Tuesday, April 03, 2007

Afungwa Marekani kwa kutokuvaa Mask! Anaumwa Kifua Kikuu!


Jamani, leo nimeshutushwa na habari ya Mrusi kufungwa jela tangu mwezi Julai mwaka jana kwa ajili ya kutokuvaa mask hadharani. Jamaa amefungwa huko Pheonix, Arizona. Anaitwa Robert Daniels, na ana miaka 27. Anaumwa ugonjwa hatari wa kifua kikuu (Tuberculosis au TB). Kisa cha kumfunga ni kuwa anaumwa aina ya TB inaitwa XDR-TB. Wanasema kuwa ni drug resistant na haitibiki.

Mahakama ya huko Phoenix, inasema kuwa ilibidi Daniels afungwe kwe vile akikataa kuvaa mask (kizuio kwenye mdomo na pua), akitoka nje na kuwa na watu wengine. Walisema kuwa ana nia mbaya ya kutaka kuambukiza watu huo ugonjwa wa TB kwa maksudi.

Habari zinasema kuwa haijulikani atafungwa mpaka lini na huenda atafungwa mpaka anafia huko jela. Baada ya kusoma hivyo nikasema ni kweli wana haki ya kumfunga hasa kama hiyo TB haina tiba. Wakubwa wanasema kuwa kama watu wengine watapatikana na huo ugonjwa itabidi nao wafungwe.

Wataalam wa afya wanasema kuwa kama mtu anaumwa HIVAIDS (UKIMWI) na akipata huo ugonjwa atakufa siku 25 tu, baada ya kuambukizwa. DUH!

Na walivyo na woga na huo ugonjwa jamaa haruhusiwi kuoga kwenye shower. Anatumia wipes (vifutio). Hana TV, simu wala redio. Anasema kuwa maisha yake huko jela ni mabaya kuliko ya mtu alifungwa kwa kosa la jinai.

Chumba chake kina ventilation ya peke yake na filters za chumba zinachomwa moto, na watu waliojifunika kama vile astronauts! Ama kweli waMarekani hawataki huo ugonjwa usambae na siwalaumu.

Mnasemaje wapendwa wasomaji?

Kwa habari zaidi ya kufungwa kwa Robert Daniels mnawaeza kusoma:


3 comments:

Anonymous said...

Baada ya kukohoa kohoa kuna jamaa yetu mTZ alikutwa na TB hapa ulaya, akawahishwa hospitali utadhani ni emergency, wakampa chumba kumlaza anywe dawa kwa muda wa wiki mbili humo hospitalini. Tulipokwenda kumuona mgonjwa wetu, tulipewa masks tukavaa kila siku na pia tulipotoka tukanawa na hibitane. Wana darasa wenzake na pia alokuwa anakaa nao floor nzima walipimwa. Ja, TB ni notifiable nchi hizi.

Anonymous said...

ni sawa walivyofanya kwa kumfunga lakini nahisi kwa kumnyima simu, televisheni na kukoga chooni (shower) kama wenzake huo ni uonevu. kwanini asingeliwekwa kwenye chumba peke yake na kupatiwa huduma hizo au hata kusikiliza redio kutapelekea maambukizi.
ninahofia huyu mgonjwa atakufa kwa ukiwa zaidi kuliko maradhi.
hakuna anayeomba maradhi hasa mabaya kama haya sasa tujifikirie mimi na wewe, Mungu atuepushie mbali lakini pindipo ukitokezea ugonjwa huo tutakluwa radhi kufanyiwa namna hiyo???

Anonymous said...

Sasa na yeye kama alijua anaugonjwa contageous hivyo mbona hakuvaa mask kama alivyoshauriwa na Daktari?mambo mengine ni ya kujitakia, mi naona sawa tu afungwe, si pia unakumbuka yule tenager aliyeshuswa kwenye ndege kwa sababu ya kukohoa kupita kiasi, kuna sheria za kiafya ambazo zinaruhusu mtu kuadhibiwa endapo hatafuata ushauri wa daktari kwa manufaa ya kuokoa maisha ya wengi.