Showing posts with label Bagamoyo. Show all posts
Showing posts with label Bagamoyo. Show all posts

Sunday, February 13, 2022

Tanzia - Professor Samahani Kejeri

Mwanahistoria na Mtembeza Watalii maarufu, "Professor" Samahani Kejeri, amefariki dunia, leo Februari 13, 2022, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alikuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu ya kansa.

Binti yake, Furaha Kejeri amethibitisha  habari hiyo, Mazishi yatafanyika kesho, Jumatatu, Februari 14, 2022 nyumbani kwa marehemu, Magomeni, Bagamoyo. (Siyo Magomeni ya Dar es Salaam)

Prof. Kejeri alipewa jina la "Professor" kutokana na ufahamu wake wa Historia ya Bagamoyo.  Alikuwa anatunza vitabu, "friend books" ambazo zimesainiwa na watu ambao aliwatembeza Bagamoyo.  Mimi mwenyewe nilikutana naye mara la kwanza mwaka 1988, nikiwa mwanafunzi wa Tanzani School of Journalism.  Tulienda Bagamoyo kwenye Field Trip na alitutembeza na kutoonyesha sehemu muhimu za kihistoria ya Bagamoyo ikiwemo "hanging tree" ambako wajerumani walikuwa wananyonga weusi.  

Prof. Kejeri pia aliigiza katika sinema Maangamizi the Ancient One kama Mganga Simba Mbili.  Sinema hiyo ilikuwa ya kwanza kutoka Tanzania kuwa katika mashindano ya Academy Awards (Oscars) Hollywood.

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin



Prof. Samahani Kejeri, Prof. Amandina Lihamba na Msanii Barbara O katika sinema Maangamizi the Ancient One

Prof. Samahani Kejeri Explains History of His Name - YouTube



Sunday, July 10, 2016

MAANGAMIZI: THE ANCIENT ONE - Sinema ya Kwanza ya Tanzania Kwenda Oscars!

   Hii ni sinema ya kwanza kutoka Tanzania kushindana katika Academy Awards (Oscars)!

Thursday, January 01, 2015

Rais Kikwete Asherekea Mwaka Mpya Kijini Msoga, Bagamoyo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge  wa
Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakijumuika na wananchi katika
kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiomba  dua  pamoja na Mashekhe  wa
Bagamoyo na wananchi  wakati wa hafla ya kumuombea dua katika mkesha
wa mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukurani kwa  Mashekhe
wa Bagamoyo na wananchi  kwa kumuandalia  hafla ya kumuombea dua
katika mkesha wa mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa jamii ya
wamasai wanaoishi mkoa wa Pwani. Kiongozi mkuu wa jamii hiyo, Laiboni
Tikwa Moreto (wa pili kushoto), Majaliwa Lihalei na Zuberi Tangono
katika hafla ya  kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze,
Mkoa wa Pwani.

Wednesday, June 25, 2014

Mbunge Shukuru Kawambwa Yuko Canada - Hajafa! Ilikuwa Uzushi

 
Mb. Shukuru Kawambwa

Kutoka Facebook

TAARIFA TOKA BAGAMOYO
Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.

UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.


Wednesday, August 22, 2012

Rais Kikwete Shambani Kwake Msoga



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mjukuu wao Aziza Ridhiwani (3) katika ghala ya mahindi yaliyovunwa kwenye shamba lao kijijini Msoga, nje kidogo ya mji mdogo wa Chalinze, Mkoa wa Pwani. Rais Kikwete ni mkulima na mfugaji kijijini hapo na ameonesha kufurahishwa sana na mavuno makubwa ya mahindi shambani kwake. Hii katika kutekeleza kwa vitendo sera ya Serikali ya kuendeleza kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya sekta ya kilimo katika Tanzania.



PICHA NA IKULU

Wednesday, August 31, 2011

Marian Schools Bagamoyo Fundraising Gala Dinner Invitation Sept. 4, 2011

Uongozi wa Shule za Marian Bagamoyo unawakaribisha wote kwenye Fundraising hii ya Kujenga na kuendeleza Shule hizi.

Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba

Wazazi,wanafunzi wa zamani,wenyeji wa Bagamoyo na wote wale wenye Mapenzi mema mnakaribishwa sana sana tarehe 4th SEPT Diamond Jubilee Hall saa Moja jioni.

Asanteni!

Saturday, January 15, 2011

Clip From Maangamizi the Ancient One



Hii ni clip ktuoka sinema Maangamizi the Ancient One. Ni sinema ya kwanza ambayo Tanzania ilietua katika Academy Awards (Foreign language category). Ingawa haikuchaguliwa kuwa katika sinema tano bora za mwaka huo 2000 ilikuwa hatua kubwa sana kwa Tanzania kujulikana katika dunia ya sinema.

