CHRISTOPHER MTIKILA BADO HAJAPATIKANA MBADALA WAKO
Na Happiness Katabazi
LEO
Oktoba 4 Mwaka 2016 , naadhimisha Mwaka mmoja kifo cha aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic ( DP) , Mchungaji Christopher Mtikila
tangu alipofariki kwa ajali ya gari Katika Kijiji cha Msolwa ,Jimbo
la Chalinze Mkoani Pwani ,Barabara Kuu ya Morogoro ,saa 11 alfajiri ya
kuamkia Oktoba 4 Mwaka 2015 akitokea Mkoani Njombe Kwenye shughuli za
siasa akirejea Dar Es Salaam.
Binafsi
urafiki wangu na marehemu Mtikila ulianzia alipoanza kusoma makala na
habari zinazohusu habari za mahakamani,siasa nilizokuwa naziandika NA
kuchapishwa Katika magazeti Kadhaa nchini.
Mtikila ,Mkewe Georgia na viongozi wa Chama Chake DP, walinipenda sana na Mtikila na Mkewe walinigeuza Kuwa kama binti Yao.
Muda
wowote nilikuwa nakwenda nyumbani Kwa Mtikila Enzi zile akiishi lla la
Mchikini na hadi alipoamia Katika nyumba Yao Mikocheni nilikuwa
nikifika hapo kwake naenda kupiga story na Mtikila na Mkewe tunacheka na
Mtikila alipachika jina la ' Mpambanaji' .
Nakumbuka
Mtikila yeye alikuwa aogopi mtu Akiamua kuandika Waraka wa
kumkosoa,kiongozi yoyote Yule anaingia ofisini kwake ambapo Mikocheni na
Ilala alipokuwa akiishi alitenga chumba kimoja kama ofisi ya nyumbani
kwake na akawema kompyuta kwaajili ya kufanya kazi zake awapo nyumbani
kwake anaandika waraka mrefu Una maneno makali sana ananiiita
niusambaze nami nilikuwa nafanya hivyo .Nilimpenda sana Mzee wangu
Mtikila ambaye bado pengo lake halijazibwa na uenda itatuchukua Miaka
Mingi kama Taifa kumpata mtu wa aina ya Mtikila .
Nikiupeleka
waraka wa Mtikila kwa Mhariri ,hataki kuchapisha eti Waraka huo Una
matusi hivyo hawezi kuchapa Kwani Gazeti litashitakiwa.Na kweli Mtikila
alikuwa aliandika maneno makali Katika Waraka alizokuwa akiziandika.
Kesho
yake Mtikila akiona hakuna gazeti halijachapisha habari yake ,Mtikila
ananipigia simu na alikuwa akianza kwa kunisalimia hivi ( Saa ya
Ukombozi) minamjibu ni ( Sasa), ananiuliza Hao " wahariri Njaa" kwanini
wamekataa kuchapa Habari yake namweleza Sababu .Mtikila ananiombia
wahariri Hao ni weu wanaho gwa hela na CCM wasitoe Habari zake Kwani
eti yeye Mtikila ni Kiboko ya CCM,CCM ina muogopa sana.
Mtikila
alikuwa ni mwanasiasa wa aina yake kwani licha ya Kuwa mwanasiasaia
alikuwa ni kiongozi wa Kanisa na hakuwa Mwoga alikuwa akisimamia
anachokiamini hadi mwisho na hata siku Moja hakuwahi na tabia kama za
baadhi ya Vyanzo Vya Habari vingine ambavyo vinakupa taarifa Fulani
ukaandike Kwenye magazeti ,halafu akiona taarifa hiyo amebanwa ,Chanzo
hicho kinaibuka na kumkana Mwandishi wa Habari Kuwa hakumpa hiyo
Mwandishi wa Habari.Nilimpenda sasa .
Mtikila
alikuwa akishavamiwa na polisi nyumbani kwake Ilala mchikichini,
Mikocheni alikuwa akimtaka Mkewe ( GORGIA ) anipigie simu haraka mimi (
Happiness ) ili nifikie eneo la tukio niandike Habari.Na kweli nilikuwa
nikifika haraka na kushuhudia Polisi wakiwa wamezingira nyumba yake na
Kisha kumkamata kwenda naye Kituo Cha Polisi Kati.
