Blogs in Kiswahili, the main African language of EAST AFRICA.
Friday, February 18, 2011
Wanafunzi wa Mwenge University Wafukuzwa Chuo!
Wiki chache zilizopita wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mwenge huko Moshi walishiriki katika mgomo. Sasa wamepewa barua wajieleleza la sivyo watafukuzwa kwa kuvunja sheria za Chuo.
Kabla ya hawa wanafunzi kupata msaada kutoka kwa wanasheria, ni vyema wakajijua kama wanaumoja ulioimara na kusimama kutetea kile kilichotokea! Kwa uzoefu wangu katika mambo haya ya migomo chuoni, ni kwamba vyuo vina student by-law ambazo ni sheria ndogondogo zinazowahusu wanafunzi. Kawaida migomo huwa haiibuki hivihivi tu, hutokea pale makubaliano kati ya wanafunzi na uongozi husika wanaposhindwa kufikia makubaliano!
Lakini hawa wanafunzi watuambie wazi kama mgomo huu ulipewa baraka na Serikali ya wanafunzi, kama ulipewa baraka na wanafunzi, basi hata wanafunzi wenyewe wanaweza kuwarudisha wenzao kwa umoja wao! Je, kwanini wanafunzi wameamua kurudi madarasani kama madai yao hayajatimizwa? au waligoma tu ilimradi? Let them (students) be openly on that ili wapate msaada kutoka kwa wadau wa sheria!
I worked for Tanzania's Daily News for 11 years leaving as a Senior Reporter. I love acting, films, short story writing and cooking. I blog in English and Swahili. I am a member of the Screen Actors Guild (SAG) and AFTRA.
You can contact me at chemiche3@yahoo.com.
3 comments:
poleni wanafunzi,
www.pamojasms.com
Tumieni www.pamojasms.com kupashana habari dunia nzima

Post a Comment