Saturday, July 17, 2010

Pombo Mtundu 'Moko' Azikwa New Zealand

Nzoga ya Moko alivyokutwa kwenye kiswa cha Matukana
Moko katika Uhai Wake

Pombo (dolphin) mtundu sana, 'Moko' ambaye alikuwa anapenda sana kucheza na binadamu baharini na hata kuokoa nyangumi amezikiwa kwa heshima huko New Zealand. Kwa vile alizikwa nchi kavu, pombo na samaki wengine wa baharini hawakuweza kuhudhuria mazishi yake.

Moko alikutwa amekufa kwenye kisiwa cha Matakana huko Tauranga, New Zealand. Wataalam wa bahari wanafanya uchunguzi kugundua nini kilimwua.

Moko alikuwa kipenzi cha wenyeji na watalii. Alikuwa na mchezo wa kupindua maboti aina ya kayak. Alikuwa anapenda sana kuchokoza watu kewenye surf boards. Aliwahi kumpeleka mama moja aliyekuwa kwenye surf board kwenye maji marefu baharini halafu aliiba board yake. Yule mama alibakia ku'angania buoy mpaka watu walikuja kumwokoa.

Alipata umaarufu mwaka 2008 wakati nyangumi wawili walikwama katika maji mafupi. Maisha yao yalikuwa hatarini, lakini Moko aliwapeleka kwenye maji marefu na wakaenda zao.

Huko New Zealand, Moko kazikwa kwa heshima. Nzoga yake ilizikwa ndani ya jeneza rangi ya bluu, na hata head stone.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.stuff.co.nz/nelson-mail/news/national-news/3900065/Competing-claims-for-Moko-the-dolphins-remains


http://www.csmonitor.com/From-the-news-wires/2010/0716/Dolphin-funeral-draws-hundreds-of-humans-but-no-other-dolphins

5 comments:

John Mwaipopo said...

siku akifa pweza paulo (octopus paul) yule aliyetabiri sahihi mechi za ujerumani na ile ya fanali sijui itakuwaje. sijui wajerumani watampa heshima ya kutabiri sahii (hata kufungwa kwa wajerumani world cup) au watamshiti kwa kuwa alitabiri wasivyopenda wao.

Anonymous said...

Moko kafa jamani! Lazime tuwe na majonzi! Nashangaa hawakufanya national day of mourning for a fish.

Anonymous said...

Ina maana umesahau Kiswahili au mimi ndie sijui? Nzoga ndio nini. Neno sahihi ni Mzoga halafu itakuwa "wa" siyo "ya" acha kuandika Ki-Manda. Mwalimu Mwaipopo unasemaje hapo?

John Mwaipopo said...

typing error

Anonymous said...

Asante sana Mwl Mwaipopo, nasimamia pale pale hiki ndio kiswahili cha Chemi. Ningeelewa kuwa ni typing error kama angeandika Nzoga wake, hapo ningejua alikusudia Mzoga wake. Lakini Nzoga yake tena kwa kurudia rudia hapana haikubaliki. Between huyu ni mwandishi mkongwe na siyo kanjanja, editing ulichoondika nisehemu ya mafunzo. Asante