Wednesday, April 11, 2007

Sinema ya ROOTS




Tangu jumapili TVOne, wamekuwa wakionyesha sinema kabambe ya ROOTS. Hiyo sinema ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mwaka 1977 na kuingia katika vitabu vya historia kwa watazamaji wengi. Zaidi ya watu 130 milioni nchini Marekani walitazama.

Nasifia sana hiyo sinema maana inakumbusha watu na hasa waMarekani weusi kuwa wametoka mbali. Inaonyesha kuwa waafrika walikuwa na utamaduni na mzungu alijaribu kuifuta kwa kuzuia watumwa kutoongea lugha zao, kuchukua majina ya kizungu, na walizuiliwa kufanya kitu chochote cha kiaafrika. Katika Roots unamsikia binti Fanta, akisema mimi nimesahau kila kitu cha Afrika, nia yangu niishi. Na utasikia watumwa waliozaliwa Marekani wanavyowakashifu watumwa waliotoka Afrika. Watumwa wanajiona bora kuliko wale waafrika.
Roots ilitungwa na marehemu Alex Haley. Inahusu historia ya familia yake na inaanzia kijiji huko Gambia, na kuzaliwa kwa Kunta Kinte. Kunta anakamtawa na kuletwa Marekani. Ukiona walivyokuwa wanasafirisha weusi utalia. Huko nakumbuka dada moja mmarekani mweusi kaniambia eti kafurahi kuwa mababu zake waliletwa kama watumwa kutoka Marekani maana ana maisha bora na hashindi njaa. Pia inasikitisha ukiona Kunta Kitne kafungwa cheni shingoni na wanam-pat kichwani kama mbwa!
Huko mashuleni Marekani ni lazima vijana watazame sinema ya Schindler's List kusudi waelewe wayehudi walivyouliwa na Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Sasa kwa nini isiwe lazima watazame ROOTS kusudi waelewe history ya mwafrika Marekani na mateso waliopata.
Ukitazama Roots, pia utaweza kuelewa vizuri zaidi matatizo yanayowakabili wamarekani weusi kwa sasa. Matatizo mengi yanatokana na historia yao ya utumwa. Na kwa maoni yangu wengi bado wana mawazo ya kitumwa.
Leo wataonyesha tena TVone sehemu ya nne. Itatoka kwenye DVD May 22.
Karibuni mtoe maoni yenu.

6 comments:

Anonymous said...

Mimi nilisoma kwanza novel ya ROOTS mwaka 1984 kabla sijaona sinema yake. Ni kitabu kizuri sana, kimeandikwa katika msingi imara wa habari zilizotafitiwa kwa umahiri mkubwa, ni zaidi ya tasnifu nyingi za shahada za uzamivu (PhD). Hata hiyo sinema haina utajiri wa taarifa na maarifa kama ilivyo kwenye kitabu hicho. Nawashauri mnaoweza kukipata kitabu hicho mkisome, hasa mlioko huko Marekani nadhani kinapatikana kwa urahisi kuliko huku nyumbani. Ni nafasi nzuri ya kumrejeshea mwafrika ufahamu wake kuhusu nafasi yake katika ulimwengu huu wa kibaguzi na wa kibeberu, kujenga utaifa wa kiafrika (African Nationalism) na kukataa utumwa wa kiakili (mental slavery). Asante dada Chemi

Anonymous said...

Kuna mdau kasema kwamba huko Marekani weusi kwa weusi wanabaguana, kwa kutambuana kwamba huyu ni mzawa na yule ni wakuja. Kwa mtindo huo hata hiyo mental slavery unayoisema kuitatua ni shida. Waafrika bwana sijui tumerogwa au tuna mapepo ya ubaguzi. Anyway wahenga walisema "If you can't fight join them" Yungiz

Anonymous said...

Chemi asante kwa bandika bandua ya stori wiki hii, zote ni nzuri sana.
Hiyo dvd ya roots ikitoka tupe habari ili tuifuatilie. usisahau kutupa bei yake pia maana itatoka huko US kwanza!!!

Anonymous said...

Da Chemi napenda unavyoandika yaani nikisoma nanogewa kweli wewe mwandishi uliyekubuhu haswa.nafikiri unaweza kuandika poetry pia.au?

Anonymous said...

Watu waishio US una access kwenye public library itaipata the roots mimi nimeicheki kama miaka miwili ni ndefu sana kama 4 parts.huwezi kuangalia mara moja ukaimaliza ila itakusisimua ila mbaya na unawezapata asira mbaya mno

Anonymous said...

Hiki ndio kitabu changu cha kwanza kukisoma kama "novel"ilikuwa 1988 sijawahi kukuchoma na pia series zake nilifanikiwa kuzipata Nika angalia zote kwa mababu zetu wamepitia wakati mgumu sana zama za utumwa America.