle. Ingekuwa vizuri kama angeenda kuwasaidia pia. Tena Liberia wanafanya re-building.

Anonymous said...

Mimi sioni tatizo kwa Oprah kujenga shule ya hadhi hiyo. Kwa mujibu wa maelezo yake anandaa viongozi wa baadae watakao saidia kukomboa jamii zao na hususani Mwanamke wa Africa. Hivyo kwa mtazamo wa Oprah amejali ubora kuliko uwingi, naona kwa maoni ya wengi Oprah angejali uwingi kuliko ubora - mara nyingi vitu hivyo huwa haviendi pamoja.Kuhusu kama wataishije wakirudi kwenye familia zao ambazo ni maskini, mimi nadhani pia hilo sio tatizo kubwa - bila shaka Oprah atakuwa na wataalamu/walimu wanaowandaa hao wanafunzi kisaikolojia juu ya wajibu wao na nini matarajio ya jamii kwao. Oprah ana mpango wa kuwaalika wazazi wa watoto hao ili waone watoto wao wanishije - kitu ambacho naona pia kitakuwa changamoto kwa wazazi hao. Kwa Mtanzania anayeishi nje ya nchi kama America au Ulaya tofauti ya maisha na nyumbani hasa vijijini ni kubwa sana, sidhani kama ukifika kijijini utadharau au utashindwa kuishi maisha ya kijijini - naamini ni kitu hicho hicho kitatokea kwa hao watoto ukizingatia ni watoto wenye vipaji ndio wamebahatika kupata nafasi hiyo.

Anonymous said...

Mara nyingi watu mashuhuri wakifanya kitu inakuwa ni about themselves - not necessarily those in need.
Tatizo sio kuishije baada ya kumaliza shule. Tatizo ni kwamba watakuwa na uwezo wa kuendelea na vyuo vikuu? Msisahau kule kupata chuo kizuri ni shida sana - na wanaopata sponsorship, whether kwasababu ya affirmative actionau la ni wachache sana.
A

Anonymous said...

Chemi hii habari ya Oprah kuwajengea hawa wasichana shule ya Gharama mimi nakubaliana nayo kabisa. Kwenye mtazamo wangu naamini kabisa kwamba matayarisho mazuri ya kimaisha/ masomo na mwelekeo huleta faida. Oprah hakuchagua wasichana wa kawaida wengi wao au wote ni straight A students ambao wana maisha magumu. oprah kawapa second chance na sijui kama wataipoteza. maana amewapa chance ya ku "aim higher so that the failure can still be a success to the majority".
Ukiipoteza hiyo nafasi kwa kutokusoma utamlilia nani? Nadhani ni jitihada yake binafsi na anatoa mfano kwamba natural Queens are in AFRICA. BRAVO OPRAH WINFREY I LOVE YOU DO MORE TO ENLIGHT ALL THE SUFFERING CHILDREN.

Anonymous said...

Mawazo yaliyotolewa na wadau hapo juu yote yana uhalali.

Ubora vs.wingi, nafikiri hili ni jambo muhimu sana. Ni bora kufanya kitu kidogo ukakifanya vizuri kuliko kufanya vitu vingi ukarashiarashia tu. Vile vle tusisahau kuwa Oprah sio serikali ya Afrika Kusini, inaonaekana wadau wengine wanataka Oprah achukue jukumu la serikali. Yeye ni mtu binafsi, na ana uhuru wa kufanya anachokitaka.

Mimi naamini, kwa nchi zetu za Africa-msaada wowote hasa wa maswala ya Elimu au Afya, utatusaidia sana.
ZIDUMU FIKRA ZA OPRAH!

Israel Saria said...

Mnatakiwa nyie mlioko karibu naye huko USA Mumpe somo juu ya Tanzania..huwezi jua anaweza kuamua kuja bongo na kujenga chuo kiku ..kuuu!!

Anonymous said...

Si uwongo, hiyo $40 million dollars zingetosha kujenga Vyuo Vikuu vinne, au shule za sekondari 400, na primary school 1000. Tena zingekuwa nzuri kabisa!

Anonymous said...

Oprah ni mtu aliyekuzwa na ubeberu, kamwe hawezi sahau hulka hiyo. Alichokifanya ni amali ya kibepari. Bepari haoni faida ya kufaidisha wengi, kwake maisha mazuri ni ukiwa, uchache.Ndiyo maana hata fikra ake zinaelekea kufaidisha wachache ili waingie ktk ulimwengu wa ubepari. Saluni ya kutengeneza nywele ili ziweje? Waafrika wana shida nyingi na kubwa, kutengeneza nywele si mojawapo.

Binafsi sifurahishwi na na mkabala alioufuata. Bila shaka yoyote lililo kubwa kwake ni kutengeneza jina tu na si kusaidia watu.

Anonymous said...

Mara nyingi Waafrika wamezoea kupigana vita wenyewe kwa wenyewe. Kuoneana wivu uliokuwa na mbele wala nyuma ndio chakula chetu. Kuna ubaya gani mwafrika kusoma katika mazingira mazuri? Wamuachi yakhe? Dada wa kiafrika anawasaidia waafrika wenzake imekuwa nongo nongo. Angekuwa mzungu msingesema kitu. Tuache unafiki mwenye uwezo asaidie wenzeke jamani...Namuunga mkono yule aliyesema nyinyi mnaoishi huko USA mkija vijinini mwenu mtashindwa kuishi. Kuishi sehemu mzuri peke yake ni changamoto. Lawama ni dalili ya choyo cha roho. Hebu nyie uliohuko fanyeni njia muulete huyo mama huku Tanzania. Mimi nitampeleka kijijini kwetu www.mzuri-kaja.or.tz anisaidie. La kufanya huko watafuteni watu wenye mapesa waje huku. Mimi niko tayari kutoa maeneo ambayo yatakuwa na majina yao kwa mujibu ya kile walichokifanya au hata kuwapa ulezi wa kijiji changu. Tuacheni kupigana vita. Tusaidiane. Sisi ndio kabila (race)iliyokuwa nyuma duniani. Waasia wanatukimbia na nyinyi ambao mnaishi huko ushahidi wa kutosha mnao. Katika chuo cha Oprah ukimpata mtu mmoja tu mwenye imani kama yake basi mchango wake ni mkubwa mno. Hilo linawezekana. Leteni waswahili wenye pesa Zanzibar mtaona inavyobadilika. Maneno vijineno vya nini? Nampongeza Oprah kwa nguvu zangu zote na Mola amtie peponi. AMIN

Anonymous said...

Oprah has always been my hero,sometimes I feel that she wishes she was a typical African, so what kama ni therapy yake mwenyewe, wazungu kimewauma sana kwamba hawajashirikishwa kwenye zoezi hili ndio manaa maneno mengi, kaondoka kinyemela kwenda south africa na a few of her friends, na amefanya alichodhamiria kufanya, wazungu walitaka atangaze but that was not the case, Oprah is not stupid, she's actually one of the very smart black american womEn I have ever seen, in the next 10years utasikia anaenda kuishi south africa, marekani imekwisha, celebrities wote wanatafuta makao nje, anyways whatever the case she deserves a huge applause for what she did!!
She doesn't need to be an American president to show what she has to offer to the world, she does what she does cause she is Oprah and guess what, SHE IS RICH TOO!!!