Friday, February 04, 2011

Mgomo UDSM

Wanafunzi wa UDSM wamegoma tena! Hivi wana soma saa ngapi? Kazi kujadili watagoma lini. Kwa kweli sifurahii migomo. Kwa wanaokumbuka Mwalimu alikuwa anawadhibiti vikali viongozi wa migomo. Wengine walikuwa wapelekwa na mbu sehemu fulani pale Oyster Bay na kuminywa gololi zao! Ubaya wengine ni watoto wa wakulima, wazazi wao wamejipiga wapate visenti ili watoto wao wawe na maisha bora kuliko wao.
Hatimaye, mtoto anafukuzwa chuo hata kazi ya maana hawwezi kupata maana kawa black sheep, yule mtoto wa mkubwa aliyeshiriki anapelekwa kusoma kwingine au nje ya nchi. Hebu mfikirie Kwanza jamani! Hakuna baraza la viongozi wa wanafunzi? Fanyeni Dialogue. Hakuna faida kwa wote Chuo kikifungwa. Nilishapambana na hiyo teargas na mafarasi wa FFU Dar si mchezo! Kuna hatari ya mtu kupoteza maisha yake.


Kuna mdau amaeleta habari hizi:

Kwa habari zilizonifikia hivi punde, wanafunzi wa UDSM wametawanywa kwa mabomu ya machozi maeneo ya mlimani city na ardhi university wakiandamana kwenda ikulu kupinga posho ya tsh 5000 na kudai tsh 10000.

Hivi mabovu ya machozi ndio njia kuu ya kuzuia maandamano?
Serikali haijui wajibu wake mpaka ikumbushwe kwa maandamano? Mbona wabunge wanajiongezea posho zao bila migomo?

Hapo awali serikali ilahidi kuwa kila baada ya miaka mitano posho itakuwa ikiongezwa kwa ajili ya kujikimu chuoni?

Sasa karibu kila chuo kinagoma, kila siku taarifa za habari lazima ziongelee kuhusu migomo elimu ya juu, JK halioni hilo? Kiongozi imara lazima angeshituka kuhusu hali hii inayoendelea nchini. Ya Tunisi na Misri yasifumbiwe macho, yalianza kama hivi tuonavyo hapa kwetu.

Nawasilisha!

******************************

Kwa habari zaidi na picha mtembelee Kaka Michuzi

http://issamichuzi.blogspot.com/2011/02/wanafunzi-chuo-kikuu-cha-dar-es-salaam.html#comments

13 comments:

Anonymous said...

TUNASHABIKIA TU MIGOMO NA VURUGU? LEO HII UKIMWAMBIA MZAZI ALIYEUZA KUKU WAKE UKAPATA NAURI YA KUJA MJINI KUSOMA ETI HUTAKI POSHO YA 5000, UMEANZISHA VURUGU UKAVUNJWA MGUU JE ATAKUELEWA WAKATI YEYE NA MAMAYAKO PAMOJA NA WADOGO ZAKO NA WATOTO WA DADA ZAKO 5000 NDIO PATO LAO LA MWEZI NA WANAISHI.

TUTAFAKARI....

Anonymous said...

Nashangaa sana watu wanahamaki wanafunzi kudai pesa za kujikimu maisha. Kwanza ni mkopo ambao watakuja kuulipa. Serikali inasema hii nchi masikini, hawana bajeti ya kuwalipa wanafunzi. Je, wametoa wapi 100 billion shillings za kuwalipa DOWANS kwa mkataba wa kifisadi? Hivi kwa gharama za maisha ya leo, bajeti ya shilingi elfu 5 hapa Dar utaitumiaje kwa siku? Hesabu bei ya chai, lunch na chakula cha jioni. Hapo bado maji ya kuoga, kufulia etc lazima wanunue kwa ndoo. Let's be realistic, shilingi elfu 5 kwa siku is peanuts kwa maisha ya hapa jijini. Makusanyo ya kodi za serikali kwa mwezi ni karibu 500 billion shillings. Zinakwenda wapi hizi pesa kama si kununua mashangingi, posho na safari za nje za viongozi kila siku?