Ndiyo
maana nililia sana Mtikila alivyofariki na ninavyoandika makala hii
nakumbuka vile vituko vyake,harakati alizokuwa akizifanya za kukuza
Utawala wa Sheria ikiwa ni kwa yeye Kufungua mahakamani Kesi mbalimbali
alizoana Haki na Sheria za nchi zimevunjwa ,kufanya mikutano na
waandishi wa Habari kujadili mambo mbalimbali ya Kitaifa Hali
iliyosababisha umma nao kuacha woga nakuanza kuwakosoa viongozi bila
woga.
Kama
siyo Mtikila na baadhi ya wana mageuzi wengine kama marehemu
Dk.Sengondo Mvungi,James Mapalala, Augustine Mrema, na wengine Leo hii
sisi vijana Tusingekuwa na lakusimulia,au uenda Leo hii tungekuwa na
uwoga kwa Kudai Haki zetu kuikosoa serikali.
Hata
hivyo Leo wakati tukiazimisha Mwaka mmoja wa kifo Chako ( Mtikila )
,Yale maneno yako kuhusu baadhi ya viongozi wenzio Vya vya upinzani Kuwa
siyo wapinzani wa kweli ,wanasalitiana na ndiyo maana hukutaka kabisa
kujiunga na Umoja wa UKAWA kwasababu unafahamu vyema viongozi Hao
wanaounda UKAWA ni wahuni na wasaliti umethibitika Kwani Tayari ndani ya
CUF Hali Si shwari wanatimuana ovyo ovyo na hawaamini tena baadhi ya
viongozi kila mmoja anamuita mwenzio ni msaliti.Pia viongozi wa UKAWA
wametangaza rasmi kumtenga Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye mara kadhaa
ulikuwa ukimpinga Lipumba kuwa siyo mpinzani wa kweli.Hatari sana.
Kwa
Sisi wasomi wa Sheria ,Wadau wa Utawala wa Sheria tutamkumbuka sana
Mtikila na kuenzi na kuthamini mchango wake wa kushiriki kukuza
Demokrasia na utawala wa sheria nchini ikiwa ni pamoja ya yeye Enzi za
Baba waTaifa, Julias Nyerere yupo hai ,Mtikila alikuwa akitumia ujasiri
wake kumkosoa Myerere,Rais Benjamin Mkapa,Jakaya Kikwete. Enzi
walipokuwa madarakani.
Na
wakati akiwakosoa,watawala walidai anatoa maneno ya uchochezi serikali
ikawa ina mfungulia Kesi za uchochezi pale Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu na Kinondoni.
Enzi
za Utawala wa Rais Mkapa, Serikali ilimfungulia kesi za kutoa maneno ya
uchochezi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mfano Kesi maarufu
ambazo sisi waandishi wa Habari za mahakamani tuli zibatiza Kesi ya
Nyerere. Katika Kesi hiyo Mtikila alipokuwa akihutubia mkutano wake
Uwanja wa Jangwani Dar Es Salaam, alisema maneno yafutatayo ( Rais
Nyerere ambaye hivi sasa ni marehemu ni Nyamafu na amekwenda
Kuzimu).Mtikila alikuwa akitetewa na Marehemu Wakili maarufu Moses
Maira. Hii Kesi mwisho wa siku Mtikila aliachiwa huru baada ya Mahakama
kuamua kuifuata .
Kesi
nyingine ni Mtikila alisema Rais Mkapa siyo Raia wa Tanzania ,Ana
ushahidi Kuwa Mkapa ni Raia wa Msumbiji. Mwisho wa siku Mtikila alikuja
Kuachiwa huru na Mahakama ya Kisutu.
Ila
Kesi ya Kusema CCM ndiyo ilimua aliyekuwa Katibu wa Mkuu wa CCM'
iliyokuwa imefunguliwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Hakimu
Gabriel Mirumbe ambaye Kwa sasa ni marehemu mwaka 1999 alimfunga Mtikila
Kifungo cha Mwaka mmoja gerezani. Ni Kesi Moja tu Kati ya zote
aliziwahi kushitakiwa ndiyo aliyofungwa gerezani Mwaka mmoja .