Je, sinema gani kutoka Tanzania itakuwa ya pili kutueliwa? Kwa wasiojua mimi niliigiza kama Nesi Malika katika Maangamizi, ilikuwa sinema yangu ya kwanza. Ilipigwa Bagamoyo mwaka 1994 kabla mji haujajengwa kama ilivyo sasa.

Friday, December 11, 2009

UKIMWI Bagamoyo


Pamoja na kuwa watu 880 wameptikana na virusi vya HIV ni bora wajuwe ili wapate dawa za VVU/ARV kurefusha maisha yao. Na hao 880 waliopatika na virusi ni kati ya 7,985 waliojitokeza. Je, ni asimilia gani katika wasiojitokeza? UKIMWI bado ni tishio tusizembee.

**********************************************
Kutoka ippmedia.com

Watu 880 Bagamoyo wakutwa na Virusi
Na Futuna Seleman
11th December 2009

Jumla ya watu 880 wamegundulika kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kati ya watu 7,985 waliojitokeza kupima virusi hivyo kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu.

Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Bagamoyo, Erasto Mfugale, ametoa taarifa ya utekelezaji ya mapambano ya ugonjwa huo kwa mkoa wa Pwani hivi karibuni.

Akasema idadi hiyo ni sawa na asilimia 11 ambayo chanzo cha taarifa zake kinatoka kwenye Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na pia taarifa za asasi.

Akasema kwa kipindi hicho, jumla ya watu 10,653, wanaume wakiwa 4,127 na wanawake 6,516, walishauriwa kupima kwa hiari na kati yao, watu 7,985 walipimwa VVU, huku miongoni mwao, watu 880 wakikutwa na maambukizi hayo.

Thursday, March 26, 2009

Roho Juu Juu Resolti!

Translation: OUR TOURIST HOTELS

Sign says : Extremely Anxious Resort Welcome!

Hotel Owner: STOP! Keep that cigarette of yours over there, you will cause me severe losses!


Tuesday, March 24, 2009

Mmiliki wa Paradise Resort Aongea


Two Somali owned 5 star hotels located at the historical town of Bagamoyo some 60km from Dara-Salaam the capital city of Tanganyika has turned to ashes on Monday.

“In fact my Hotel was among the leading deluxe hotels in the town of Bagamoyo, and there were 280 workers working in the hotel, and the cause of the fire is yet mysteries, but investigations are underway to detect out the cause of the fire, the fire was very ferocious, and has annihilated money worth 10 million U.S$, but the goodness is that it is registered in the insurance company, the fire swiftly spread to another hotel in the next building owned by a Somali man as well, and it has also completely destroyed it, this hotel of mine was built in the year 1997, everything happens in the will of God the almighty and this simply a building in the world and thanks to God to what has hppend we are Muslims we should come up with strong and unshakable faith to what ever we come across evil or good” said the Abdullahi Noor Gulled the owner of hotel Paradise in Tanganyika speaking to Somaliweyn correspondent in the town of Arusha in Tanganyika.

Since the last effective central government in Somalia collapsed in the year 1991 the Somalis have scattered in the entire of the world and East Africa is one of the places where they have occupied most, in Kenya for instance they have big hotels and shopping malls.

Monday, March 23, 2009

Moto Bagamoyo

Picha kutoka Michuzi Blog

Wadau, baada ya kusoma hii habari kwenye gazeti la Daily News, nikajiuliza kama walikuwa na fire alarms kwenye hizo hoteli. Alarms zinasaidia kujulisha watu kuwa kuna moshi/moto na moto huzimwa mapema. Pia zinasaidia kuokoa maisha! Tena wangeweza kununua alarms za bei chei kabisa na kuweka kwenye kila chumba. Nimeshutuka pale niliposoma kuwa moto ulikuwa una waka na watu waliokuwa kwenye ukumbi kwenye masomo hawakuwa na habari kuwa kuna moto mpaka walifungua dirisha.

****************************************************************

Kutoka Daily News:

Fire guts two beach resorts

JIANG ALIPO, 23rd March 2009

Two popular beach resorts in Bagamoyo, Coast Region, Paradise Holiday Resort and the Ocenic Bay Hotel and Resort were today reduced to ashes in less than fifteen minutes due to a fire that began in the kitchen of the former.

Hundreds of the fast growing seaside township’s residents rushed to witness the mid-morning inferno that is likely to render about 380 workers of the two hotels jobless. Eyewitnesses told the ‘Daily News’ ‘that the fire, which is believed to have been ignited by a gas cooker inside the Paradise Resort kitchen, spread fast to other parts of the hotel due to thatched roofs and the strong ocean winds.