Mimi naona kuwalipa wanafunzi elfu 10 kwa siku ni kitu kidogo sana, hakiwezi kuwashinda serikali hata kidogo. In fact, nina amini kwa dhati kabisa kuwa elimu BURE inawezekana. Uganda na wengine wameweza, kwa nini sisi tushindwe? Tanzania inaongoza kwa kupata misaada ya donors kwa bara la Afrika. Tuna dhahabu, tanzanite, almasi, bandari, utalii, ardhi na rasilimali tele. Pesa hizi zinakwenda wapi? Kila siku vigogo serikali wanasafiri kwenda ulaya first class, wananunua mashangingi mapya kila mwaka, posho kila mara. Ripoti ya CAG imesema kwa mwaka serikali inatumia I think karibu 20 billion shillings kwa chai, biskuti na maandazi kwenye ofisi. Kuna wizi mkubwa na matumizi hovyo ya pesa zetu sisi walipa kodi ndiyo maana kima cha chini cha mshahara kiko chini, wanafunzi wananyimwa pesa za kujikimu. Lazima serikali ibane matumizi, iache anasa na izuie wizi za pesa za umma. Badala ya Land Cruiser VX zenye 4,500cc na kuuzwa 300m/-, kwa nini viongozi waserikali wasitembelee RAV4 zenye 1,800cc na kuuzwa 30-50m/-? Jirani zetu Kenya mawaziri wanatembelea Volkswagen ingawa mishahara yao iko juu kulinganisha na Tanzania.

Ninaunga mkono kwa asilimia 100 madai halali ya wanafunzi kutaka pesa za kujikimu ziongezwe ingawa maandamano yanaweza kuwa si njia sahihi ya kuwasilisha madai hayo.

Anonymous said...

Nami kwa niaba ya TYVA niweke msisitizo katika hili, yaliyotokea Misri, Tunisia na yale yanayoendelea Yemen huenda yakaikumba na Tanzania kama hatua za makusudi hazitachukuliwa kutatua migogoro katika elimu ya juu. Natoa rai kwa Serikali ya Tanzania, haiba budi kuongeza posho kama walivyoahidi hapo awali. Hali ya kutumia nguvu hasa ya mobomu ya machozi huenda ikasababisha maafa zaidi ya kile ambacho wanafunzi hawa wanachokidai endapo wasiposikilizwa.

Aidha hali hii inaweza kutumika kuondoa uvumilivu na kuchochea hasira za wananchi wengi kujiingiza katika migogoro isiyokuwa na sababu endapo madai ya wanafunzi wote wa elimu y a juu yatapuuzwa.

Ninaamini kabisa serikali inaouwezo wa kuongeza posho za wanafunzi katika elimu ya juu. Wapo viongozi wenye dhamana katika hili, TYVA inawakumbusha viongozi wa serikali kuhakikisha wanafunzi hawa hawabughudhiwi kwa kuwa ndio tumaini la Taifa letu na usomi wao hutoa dira ya mustakabari wa Taifa hasa kuchochea uadilifu na ueledi katika fani mbalimbali.

Katika hili sisi kama asasi ya vijana ya Kirai hatutanyamaza kimya bali tutatea vijana wa Taifa hili. Mengi tumeyasema kupitia Ajenda ya Vijana 2010. Hali hii ni dalili mbaya, hatupo tayari kuiona nchi inaingia katika machafuko yasiyokuwa na maana,wala tija mahali ambapo suluhu inaweza kupatikana bila kutumia nguvu. Tunawaomba viongozi wa serikali wanaohusika na posho hizo kuwasikiliza wanafunzi na kuwajibika katika hili.

Anonymous said...

migomo na kuandamana sio njia nzuri ya kumaliza matatizo na kamwe siombei nchi yetu ifikie au hata ikaribie egypt peoples voice, ila naamini mlolongo wote wa migomo iliyotokea hivi karibuni almost all university ,najua hata walimu waligoma udom na madai ni ya wazi, tufike maaali serikali iingalie watendaji wake ,ndo chanzo ya yote sidhani kama hao vijana wameaka tu jana na kudai 5000 haitoshi watakuwa walishawakilisha their analysis ila wanaona wamekuwa ignored ndo sababu wamechukua hiyo decision ,tunaomba vijana wasikilizwe waweze saidia hilo taifa huko mbeleni

Anonymous said...

imi sijui kama kweli tunaona seriousness ya what is happening around LCDs (least devloped countries)now, and how serious sisi watanzania tunaoona mbali tunalichukulia hali/wimbi hili.

