Monday, August 27, 2012

Polisi Waua Morogoro Leo!

Marehemu Ally Zona,  alikuwa ni muuza magazeti. Alipigwa risasi kichwani akiwa ameshika magaztei yake!  Hiyo jieraha inaonyesha kuwa marehemu alikuwa anakimbia kutoka kwa polisi. Alipigwa kwa nyuma.


Hapo awali ilielezwa kuwa wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisitiza kufanya maandamano leo kisha mkutano mkubwa wa hadhara, kuliibuka mvutano baina yake na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kufuatia Kamanda wake, Faustine Shilogile kupiga marufuku mandamano hayo.

Kamanda Shilogile alieleza sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa ni udogo wa barabara za Morogoro na kwamba leo ni siku ya kazi hivyo yanawezesha kusababisha usumbufu kwa wakazi wa mji huo.

Wakati Shilogile akieleza kuzuia maandamano yanayotarajiwa kuanza saa 5 asubuhi, Mkuu wa Operesheni Sangara, Benson Kigaila, alisisitiza kuwa watafanya maandamano kwa kuwa waliskubaliana na Kamanda Shilogile kabla ya kuwageuka.

Kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe la 27 August 2012, ilielezwa kuwa Kamanda Shilogile alidai kuruhusu baiskeli na watu kutumia barabara kwa sababu ya mikutano ya Chadema itakuwa ni kuwanyima haki wananchi wengine, na hivyo wataruhusu watu wasiozidi 50 kupita kwa wakati mmoja pasipo kuwa na ishara ya kuonyesha kama wanaelekea katika maandamano.

Pichani ni kijana aliyeelezwa kupigwa risasi kichwani katika tafrani hizo na baadae kupoteza maisha Ametambulishwa kwa jina la Ally Zona, ambae alikuwa ansoma magazeti katika stendi ya Msamvu. Tukio hili lilitokea mapema leo asubuhi kuelekea saa sita mchana wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi hao wa chadema. Mtoa taarifa anasema Polisi wanadaiwa kutumia risasi za moto pamoja na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamani hao.

Watu wengine waliojeruhiwa katika tafrani hiyo wameelezwa kuwa ni mwenesha baiskeli Hashim Seif ambae amejeruhiwa kwa risasi mguuni akiwa napita na baiskeli yake na kijana mwingine aliielezwa kuwa ni muuza matunda Frank Valimba ambae amejeruhiwa na risasi tumboni.


KWA HABARI NA PICHA ZAIDI TEMBELEA KIBONGO BONGO BLOG:

********************************
TAMKO KUTOKA TANZANIA JOURNALIST ALLIANCE (TAJOA)


Jumuia ya Waandishi wa Habari Tanzania (Tajoa) inalaani kwa nguvu zote mauaji ya makusudi yaliyofanywa na Jeshi la Polisi leo mjini Morogro. Inashangaza Tanzania sasa inataka kugeuka taifa la polisi wauaji. NI vyema busara, ujuzi na mbinu stahiki zikatumika badala ya kuendelea kuua raia hata wasiokuwa na hatia.

Hebu ona huyu masikini alivyouawa kwa kupigwa risasi kwenye paji lake la uso na kumsab
abishia kifo cha papo hapo. Inaelezwa alikuwa muuza magazeti aliyekuwa kibandani kwake. Sasa tusubiri taaria ya Polisi ambayo huenda ikasema alikuwa amebeba silaha.

Tanzania, tusikubali kuwa taifa la polisi wauaji.

Marafiki wa Tajoa, nini sasa kifanyike kukomesha hali hii ambayo inaonekana kuota mizizi? Toa maoni yako hapa ili nasi tuyapeleke kwa Jeshi la Polisi

— 
Wafuasi wa Chadema wakiwa na maandamao hayo mjini Morogoro


Moshi wa mabomu yaliolipuliwa kutawanya maandamano ya Chadema leo mjini Morogoro

Akina Mama wakikimbia mabomu ya machozi

5 comments:

Anonymous said...

Ni kweli. Polisi wamevuruga maandamano yaliyokuwa yafanyike kwenda eneo la mkutano, Uwanja wa Ndege, hapa Morogoro Mjini. Wamedhalilisha viongozi waliowakamata na sasa wameanza kuomba samahani, yaishe.

