Wednesday, November 03, 2010

Gavana Mweusi wa Massachusetts Ashinda Uchaguzi!


Gavana wetu, Mh. Deval Patrick, ameshinda katika uchaguzi wa jana. Ataongoza mkoa wa Massachusetts miaka minne zaidi. Gavana Patrick ni mweusi wa kwanza kushika wadhifa huu na kuwa kachaguliwa tena inasema mengi. Yuko katika chama cha Democrats. Kwa kweli watu wengi hawakutarajia kama atashinda. Aliwaudhi sana baadhi ya wazungu hapa na siasa zake za eti kupendelea maskini na wahamiaji. Lakini ukweli Gavana Patrick amejitahidi sana kunyanyua Massachusetts katika uchumi mbaya. Haya kapata miaka minne mingine ya kuongoza Massachusetts. Wazungu kibao wametangaza kuwa wataondoka Massachusetts na kuhamia mikoa mingine. Na sisi tunasema, "GOOD-BYE!" Lakini mbona alivyoshinda kwa mara ya kwanza mwaka 2006 walisema hivyo hivyo na bado wapo! Chekeni!

4 comments:

Anonymous said...

i take an offence when you call governer mweusi...when it should be african american...c'mon dada...acha hayo lugha ya whites!

Anonymous said...

Kweli kuna wazungu ambao hawajafurahi ushindi wake. Wanaona kuwa Obama atashinda tena na hawana hamu kuongozwa na weusi.

Anonymous said...

Wapeni mbeleko wajibebe na tea party zao, wamwalike na malkia kabisa kwenye hizo chai za jioni. Wakihama waambieni waafrika ambako hawajafika ni mwezini tu lakini dunia nzima wapo!

Anonymous said...

Hivi ni kwanini da Chemi unapenda kutaja neno MWEUSI kumtambulisha mtu mweusi??!! Gavana mweusi,mweusi wa kwanza kumiliki aiport,mwanafunzi mweusi achomwa kisu,mweusi aonewa na police,mweusi akamatwa na madawa,raisi mweusi,wazungu wamechoka na black na wanahofu Obama(cuz he's black) atashinda tena....

Mweusi,mweupe,mweusi,mweupe yanini hiyo? We leta habari tu na achana na hiyo kitu mweusi,inaonesha ni ajabu kwa mweusi kufanya jambo liwe ni zuri au baya,au we hujikubali/kukubali kuwa unaweza/mweusi anaweza??????

Potz
Mashariki ya mbali.