The waves which have started tunisia na misri,etc is inevitably linakuja tanzania, why? sababu hali ni mbaya na watu wanalia sana, uchafu wa kila anina uko kila mahali, nchi inaliwa mbele ya macho ya watu bila aibu kabisa.

Zaidi sana the government, leaders, na machineries zinazosimamia social justice, equalities, freedom, maisha bora na fairness in the societies zimeshindwa kuwa effective; hence inequalities imetokea, na corrupt ones have becomes filthily rich, while the vulnerable ones have been forced into unbearable poverty. You don’t need to be told about this, do you!

As Tanzanians were not exempted on the wave of change, which is catching up now. The only way tunaweza fanya ni kujiandaa vizuri na kuchukua pre-emptive measures kuhakikisha tunatatua matatizo yanayoweza kua chanzo cha mpasuko mkubwa katika jamii.na watu wanapata haki yao.

Yaani kama tutakaa kimya na tunaona kabisa tatizo hili lazima litatokea hata hapa kwetu Tanzania, we are not doing the people a favour, we are letting them down.

Na wimbi hili kama tusipojiandaa likija nataka nikuambnie hata wewe unayepuuza, utakimbia kimbia tuu, you would not have the comfort you are having now.

Tusiwe watu tusioona mbali lazima tuwe na mikakati ya kuisaidia jamii, na ku-engage serekali ili, changes for the better zije. Kweli tusiofanya hili, I can confirm to you, it is just a matter of time kabla ya watu kuanza kuchinjana, watu wanauchungu sana sana kwa jinsi hali ilivyo, hajapatikana tuu mtu wa kuwasha kibiriti; na moto wake itakuwa neema sana kuzimika, na hata ukizimika kutakuwa tiyari na doa kubwa sana kwenye jamii yetu, we will never be the same any more.

Pls pls pls tusisubiri mpaka hilo litokee because that opportunity to mend our society and country would be gone; lets do something now, we still have time as long as this hali ya amani kidogo ipo.

This should be an immediately thing, it has to be within six months, sithani kama watanzania watakuwa na subira much more tena.

Hutuwezi kufunbia macho haya yanayotokea duniani, Tanzania tunabahati kwa sababu tunayaona, lest not blame ourselves that we had a chance ya kufanya kitu and we didn’t.

ACTION

For many of us, together we can collect our concerns for change and compile them onto an action plan which we then send it to the government i.e raisi, waziri mkuu, mawaziri na wabunge. Media local & international, important embassies etc. We have to be strong but dignified and direct to what the people want.

I am ready to be one of the team to collect mawazo haya haraka, na hata kuwa mmoja wa watakao kwenda kupelea jumbe hizi. Na hata kama hakuna mtu tuki-compaile naweza kuorganise kuanzia vyombo vya habari mpaka kwa rais and government yake yote, embassies na international media.

Jamani huu ni muda nyeti sana, sio wamchezo kabisa, we have this last chance to correct the course of destiny of our country, llets do it. Watanzania wanangojea kuona who will take lead for better, na kama hakuna, I can assure you we are doomed and there will be no one to blame except ourselves.

Anonymous said...

Hivi kulikuwa na ulazima gani kwa polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi kuzuia maandamano hayo? Polisi wa Tanzania bado hawajui kitu kuhusu ‘crowd control’. Wanachojua wao ni kutumia maguvu na ubabe usiokuwa wa lazima. Nilikuwa karibu na Mlimani wanafunzi walipoanza kuandamana na nilihesabu askari polisi si chini ya 20 wakiwa na bunduki aina ya AK47 na wengine wengi wakiwa na mabomu ya machozi. Serikali inapaswa kuelewa kuwa hii inaipa Tanzania jina baya mbele ya jumuiya ya kimataifa. Nilitarajia kuwa tutakuwa tumejifunza baada ya matukio ya Arusha lakini inaelekea bado polisi Tanzania wanatumika kama chombo cha kukandamiza raia na kuwanyima haki zao za msingi.

Anonymous said...

Nahisi kuna watu wako katika mpango kabambe wa kuitafuna nchi hii hakika tunako elekea sio pazuri leo nchi ya tanzania yenye utajiri wa kutosha na iliyo pata uhuru miaka mingi iliyo pita wagonjwa wanakosa dawa hospitali lakini waziri ajengewe nyumba mbunge alipwe posho kubwa zaidi sijui kama tutafika jamani yangu macho.