Kamanda wa Polisi Morogoro, Shilogile (mnaojua alihamishwa Dar es Salaam kuja hapa...) amevunja makubaliano yaliyofanyika mara mbili ya kuruhusu maandamano. Tunajua wapo wanasiasa hapa Morogoro ambao hawataki meseji ifike leo kwa wakazi wa Morogoro Mjini.

Inajulikana namna ambavyo CCM wamekuwa shaken big time na operesheni iliyokuwa na mafanikio huko vijijini, itawaumiza zaidi ikifanikiwa hapa mjini. Kwa hiyo lengo hapa si kuvuruga tu maandamano, bali ni kuvuruga mkutano, ili hatimaye watu waogope kuja mkutanoni, ujumbe usifike. Hawatafanikiwa kwa hilo, maana wananchi sasa wanazidi kujikusanya, maeneo kama ya Masika, kwenda eneo la mikutano, kwa maandamano.

Polisi wanachafua mji sasa, polisi wanawapitisha wana-Morogoro kwenye tanuru ambalo watu wa Mwanza, Mbeya, Arusha, Moshi, Musoma, Tarime, Ruaha na kwingineko kwingi, walipita/kupitishwa ili kuwa hapo walipo wakiwa na imani isiyoyumba katika mapambano haya ya kudai na kuwaandaa Watanzania kwa mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala. Chuma hakiwezi kuwa chuma mpaka kipite kwenye tanuru, lakini why doing it unnecessary?

Anonymous said...

Habari za uhakika ni kua polisi wameua mtu maeneo ya Msamvu bila sababu ya msingi,kisa ni kua walikua tu wanajaribu kuzuia maandamano ya Cdm na kijana huyo aliyekua akiuza magazeti aliwaonyesha alama ya V ndipo walipomlipua! My take: ni wazi jeshi la police chini ya IGP Mwema limeshindwa kuwalinda raia na mali zake,na kuwachukulia hatua wezi wakubwa na wahujumu nchini,bali jeshi la polisi limegeuka kua la mauaji kwa raia wasio na hatia kwa jinsi watakavyo! Source: mimi mwenyewe nipo kwenye mkutano hapa Morogoro

Anonymous said...

Hivi viongozi wa nchi hii ni wasomi kweli na ni watu wenye kuona mbali?

Hivi raisi kweli huwa anapima ushauri anaopewa na wasaidizi wake?

Hivi ushauri bora ni kuzuia maandamano kwa risasi au kuacha watu waandamane na kuwapa ulinzi?

Kuua raia kwa risasi,ccm na chadema yupi mwenye hasara hapo kama sio ccm?

Tangu lini risasi za moto zikashinda nguvu ya umma?CCM hamjifunzi kwa yanayotokea nchi za wenzetu?

Raisi Kikwete hutambui kuwa 2015 wana ccm watakulaumu wewe na wala si washauri wako?

Raisi Kikwete hutambui kuwa wanaokuunga mkono leo kesho mambo yakiharibika watakugeuka na utabeba lawama peke yako?

Tafakari waliokuwa wanakushauri juu ya katiba mpya kama mfano mmoja tu na alafu ujiulize kama kweli una washauri wazuri na unaopaswa kuendelea kuwa nao mpaka leo

Raisi Kikwete tafakari sababu zilizokupunguzia kura kutoka aslimia 80 mpaka 60 kama mpake leo hii umezifanyika kazi au ndio zinazidi kuongezeka

Hivi leo hii nani asietambua ukweli kuwa chadema kimelenga kutetea maskini na ccm kimelenga matajiri wachache?

Mwisho mjiulize nchi hii wengi ni matajiri au maskini?

Sintashangaa na ninaomba chadema wachukue nchi hii 2015 alafu muje kuwajibika kwa mauaji haya.

emuthree said...

Yale yale, yalianzia kwa wale waliotungiwa jina na kuitwa `imani kali,ikaja kwa KAFU, wote hawo walionekana ni wahuni! Sasa zamu ya ChADUMA

Anonymous said...

Naililia nchi yangu!