Tuesday, March 09, 2010

Unayanyasaji wa WaBongo Saudi Arabia - II

wanablog na watz wote.
habari za kazi na poleni kwa juhudi zenu za kuwahabarisha watanzania kwa njia ya mtandao. nawatumia link hizi kuonesha hali halisi ya raia wa kigeni wanaokuja kutafuta maisha saudia jinsi wanavyofanyiwa. hatua hii imetokana na mimi mwenyewe kuwa nipo katika matatizo haya lkn mbaya zaidi kuona kuwa walionileta kutoka huko tz wanaendelea kukusanya vijana wengine kama mimi na kuwadanganya kwa kuwaahidi maisha bora wakifika huku saudia.
link hizi ni za vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiripoti manyanyaso haya sio tu ndani ya saudia bali pia nje ya saudia lakini kwa makusudi serikali ya hapa inafumba macho na kujifanya kuwa inatenda haki. wapo waliouwawa, waliopata ulemavu wa kudumu, nk na daima makosa huwa ni ya wageni. wasaudi hawana kosa hata kama wataua au kumpa mtu ulemavu. nchi nyingine za asia zimeanza kuzuia raia wao kuja kufanya kazi hapa kutokana na hali hiyo.
vyombo vya sheria ndio kabisa kuanzia polisi hata mahakama. kwanza ukifika kulalamika utaambiwa hatujui kiingereza zungumza kiarabu kama hujui ukatafute mwanasheria. sasa mshahara wenyewe riyal 500 hadi 800 (riyal 1 ni tsh 300) utamlipa mwanasheria gani? pili huyo jamaa unayemlalamikia ni bilionea hivyo hata polisi hafiki utasikia unajibiwa huu ni uzushi msaudi hawezi kufanya hivi nenda zako. hapo kesi imeisha.
naomba musambaze taarifa hizi kadri muwezavyo hata kutumia magazeti, redio na tv ili vijana wenzangu watz kama mimi wanaotafuta kazi za udereva, uhouse girl, kuuza maduka, kwenye viwanda na makampuni nk wasidanganywe na kuja kupata mateso kama yaliyonikuta mimi hivi sasa.
tafadhali pokea link hizi.....

2 comments:

Anonymous said...

Asante sana na pole sana kwa kutupa habari hizi za kusikitisha. Nadhani hili ni onyo la kutosha kwa Watanzania wote na Waafrika kwa ujumla wanaodhani kwamba maisha ya ughaibuni ni rahisi.

Zaidi ni kwamba haya uliyoyasema, sio mara ya kwanza kutokea, au kurepotiwa. Raia wa nchi kama Philippine, India, na Somalia wamekumbwa sana na haya matatizo katika nchi za Uarabuni na kwingineko duniani.

Lakini nadhani itakuwa ni makosa kuweka dhana kwamba ni waarabu peke yao ndio wanaofanya mambo haya. Leo hii tunaongeelea Saudia kwa sababu ya ujasiri wako, lakini haya mambo yanatendelka dunia nzima. Ni juzi tu tumeshuhudia WAAFRIKA kule ITALY wakinyanyaswa na kuuwawa mbele ya polisi kwa sababu ya kutokuwa na makaratasi, au kuingia kwa kupitia njia za panya. Hata wengine ni RAIA AU WANAISHI kihalali kabisa, lakini wanaishi maisha ya kunyanyasika kuliko hata walivyokuwa makwao (AFRICA).

Hapa Marekani, hali ni hiyo hiyo, kuna wageni weengi sana hapa ambao wanaishi maishi ya kunyanyaswa, kuteswa, na hata kupigwa au kutolipwa mishara kabisa kwa sababu ya ungonge wa kutokuwa na karatasi. Malatino na Waafrika wasiokuwa na makaratasi wameisha zoea haya matatizo.

Kwa maoni yangu, suluhisho ni gumu kupatikana, kwa sababu ni wachache sana wenye moyo kama wa huyu bwana wa hata kudiriki kulileta kwenye BLOGS za watanzania ili watu wajue kinachoendelea.

Na pili, shughuli nzima, kuanzia recruitment mpaka malipo, huwa yanahusishwa VIKUNDI VYA KIJANGILI, hivyo basi, serikali na vyombo vingine vya dola huwa vinawekwa kando, au havitaki kujua kinachoendelea, ingawa wanaona yanayotendeka.

Mwisho kabisa ni kwamba, kutokana na hali ya maisha ya nyumbani, na ukosefu wa ajira, ukimuonya mtu anakuona kama lengo lako ni kufaidi mwenyewe. Kwa hiyo, kuna watu kama kumi ambao wapo tayari kuchukua nafasi yako wakati wowotw ule. Kwa hiyo, hizi ni miongoni mwa sababu ambazo hii HALI HAITAWEZA KAMWE KUISHA.

La msingi ni kwamba, hakikisha UBALOZI WAKO (KAMA UPO HAPO ULIPO)wanataarifa kwamba upo, na kinachoendelea. Suala la kama wataweza kukusaidia au la ni lingine, kuliko kukaa tu bila ya muwakilishi wako kujua kinachoendelea.

NB:UNYANYASAJI HAUNA DINI, RANGI, KABILA, WALA UTAIFA. UPO KILA MAHALI.

Anonymous said...

Dah! Aisei kumbe ndo hivyo! Polseni sana. Naomba serikali isaidie kurejesha watanzania wanoataka kurudi nyumbani.