Thursday, February 24, 2011

Wanaomba Msaada wa Gharama za Matibabu - Christina Masimba

Christina Alivyo Sasa
Christina Kabla ya Kuugua

Sisi wazazi wa Christina Nasson Masimba, Bw na Bi. Mwinjilist Masimba, tuna ujasiri mbele za MUNGU kukushirikisha/kuwashirikisha hitaji la msaada ili kukidhi gharama za matibabu ya mtoto wetu mpendwa.

Christina ni binti mwenye umri wa miaka 6, akiwa ni mtoto wetu wa mwisho kati ya watatu ambao Bwana ametubarikia. Ni mtoto mchangamfu sana, na anayempenda Mungu wake.

Tangu tarehe 9 Septemba 2009, binti yetu huyo aliugua malaria ambayo inasadikika kupanda kichwani na kumpa shida kubwa katika ubongo wake. Na hiyo imekuwa ndiyo chanzo cha kuugua kwake mpaka sasa. Kufuatia kuumwa huko, Christana alilazwa na kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera (Bukoba Government Hospital) zaidi ya mara tatu. Baadaye Januari 2010, alilazwa pia katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma (Dodoma General Hospital) wakati tukiwa likizo, na kisha akalazwa tena Bukoba Government Hospital, tuliporudi kazini Bukoba baada ya likizo.

Christina katika hali yake ya sasa, akiwa hana furaha tena yakutosha, kutokana na kuugua kwa muda mrefu! Aidha, amelazimika kusimama Shule kwa ajili ya kutibiwa.

Ukweli Christina na sisi wazazi wake tunahitaji sana watu wenye mapenzi mema,(WASAMARIA LUKA 10:25-27) ili aweze kupata huduma ya matibabu ya kumfaa, Pia uone Christina akiwa tayari kwenda shule asubuhi, kabl;a ya kuumwa, alipenda sana kusoma nakufurahia Shule.

Kati ya Aprili na Agosti, 2010 ugonjwa ulizidi kuongezeka na kuonyesha dalili za kupooza baadhi ya viungo vyake upande wa mkono wake wa kuume. Tulijitahidi kwa kila hali kwa maombi na tiba lakini bado hali yake ilizidi kuwa mbaya kadri siku zilivyopita.

Mnamo mwezi Novemba 2010, madaktari wa Bukoba Government Hospital walitutaka twende katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Baada ya vipimo na matibabu kwa zaidi ya mwezi mmoja bila mafanikio, madaktari wa Bugando Hospital walitupa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (Muhimbili National Hospital - MNH).

Muhimbili walitupokea tarehe 18 Novemba, 2010 na kumtibu mpaka 21 Desemba, 2010. Walijitahidi kupima kila kipimo walichofikiria na, pale walipohitaji kipimo kilichokuwa hakifanyiki hospitalini hapo, walituelekeza kukipata katika hospitali nyingine nasi tulitekeleza maelekezo yao. Kwa ujumla, vilifanywa vipimo 14 kama vilivyoainishwa hapa chini. Ndipo shida iliyompata alipougua kwa mara ya kwanza ikagundulika.

Vipimo alivyopimwa ni:

CT – Scan (Kichwa).
EEG – (kipimo cha utendaji kazi wa ubongo).
FBP – (kipimo cha damu) Normal.
Sickling test –(Negative).
HB electrophoresis AA.
Echocardiogram (ECG) – normal.
CXR (normal).
Abdominal ultrasound.
LFT (normal).
RFT (normal).
TCD NCA (Middle Cerebral Artery) - both normal.
PT, PTT and INR (all normal).
HIV screening (Negative).
EEG – (consistent with focal seizure disorder).

Hata hivyo, vipimo hivyo na matibabu aliyopatiwa havikuleta ufumbuzi au unafuu katika hali ya Christina, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya. Mnamo tarehe 20 Desemba, 2010 MNH walituruhusu (discharge) ili turejee nyumbani kwa kupitia Bugando Referal Hospital kwa kujigharamia, na kututaka turudi hospitalini hapo baada ya muda wa miezi miwili (2) ili waangalie hali yake.