Enzi
za Utawala wa Rais Kikwete ,Mtikila alishitakiwa Mahakama ya Kisutu kwa
Kesi ya kumuita Rais Kikwete anagandamiza Ukristo anakumbatia ugaidi '
Kesi hii Mtikila alishinda na hivyo kuachiliwa huru na Mahakama.
Mtikila
alifungua Kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, kuomba
Mahakama hiyo I mpunguzie madaraka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP)
,aliyopewa katika Kifungu cha 91 ( 1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa
ya Jinai ya Mwaka 2002. Ambapo Kifungu hicho kinampa mamlaka DPP Kufuta
Kesi ya jinai na Hakuna mtu anayepaswa kumhoji.
Septemba
8 Mwaka 2011, Mtikila, alifungua kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam ,akiomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia jengo
la Mahakama ya Rufaa lililopo eneo la Kivukoni Front, lisiuzwe kwa
mmiliki wa Hoteli ya Kempinski.
Kwa
mujibu wa hati ya madai ambayo tayari imeshapewa namba 23 /2011 ,
Mtikila anamshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Katiba na
Sheria na Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kuruhusu jengo hilo la mahakama ya
juu nchini liuzwe.
Mtikila amefungua kesi hiyo
chini ya ibara ya 27(1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977, inayosomeka: “Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri
mali ya mamlaka ya nchi na pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na
ubadhirifu na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio
waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”
Anadai
kuwa amefikia uamuzi wa kuwashtaki walalamikaji hao kwa sababu wadaiwa
hao wana dhamana ya kulinda mali za umma zisifujwe lakini cha kushangaza
ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kwa kushindwa kulinda jengo hilo ambalo
ni mali ya umma na matokeo yake wameshiriki kuharibu mali hiyo ambayo ni
jengo la kihistoria.
Hatua
hiyo ya Mtikila kufungua kesi, imekuja ikiwa ni siku chache toka Waziri
wa Katika na Sheria, Celina Kombani, kuueleza umma kuwa taratibu za
kisheria zimefuatwa za kuliuza jengo hilo. Hadi sasa jengo Hilo la
Mahakama ya Rufaa halijauzwa.
Mtikila
alifungulia Kesi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aliyekuwa
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ,Askofu Dk.Valentino Mokiwa kwa
kumpapasa Makalio ,Kesi ambayo hadi umauti unamkuta ilikuwa bado
haijamalizika.
Mtikila
alifungua kesi ya Kikatiba Na.14/2015 Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar
Es Salaam, kupinga serikali isiwasilishe bungeni muswaada wa kuanzishwa
kwa Mahakama ya Kadhi nchini.Hadi anafariki Dunia Kesi ilikuwa
haijamaliwa na serikali mwisho wa siku serikali ikafuta uamuzi wake wa
muswaada huo bungeni.
Mwaka
2011 , Mtikila alifungua Kesi ya Kikatiba Katika Mahakama ya
Kimataifa ya Haki za Binadamu,Arusha kupinga hukumu Na.45/2009
iliyotolewa na Jopo la Majaji saba wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Katika
rufaa hiyo iliyokuwa imekatwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya
Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akitetewa na wakili wa
kujitegemea Richard Rweyongeza na Mpare Mpoki ambapo Mahakama hiyo ya
juu kabisa nchini ilitengua hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es
Salaam Na. 10/2005 iliyokuwa imeruhusu uwepo wa mgombea binafsi
Tanzania.
Hukumu
hiyo ya kihistoria ilitolewa na Mahakama ya Haki za Binadamu ,Juni 2013
, Mahakama hiyo ilisema Tanzania inakiuka haki za binadamu kakuzuia
uwepo wa mgombea binafsi.
Hakuna
ubishi kwamba hadi Leo tukiazimisha Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa
Mwanasiasa Mkongwe nchini Mtikila Hajapatikana Mbadala wa
Mtikila.Mtikila alikuwa ni Mwanasiasa wa vitendo yaani Anachukua Hatua
za kisheria pindi anapoona au kudhani kuna Sheria na Haki zinavunjwa kwa
kwenda Kufungua Kesi mahakamani siyo Kulalamika majukwaani.
