Thursday, July 29, 2010

Ombaomba Afanya Fujo Back Bay Boston



Wadau, kwenye saa nane na nusu mchana leo nilienda kwenye lunch break Copley Square hapa Boston. Kufika Back Bay Dartmouth St nje ya kituo cha treni na basi, nilishangaa kuona huyo ombaomba anayetumia wheelchair kazuia basi la abiria na hiyo kiti chake. Wakina mama weusi walimzunguka na kumsihi aache kufanya fujo barabarani maana ataenda jela. Mwingine alimwambia kuwa anafanya maksudi kusudi apelekwe hospitali ili apate chakula na sehemu ya kulala. Jamaa alisema kuwa dereva wa basi alimzuia kupanda hiyo basi kwa vile kiti chake kilikuwa na huo mti wa kutundika dawa. Alisema kuwa naye aliamua kuzuia basi isiene popote mpaka aruhusiwe kupanda. Baada ya dakika tano hivi, jamaa aliondoa kiti chake na basi iliendelea na safari. Bahati yake polisi hawakuwa karibu.

Kitu kingine, kumbe huyo jamaa mzima anaweza kutembea! Siku zote nilidhani hawezi kutembea.

3 comments:

Anonymous said...

Dunia hii kuna mambo kumbe hata huko nako wamo? Ingekuwa hapa bongo sijui tungezungumza mengine!
Mbona hilo basi limeandikwa out of service lakini lipo barabarani?

Chemi Che-Mponda said...

Ile basi iliwa Route 10. Lakini jamaa alivyozuia basis ilibidi dereva abadilishe bango na kuita polisi. Wakati mwingine kama kuna fujo ndani ya basi utaona bango inasema EMERGENCY CALL POLICE. Walio ndani hawana hata habari.

Anonymous said...

Na hizo ni Eletronic signbord sio bango lilioandikwa na chaki kama ubungo kuna keybord na pia shotcut key eg press No 5 ni information ya call police no 4 ni out of order NK