Miaka 43 iliyopita, siku ya leo, marehemu Mwalimu Nyerere alichanganya udongo kutoka Tanganyika na udongo kutoka Zanzibar kama ishara ya Muungano wa nchi hizo mbili. Nchi iliyounganishwa ukaitwa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA (United Republic of Tanzania).
Kama wewe ni Mzanzibar au Mtanganyika wewe ni MTANZANIA! WaTanzania tunajivunia kwani sisi ni mfano mzuri kwa waafrika wenzetu na dunia.
WaTanzania tumepitia mengi lakini bado tuna Muungano wetu.
Mungu alinde Muungano wetu. Tuendelee kukaa kwa amani. Mungu Ibariki Tanzania!
***************************************************************************
Wafungwa wasemehewa!
Wafungwa wasemehewa!
Ni mila ya marais kusamehe baadhi ya wafungwa siku ya leo. Taarifa zinasema kuwa Rais Jakaya Kikwete amesamehe wafungwa 4,022.
Katika kuadhimisha miaka 43 ya Muungano, Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 4,022. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nchi leo imesema waliofaidika na msamaha huo ni pamoja na wale wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano ambao hadi jana walikuwa wameshatumikia robo ya kifungo chao.
Kwa habari zaidi nenda: http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2007/04/26/89258.html
10 comments:
Umejivunjia heshima kwa kuweka Konyagi hiyo, mwamnamke kuwa mlevi wa Konyagi siyo sifa nzuri. Kama ulikuwa unaigiza umejichafua tu.
anonymous wa 3:58PM, tangu lini Konyagi imekuwa kinywaji cha wanaume tu? Heh! Ujue kuna usawa katika kila kitu na hata kwenye unywaji wa pombe!
AKINA MAMA OYEE!
huyo anaesema umejivunjia heshima ana lake jambo tangu kule kwa michuzi nimeona yaani dunia ya leo mwanamke bado asinye pombe?kinachotakiwa mwanamke akinywa awe na displine,mfano asikae vibaya ,asilale na wanaume ovyo n.k sasa kama hapo chemi ana kosa gani yuko zake ndani anasherehekea muungano mwenyewe kamvunjia nani heshima tutole mambo ya kishamba huko mwanamke kuinjoi babu eeh
dada Chemi kama unavyowapa ushauri watu wengine pokea ushauri huu wa bure. Tembela gym kidogo kwa ajili ya afya yako halafu ongeza matunda na vegetable katika mlo wako maana afya hiyo inayumba sijui kama unafahamu. si kama ujipunguze kama wazembe wengine wanaoenda gym kujikamua bali kata kidogo hayo mafuta mshikaji wangu. Nimemind blog yako.big up dada ngu
si suala la mtu kuwa mshamba kumshauri dada Chemi kuacha kinywaji hicho ni ustaarabu tu. Maji hayo ni makali kwa afya ya mwanamke labda kama hajipendi kiasi fulani ila kama anapenda kunywa achague kinywaji kitulivu chenye kwa afya, maji hayo si suala la mwanamke au mwanamme yanakamua maini na koromeo kichizi na biological make up zetu hazitufanyi tuwe sawa na wanaume hata tuimbe wimbo wa usawa hadi mawingu yashuke haitatokea we are different and that is well understood hata kwetu wanawake vile tunafumba macho tusione kuwa tunaweza kuwa sawa katika gender roles lakini sio sex roles. nafikiri hizi terms kwako dada Chemi ambaye ni feminist unazielewa vizuri zaidi. usijidanganye kama kwa kunywa Konyagi unatafuta usawa na wanaume that is part of gender not sex mama maini na makorokoro yako ya ndani kama mwanamke yakiungua si sawa na mwanaume hawabebi mimba hao well labda pia huna mpango wa kuzaa. ukipenda ushauri huu chukua bure ama sivyo kata kilaji hicho kwa kwenda mbele tu mwanaangu.
Pombe ni pombe! Basi na akina mama waache kunywa bia maana nayo ina alcohol pia.
Jee unajuwa kwamba jina Tanzania alilitowa mtu wa asili ya kihindi mwenye itikadi ya ki-bohora, alikuwa akiishi Tanga na kwa sasa anaishi uingereza? (yupo hai), nani anaweza kunikumbusha jina lake? just kuelimishana!
4M's,
Daily News walitoa story miaka ya 80 kuhusu huyo jamaa. Nimemsahau jina.
Jina lingine liliopendezwa lilikuwa TANGIBAR.
Duuh, hilo la Tangibar lingechaguliwa ingekuwa kasheshe. hata sijui hapo muungano wa afrika mashariki utapowadia tutaitwaje, United States Of Eastt Africa? loooh, UGATANKEN, TANKENUGA, KENTANUGA? i THINK kentanuga UNALETA KIDOOOOGO!!!!
Kulikoni KENTANUGA, warudishe jina la zamani la eno hiyo.... AZANIA!
Post a Comment