Monday, March 14, 2011

Aibu Huko Uwanja wa Ndege wa Iringa

Hii ni gari pekee linalotumika na kikosi cha zimamoto katika uwanja wa ndege wa Nduli mkoani Iringa. (picha kwa hisani ya Mdau Francis Godwin)
Wadau, hii picha aliiposti kaka Michuzi mwezi uliyopita. Bado huo uwanja hawajaongezewa vifaa. Je, wabunge wa mkoa wa Iringa wataongelea swala huu katika Bunge ijayo? Mimi natoka mkoa wa Iringa na kwa kweli naona aibu sana. Hiyo pick-up inaweza kubeba maji kiasi gani? Je, inakaa uwanjani au inatumika kufanya shghuli zingine mfano kupeleka watoto shule, mama sokoni, kimada gesti..... Huu ni swala nzito sana. Ina maana ndege ikianguka huko ndo basi tena.

3 comments:

Anonymous said...

Wabunge wananunuliwa mashingingi mapya, airport pickup second hand! KHAA!

Anonymous said...

Madumu mawili! yaani gari lina jumla ya lita 40 za maji!

Anonymous said...

Hatari!