Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mjukuu wao Aziza Ridhiwani (3) katika ghala ya mahindi yaliyovunwa kwenye shamba lao kijijini Msoga, nje kidogo ya mji mdogo wa Chalinze, Mkoa wa Pwani. Rais Kikwete ni mkulima na mfugaji kijijini hapo na ameonesha kufurahishwa sana na mavuno makubwa ya mahindi shambani kwake. Hii katika kutekeleza kwa vitendo sera ya Serikali ya kuendeleza kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya sekta ya kilimo katika Tanzania.
PICHA NA IKULU
1 comment:
Kuna mtani mmoja, alisema yeye ni kabila la wakulima, walikuja huku Dar zamani kulimishwa na watani zao ambao hawajui kulima...nikawaza sana, hivi kweli kuna watu wasiojua kulima na wanajua kulima, kwa sisi wabongo?
Post a Comment