Na
jinsi Watanzania Wengi tulivyo wanafki tena wazandiki wakubwa Leo hii
Mtikila akiwa anatimiza Mwaka mmoja tangu afariki,Hakuna hata Jukwaa
Moja liwe la wasomi wa Sheria ,wanasiasa ,wapenda Mageuzi na hata Ofisi
ya Vyama Vya Siasa vilivyoandaa hata mdahalo wa Kumbukumbu ya kifo cha
Mtikila ambaye ameacha alama Katika siasa za nchi hii na Utawala wa
Sheria .
Mtikila
kasaulika utafikiri alifariki Miaka 300 iliyopita na wakati wa msiba
wake kuna watu wakiwemo viongozi wa kiserikali walitoa Matamko wakisema
ama kwa hakika hawatamsahau Mtikila, Na watambuenzi sana .Unafki mtupu.
Sina
cha kukupa rafiki Mtikila zaidi ya mimi rafiki yako,mwanao kuendelea
kukuenzi kupitia kalamu yangu kwa kuandika makala ili watu waelewe Kuwa
pamoja na Vituko vyako ulivyokuwa ukififanya hapa Duniani Ulipokuwa kama
mwanasiasa pia ulitoa mchango mkubwa Katika kukuza utawala wa Sheria
kwa kutumia Haki yako ya Msingi iliyoainishwa Katika Ibara ya 26 (2) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambayo
inasomeka hivi ;
"Kila
mtu Ana Haki ,kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria,kuchukua Hatua
za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi zinalindwa".
Mtikila
ni Mtanzania ambaye Tunaweza Kusema ni kama alikuwa ni kinara wa kuliko
wa Watanzania wengi kuitumia haki hiyo ya Ibara ya 26(2) ya Katiba ya
Nchi kwenda mahakama mbalimbali hapa nchini kufungua kesi .
Mwaka
1993 ,Mtikila alimfungulia kesi ya Kikatiba Mwanasheria Mkuu wa
Serikali aliyekuwa akitetewa na Wakili wa Serikali Kipenka Mussa ambaye
kwa sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini ,Kesi Namba 5 / 1993
ambapo Mtikila alikuwa akipinga uamuzi wa kuzuiwa mgombea urais ngazi ya
mgombea urais, Ubunge Katika chaguzi za kisiasa ambalo zuio Hilo
lilikuja baada ya kufanyika kwa Mabadiliko ya nane ya Sheria ya Katiba
ya Mwaka 1992.
Ambapo Mabadiliko hayo
yalifanyia marekebisho Ibara ya 39 ya Katiba ya nchi Ambapo Kabla ya
Mabadiliko hayo Ibara ya 39 Ilikuwa ikimtaka mtu yoyote anayetaka
Kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano ni lazima awe ametimiza umri wa
Miaka 40 , pia atakawa na sifa ya Kuwa mbunge mjumbe wa Baraza la
wawakilizi (Zanzibar).
Hitaji la kisheria la
kutaka kila mgombea urais, Ubunge lazima apitishwe na Chama Chake cha
siasa wakati wa uchaguzi pia kimeanishwa katia Ibara ya 67 na 77 ya
Katiba ya nchi pia Local council elections of the Local Authorities
(Elections) Act, 1979,
as amended by the Local Authorities (Elections) (Amendment) Act, _
(Act No 7 of 1992).
Mtikila
Mbele ya Jaji Lugakingira ambaye ni marehemu kwa sasa alidai Hitaji la
linalotaka wagombea wadhaminiwe na vyama vinavunja Ibara ya 21(1) ya
Katiba inatoa Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.
Akitoa
hukumu yake Jaji Lugakingila alisema kwa mujibu wa Ibara ya 39,67,77
pamoja na Kifungu cha 39 Local Authorities (Elections) Act 1979,alisema
ugombea binafsi siyo uvunjifu wa sheria kwa ngazi ya rais .Hata hivyo
Jaji Lugakingira Katika hukumu yake hiyo hakutamka Vifungo hivyo Vya
Sheria ni Batili.
