Thursday, November 04, 2010

Makochi ya Vitenge




Mwaka 1990 kuna dada fulani (Marehemu) huko Manzese aliyetengeneza maforonya na mashuka ya vitenge. Watu walimcheka.

Leo wazungu wanatengeneza makochi ambayo yamefunikwa (upholstery) na vitenge. Tena wanaziuza bei mbaya. Hebu cheki hizo kochi pichani, moja dola $1,700! Hizo ottoman za kuwekea miguu dola $200! Acheni kudharua vitenge na khanga zetu. Tengenezeni maseti ya mashuka na maforonya mpate kibunda....ohhooooo! Exported from Tanzania!
Mnaweza kuona bidhaa zaidi kwa kubfoya hapa: ANTHROPOLGIE.COM

4 comments:

emu-three said...

Hii bab kubwa, manake tunajitangaza, mfano kwenye hayo makochi wanaweka misemo ya kiswahili, mfano
`hata ukinikalia hutanikumbuka...'

Anonymous said...

Changamkeni wabongo. Kumbe miaka yote hii tungekuwa tuntajrika kwa kuexporti makochi ya vitenge!

Anonymous said...

Uchumi tunao tumeukalia tu, utashangaa Wakenya watakavyochangamkia hiyo biashara. Siku moja nimeingia duka la HMS UK mwaka 2007 nikakuta gauni ya summer imeshonwa kwa kanga nzito ya urafiki, lakini limetoka Kenya!

Kazi kubwa tunayoijua ni kulalamika tuu!

Anonymous said...

Sisi tunadharau wenzetu wanaona njia ya kutengeneza mapesa!