“We had tea break at 10:30a.m. before heading back to the seminar room. After just five minutes of business, the electricity went off. We continued with our session as we did not know what was going on,’’ a hotel guest said. Another seminar participant said it was when they decided to open the windows for air, when they heard people screaming outside.

‘We got outside only to see fire and smoke all over… we had to run for our lives,” said Mr Donath Mlawila, who was at the hotel, instructing a five-day course for Tanzania Roads Agency (TANROADS) officials. Other witnesses said that the second hotel, Oceanic Bay Hotel and Resort, caught fire when most of its staff went to offer a helping hand to the nighbouring Paradise.

The fire crossed to their hotel without their knowledge, only to realise it when the situation was out of hand. The owner and Chairman of the Paradise Holiday Resort, Mr Abdullahi Nur Guled, said that the total investment of the hotel, which was built in 1997, was 10 million US dollars (more than 13bn/-. He, however, said that the hotel was insured.

“We could not save anything… the fire began at around 11:30 am. Within 15 minutes, the whole hotel was on fire. Everything is burnt completely,” said the hotel’s Operations Manager, Mr Shukri Ali. The fire did not cause any fatalities except for the massive loss of property. Several cars parked at the hotel were burnt in varying degrees, including a four-wheel drive Nissan Patrol vehicle that was burnt beyond repair.

Two Toyota Land Cruiser vehicles, one belonging to TANROADS, Mbeya Office, and another to Mr Mlawila, were partly damaged. “When I saw the car partly destroyed, I could not believe my eyes because I failed to take it away as I had left ignition keys in my room which was on fire,” said Mr Mlawila, who said that he had borrowed the car from his friend.

By the time it was gutted by fire, the Paradise Resort had 89 guests in 82 rooms, with 70 of them participating in four meetings, including 21 TANROADS regional managers from all Mainland regions. “This is the low season, when we make between 60,000 US dollars and 80,000 US dollars (about 78m/- and 94m/-) per day, but we used to reach up to 100,000 US dollars (about 130m/-) per day during peak season.

These include accommodation costs, conference costs and all other services,” said Mr Ali. The Paradise is prominent for hosting different government and private meetings. It has 95 rooms and employs 180 people on a permanent basis. “Many people will lose their jobs due to this…not only our employees, but also other people who were supplying us with various goods and services,” said Mr Guled.

The Oceanic Bay Hotel General Manager, Mr Rahul Nayar, said the hotel had employed 200 workers but declined further details on grounds that the owner, who is in Dubai, was the only one to give such details. Bagamoyo District Commissioner Serenge Mrengo said that the district was going to suffer economically from the loss of the two hotels.

“This is a challenge to hotel owners who prefer thatched roofs. The fire this time spread faster because of the thatched roofs,” said Mr Mrengo. Due to lack of fire tenders in the district, the fire in the two hotels had to be extinguished by fire brigades from Dar es Salaam and Kibaha. “This is a problem for us. We have already ordered four such vehicles for our district and paid 400m/- for them. But delivery has not yet been effected,” said the DC.

Moto Bagamoyo katika Picha






Wadau, zimamoto Dar ilienda Bagamoyo kuzima moto. Sasa nauliza kama moto ungetokea Dar wakati huo huo ingekuaje?

Kuona picha zaidi tembelea Kaka Michuzi.

Hoteli Mbili Zaungua Moto Bagamoyo!

Paradise Hotel

Kutoka Michuzi Blog:

paradise resort:imeteketea yooote hata foronya haikuwahi kuokolewa

KATIKA KUFUATILIA KWA KARIBU BALAA LA MOTO HUKO BAGAMOYO, GLOBU YA JAMII INAPASHA KWAMBA HOTEL ZA PARADISE NA OCEANIC BAY (PICHANI) ZIMETEKETEA KABISA NA MOTO.

KWA BAHATI HAKUNA MTU ALIYEJERUHIWA ILA INADAIWA HASARA INAKADIRIWA KUWA YA MAMLILIONI YA SHILINGI.

SHUHUDA WA GLOBU YA JAMII ALIYEKO HUKO AMEHABARISHA SASA HIVIKWA VODA KWAMBA MAJENGO YOTE YA HOTELI YA PARADISE YAMETEKETEA NA KWAMBA HAWAKUWAHI KUOKOA HATA FORONYA AMA GODORO AMA UFAGIO.