Kwa kuzingatia gharama kubwa za usafiri, na ukweli kuwa hali ya mtoto ilikuwa inazidi kuwa mbaya, hatukuweza kwenda Bugando wala Bukoba. Badala yake, tulipata familia moja hapa Dar es Salaam iliyokubali kutupokea wakati tunaendelea kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya afya ya binti yetu.

Ndipo tulipochukua hatua nyingine ya imani, na kuaza kutafuta jinsi ya kupata matibabu mahali popote. Tuliendelea na huduma za maombezi na matibabu madogo madogo hapa Dar es Salaam na Dodoma. Wakati huo huo, tulianza mawasiliano na hospitali za India ili kuona uwezekano wa kupata uchunguzi wa ziada na matibabu nchini huko.

Hivi sasa nafasi ya matibabu imepatikana katika Hospitali ya Indraprastha Appolo, New Delhi, INDIA.

Mchanganuo wa gharama za safari na matibabu ya Christina katika hospitali hiyo ni kama ifuatavyo:


HITAJI *****BEI**** IDADI ****JUMLA

1 Pasi za Kusafiria ****75,000 ****3 ****225,000
2 Visa**** 150,000 ****3 ****450,000
3 Tiketi ****1,488,000 ****3 ****4,464,000
4 Uchunguzi (siku 7 za mwanzo)**** 8,680,000**** 1 ****8,680,000
5 Makazi nje ya Hospitali (siku ya 8 – 14)***** 1,550,000 ****1**** 1,550,000
6 Matibabu na Makazi (wiki 7 zinazofuata)**** 12,400,000**** 1**** 12,400,000
7 Madeni ya matibabu tangu Disemba, 2010 ****800,000 ****1**** 800,000

JUMLA ZINAZOHITAJIKA

28,569,000/- (T.Shs)

Kiasi hiki ni kikubwa sana kwa uwezo wetu, na tunaomba mchango wako wa kutuwezesha kukidhi gharama hizi. Kwa kadri Mungu atakavyokugusa rohoni, tutashukuru kupokea mchango wako kupitia katika yoyote kati ya akaunti zifuatazo:-

Jina la Akaunti
Benki
Namba ya Akaunti

Nasson Richard Masimba
CRDB
011 205 709 1300

Nasson Richard Masimba
NBC
02 720 108 8567

Nasson Richard Masimba
NMB
318 160 5859

Nasson Richard Masimba
MPESA
076 777 8583

Ahsante sana kwa hatua yako. Tunaamini kuwa, tukinia pamoja, tutapata ushindi na ushuhuda kwa MUNGU wetu.

Bw Nasson R. Masimba na Bi Mariam N. Masimba

Wazazi wa Christina

0784778583, 0715778583, 0767 778583; 0658778583, 0756930810

masimbar2005@yahoo.com
= = = = =

Unaweza pia kuwasiliana nasi au kupata maelezo zaidi kupitia namba zifuatazo, na MUNGU akubariki sana.

4 comments:

Mbele said...

Shukrani kwa kutuletea taarifa hizi. Nami ni muumini wa dini. Naamini kuwa, kwa kuruhusu hali hii itokee kama ilivyoelezwa, Mungu ametupa mtihani wanadamu, kuona kama tuna mshikamano au la. Zaidi ya hapo, mimi kama mwalimu nimeguswa na ari ya mtoto huyu ya kupenda shule. Shukrani kwa taarifa za sehemu za kupeleka michango.

Anonymous said...

Poleni sana wazazi, na pole nyingi kwa binti kwa maumivu na kukosa shule. Ila mwamweza kupunguza gharama hizi kwa mtoto kwenda na mzazi mmoja na sio wawili.
Kutoa ni moyo si utajiri, twaomba mpokee hata kidogo tutakacho hamisha kwa NMB mobile

Anonymous said...

Maskini yaani kweli Tanzania wameshindwa kumdiagnose mtoto anaumwa nini? Je, mmeenda psychiatric?

Anonymous said...

Poleni sana kwa kuuguliwa na mtoto, ili kupunguza gharama, aende mzazi mmoja, na pia huyo mzazi atakapokuwa India aishi kwenye hosteli na si hotelini, matibabu India sio gahram kubwa kiasi hicho hasa kwa upande wa vipimo, ni vema mcheki upya chanzo chenu cha habari na jaribu kuuliza kwa wale waliotibiwa india walifanyaje ili kupunguza gharama!