Anonymous said...

Hata ukiwapa 20,000/- watasema haitoshi wanataka posho sawa na mbunge! Wenzao wanaoende kusoma abroad ila scholarship mbona wanafanya kazi kubeba boxi na kusafisha barabara ili wapate visenti! Wanabahatikuwa wanapewa hiyo 5000/- kwa siku!

mchinakamanda said...

hallowww!!!!!!!!!!!!its good.have you ever heard the river flow to the hills or mountain is that what you want to make. ma friends as you fight the truth make sure you have reasonable reasons to make you win. congratulation for that, mnajifunza jeshi chuoni mko juu.

mchinakamanda said...

have you ever seen the river flows to the hills? make time and improve you are strategies, make reasonable reasons to fight with the wall unless you will die with nothing. poleni sana pia hongereni kwa kupata mafunzo ya jeshi chuoni kwenu.

Anonymous said...

MIminafikiri wakati umefika kwa serikali ya Tanzania kuacha ubabe.Maisha Dar ni magumu wapeni hao watoto hiyo 10000 kwanza mimi pia naona haitoshi kwani kama ujuavyo kwetu hakuna maji wala umeme nafikiri pia wata hitaji battery za tarch kwaajili ya kusomea ambayo ni pesa,maji ya kuoga na kufulia n.k. Mimibinafsi ni mzazi ninayeishi maisha ya kawaida lakini kwa siku mtoto wangu mmoja kkwenda shule na kurudi inanigharimu 5000 kwa mtoto kwa siku tena mtoto wa Secondary itakuwa hao watu wazima tena wana chuo. Serikali iache ubinafsi kwani Wanafunzi wengine hapo chuoni wanalipiwa na wazazi wao wala hawachukui mkopo kwa hiyo msijifanye mna mzigo mkubwa.Halafu mbona Serikali ya awamu ya 1,2 Wabunge walikuwa hawapewi ashangingi ya thamani Viongozi wa Tanzania ni wa binafai sana mbonahatujasikia bunge la uingereza wamegawana mapesa kinyume chake wamejupunguzia mshahara.Halafu nyinyi polisi kazi yenu ni kulinda amani siyo ubabe Wenzenu Uingereza wanafunzi walipo andamana Polisi walikuja kulinda amani kuangalia kama fujo haifanyiki ile iwe rahisi kwao kuwa kamata watu watakao leta fujo na nyie mnaweza kufanya hivyo mnafanya makusudi mnajifanya hamuelewi mnanelewa sana.

Anonymous said...

MIminafikiri wakati umefika kwa serikali ya Tanzania kuacha ubabe.Maisha Dar ni magumu wapeni hao watoto hiyo 10000 kwanza mimi pia naona haitoshi kwani kama ujuavyo kwetu hakuna maji wala umeme nafikiri pia wata hitaji battery za tarch kwaajili ya kusomea ambayo ni pesa,maji ya kuoga na kufulia n.k. Mimibinafsi ni mzazi ninayeishi maisha ya kawaida lakini kwa siku mtoto wangu mmoja kkwenda shule na kurudi inanigharimu 5000 kwa mtoto kwa siku tena mtoto wa Secondary itakuwa hao watu wazima tena wana chuo. Serikali iache ubinafsi kwani Wanafunzi wengine hapo chuoni wanalipiwa na wazazi wao wala hawachukui mkopo kwa hiyo msijifanye mna mzigo mkubwa.Halafu mbona Serikali ya awamu ya 1,2 Wabunge walikuwa hawapewi ashangingi ya thamani Viongozi wa Tanzania ni wa binafai sana mbonahatujasikia bunge la uingereza wamegawana mapesa kinyume chake wamejupunguzia mshahara.Halafu nyinyi polisi kazi yenu ni kulinda amani siyo ubabe Wenzenu Uingereza wanafunzi walipo andamana Polisi walikuja kulinda amani kuangalia kama fujo haifanyiki ile iwe rahisi kwao kuwa kamata watu watakao leta fujo na nyie mnaweza kufanya hivyo mnafanya makusudi mnajifanya hamuelewi mnanelewa sana.

Anonymous said...

Acheni mambo ya magomo. Someni vitabu!