HALI KAMA HIYO IMEREKODIWA PIA KATIKA HOTELI YA OCEANIC VIEW, AMBAYO NI JIRANI NA PARADISE, ILA YA LIVINGSTONE CLUB, AMBAYO PIA JI JIRANI KWA UPOANDE KWINGINE, IMENUSURIKA KABISA. INASEMEKANA HII NI KWA SABABU YA UPEPO WA BAHARI KUPEPERUSHA MAKUTI KUELEKEA OCEANIC HOTEL
AMESEMA KWAMBA MOTO HUO, ULIOANZA ASUBUHI, ULIDUMU KWA MUDA WA DAKIKA 15 TU NA HOTELI ZOTE MBILI ZIKAWA ZIMETEKETEA.

YAANI FAYA AMBAO WALIKIMBIA TOKA DAR KWENDA BAGAMOYO KWA KASI ZOTE WAMEKUTA MAJIVU TU. PICHA KIBAO ZAJA MUDA SI MREFU UJAO..

************************************************

Wadau,

Miaka mingi hizi hoteli za kitalii zimeonywa kuhusu ujenzi wa makuti hasa kuezekea makuti. Mnakumbuka hall la Bahari Beach hotel ilivyoungua moto miaka ya 80? Mnakumbuka Hall la Bagamoyo College of Arts ulivyounga na kusababisha hasara kubwa?

Ni kweli makuti yapendeza ni bei rahisi na yanvutia watalii, lakini kuna faida gani kujenga nayo wakati hakuna sprinkler system mle ya kuzima moto kama utatokea? Hebu ona sasa? Hata kulia tunashindwa, tumepigwa butwaa!

Na wageni waliofikia kwenye hizo hoteli wamepata hasara. Huenda kuna wageni kutoka nchi za nje wameptoeza mpaka hatai za kisafiria! Watalipwa fidia?

Nimetembelea hotel websites na bado unaweza kufanya booking ya chumba:

Hotel Websites:


OCEANIC BAY RESORT

PARADISE RESORT

Thursday, January 15, 2009

Kiwanja cha Ndege Bagamoyo


Hivi mlikuwa na habari kuwa huko Bagamoyo kuna kiwanja cha ndege? Naona imesahaulika! Cheki majani yanavyota huko! (picha kutoka Mjengwa blog)

Monday, August 18, 2008

Watumwa


Wadau, ukienda Bagamoyo kutalii lazima utaonyeshwa 'Fort' amabako watumwa walipelekwa kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kabla ya kwenda Arabuni. Huko waliambiwa "bwaga moyo".

Nimeona hi picha ya watumwa na baadhi ya waarabu waliokuwa wanawauza.

Tuesday, July 29, 2008

Bagamoyo Beach



Picha kutoka Maggid Mjengwa blog

Nimeona hii picha hii kwa kaka Mjengwa. Aliipiga Bagamoyo beach hivi karibuni. Kweli TV na sinema zinasababisha mabadiliko katika jamii. Miaka ya nyuma usingeweza kukuta wapenzi wakiongea hivyo hadharani. Au siyo? Lakini ni jambo la kawaida kuonyesha mapenzi hadharani katika video na sinema. Watu wameiga. Kwenye giza ni mambo mengine lakini.

Hivi mnakumbuka enzi za censorship Bongo? Enzi za Mwalimu na kabla ya TV kuingia 1993. Yaani kabla ya kuona sinema, Tanzania film company wanafuta busu, na mambo mengine ya mapenzi. Scene ya mapenzi inakatwa! Kweli walikuwa tuchunga kweli. Hata magezeti na vitabu vya mapenzi yalikuwa marufuku. Mmewahi kusoma kitabu cha After 4:30? Labda ganda ilitolewa na kuwekwa brown paper!

Lakini watu walikuwa wanapendana na kufanya mapenzi!

Wednesday, July 09, 2008

Wanaogombea Miss Vodacom TZ 2008


Hao akina dada wanagombea taji la Miss Vodacom 2008. Wamekwenda kambini leo Bagamoyo.
Kwa habari na picha zaidi mtembelee Kaka Michuzi.

Friday, December 07, 2007

Askari


"Askari eh, vitani yeee mamaaa! "
Mjerumani alipenda sana kupiga posi na askari wao huko Bagamoyo!

Tuesday, November 27, 2007

Mtaa wa Bagamoyo

Hii picha nimeona kwa Michuzi. Ni ya barabara mpya huko Bagamoyo. Sasa nauliza hii ni barabara ya matofali ni ya magari au ya waenda kwa mguu? Naona kuna watu wanatembea kwa mguu na nyuma naona gari inakuja. Sasa hii njia itadumu kweli kama ni ya magari? Hebu nyie wahandisi tuambie.

Sasa wakarabati na nyumba basi papendeze.