Sunday, December 27, 2009

MNigeria Mgaidi!


Bila shaka mmesikia habari za kijana wa KiNigeria, Umar Farouk Abdulmutallab, aliyejaribu kulipua ndege ikitua Detroit siku ya Krismasi. Kama angefanikiwa ingekuwa pigo kubwa.

WaNigeria na familia ya jamaa wanasema wanaona haya na jamaa amechafua jina la Nigeria! Mimi nasema kachafua jina la Afrika kwa ujumla! Lakini jamani, huyo kijana ni mtoto wa tajiri, millionea. baba yake alikuwa mkuu wa benki. Sidhani kama katika maisha yake amekuwa na uhaba wa pesa au njaa. Akitaka ananunuliwa, tena mtoto wa kiume! Lazima familia yake walimwoanesha upendeleo fulani. Halafu anaamua kufanya kitendo cha kigaidi. Kwenye taarifa ya habari wanasema Nigeria imejaa maskini na huyo kijana kweli alikuwa na maisha ya kifahari.

Inasikitisha. Ubaya zaidi kitendo chake kitafanya waNigeria na waafrika kwa ujumla kupata shida zaidi wakati wa kuomba visa za kuja Marekani. Pia watachunguzwa zaidi wakisafiri kwenye ndege.

Habari zinasema kuwa baba yake mzazi Umar, Al Haj Umaru Mutallab, alipeleka taarifa kwenye ubalozi wa Marekani huko Lagos, kuwa alikuwa na hofu kuwa mwanae ameingia kwenye kikundi cha kigaidi. Naona baba yake ni shujaa ingawa waMarekai walizembea. Lazima kilimwuma kuona mwanae anafanya maajabu, lakini aliona umuhimu wa kulinda maisha ya wengine.

Na mimi sasa nachukia kuwa kusafiri kwa ndege itazidi kuwa shida sasa. Utakaguliwa kila kona mpaka chooni sasa! Mwisho itabidi uvue mpaka chupi!

Kwa habari zaidi someni:

7 comments:

Anonymous said...

Mshenzi huyo! Ningeshukuru kama ningelipiwa kila kitu katika masomo yangu U.K. na nisiwe na wasiwasi na kitu! SHENZI TAIPU!

Anonymous said...

kwani da chemi lazima m-baki marekani? si mrudi kwenu afrika? kama mnataka lazima m-baki marekani muwe tayari kupekuliwa mpaka chupi. ukienda kwa warumi uwe kama mrumi. otherwise mrudi kwenu.

huyo kijana kakosa malezi ya wazazi. wakamatwe hao wazazi wajibu hoja.

Chemi Che-Mponda said...

Na jioni hii nilikuwa naongea na marafiki zangu. Tulisema tuzoee ku searchiwa mpaka chupi! Pia kila mwafrika akienda chooni kwenye ndege atasindikizwa! Au watakuwa wanamwangalia kwa wasiwasi!

Anonymous said...

asante Yesu, ni maombi tu ya watakatifu wa Mungu kwenye ndege hiyo, Mungu mwema sana

Anonymous said...

Baba yake akuwa tajiri sana kama vyombo vya habari vilivyoripoti. Kwa ujumla, baba yake alikuwa na kipato cha kawaidi and siyo kama tajiri vile, kama utakumbuka, kwenye CNN walionyesha hadi sehemu ambayo wazazi wake wanaishi, na mtangazaji alisema kuwa eneo hilo siyo la matajiri sana...kwa hiyo hizi arguments kuwa anatoka kwenye family tajiri it is nonsense. Hawa Waislamu wenye siasa kali wanaweza kukuchezea mtu wa aina yeyote, wanaweza kucheza na akili yako nawe ukawafuata...

Kuhusu kupekuliwa hilo huwezi kulikwepa, lakini hii unayosema kuwa kwa kuwa ni muafrica hata ukienda chooni watakuwa wanakuangalia...pia hilo sikubaliani nalo, mbona waarabu wamefanya makubwa mabaya lakini wanaenda chooni kama kawaida....a

Anonymous said...

Mjinga kweli! Anajilipua halafu nani afaidi warabu?

Anonymous said...

Haya ndio matokeo ya kusomesha watoto bording wala hujui wanaongea na nani huko, mzazi hauko karibu kujua ni marafiki gani anahusiana nao, hela peke yake haikuzi mtoto, mzazi unatakiwa uwe kwenye maisha ya mtoto kumuongoza njia sio kulipa hela tuu na kuacha majukumu yako ya ulezi.

Tumeshaona hata kwa watoto wa kitanzania wanaosoma nje ya nchi bila wazazi kuwepo karibu yao kujiingiza kwenye tabia zisizoeleweka mfano wale vijana waliomtesa mpaka kuua mtoto wao mchanga hapo Chicago yote hayo ni matokea ya watoto wa wenye pesa kukua bila maadili ya kueleweka. Wanaokotaokota tabia tuu. Inasikitisha sana.