Katika
rufaa iliyokatwa na Mtikila Na. 10 /2009, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa
serikali Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam Mbele ya jopo la
Majaji watatu Amir Manento ( Mstaafu ), Salum Massati ( Sasa ni Jaji wa
Mahakama ya Rufaa) naThomas Mihayo (Mstaafu) .
Katika
rufaa hiyo Na.10/2009 ,Mtikilia aliwasilisha maombi manne. Mtikila
alikuwa anapinga mabadiliko ya nane ya Katiba ya Katiba na akaomba
Mahakama Kuu itamke kuwa marekebisho ya Ibara 39 na 67 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1979 yaliyoanzisha Sheria Na.34 ya
1994 inavunja Katiba .
Ombi
la pili, Mahakama itamke Kuwa mlalamikaji anayo Haki kwa mujibu wa
Ibara ya 21(1) ya Katiba ya nchi Kugombea nafasi ya Ubunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mgombea binafsi. Tatu, alipwe
gharama za kuendesha rufaa hiyo na mjibu rufaa ambaye ni Mwanasheria
Mkuu wa serikali, Nne, anaomba alipwe nafuu nyingine ambazo Mahakama
itona itafaa.
Hata
hivyo jopo Hilo la Majaji watatu Manento,Massati, Mihayo wakitoa
hukumu Yao Walikubali Maombi hayo ya Mwomba rufaa ( Mtikila ) isipokuwa
Mahakama hiyo imelikataa ombi Moja la kutaka alipwe gharama za
uendeshwaji wa Kesi hiyo na badala yak e Mahakama ikaamuru kila upande
Katika Kesi hiyo ibebe gharama zake.
Mwanasheria
Mkuu wa serikali hakuridhishwa na hukumu hiyo alikataa rufaa Mahakama
ya Rufaa Dar es Salaam, na jopo la Majaji saba waliokuwa wakiongozwa na
Jaji Mkuu ambaye kwa sasa ni Mstaafu Augustino Ramadhani , Eusebio
Munuo, January Msoffe ,Nataria Kimaro , Mbarouk Mbarouk, Bernad Luanda,
Mjasiri wasikiliza rufaa hiyo ya Madai 45/2009 dhidi ya Mtikila ambapo
Mwanasheria Mkuu wa serikali aliwasilisha hoja Saba za kupinga hukumu
ya Mahakama Kuu iliyoruhusu uwepo wa mgombea binafsi Lakini baadae
Akaamua kuzifuta Sababu mbili Kati ya Sababu Saba.
Aliyekuwa
Mwanasheria wa serikali Katika Kesi hiyo alikuwa George Masaju ambaye
miongoni mwa hizo Sababu alidai Mahakama Kuu ilikosea kisheria
kwasababu ilishindwa kuanisha Yale yanayobishaniwa kwasababu amri ya 15
Kanuni ya 1(5) ya Sheria ya Madai ya Mwaka 2002 inataka hivyo na kwamba
Mahakama ilikosea kuruhusu mgombea binafsi kwasababu kuna mgawanyo wa
mamlaka na kwamba Ibara ya 67 (1) (b) ya Katiba ya nchi inataka mgombea
Ubunge yoyote lazima awe ni Mwana Chama aliyependekezwa na Chama cha
siasa, hivyo kuruhusu mgombea binafsi wakati Ibara hiyo bado ipo ni
kuingilia Mhimili mwingine wa kutunga Sheria ambao ni Bunge.
Akisoma
hukumu hiyo Jaji Ramadhan alisema Mahakama ya rufaa inatengua hukumu ya
Mahakama Kuu iliyoruhusu mgombea binafsi kwasababu Mahakama Kazi yake
ni kutafsiri Sheria na siyo kutunga Sheria hivyo suala Bunge ndiyo lenye
mamlaka ya kutunga Sheria ya kuruhusu mgombea binafsi na siyo mhimili
wa Mahakama.
Nitaendelea kukukumbuka Mzee wangu Mtikila na kuenzi mazuri uliyoyafanya hapa Duniani na Mabaya sitayafuata.
Hakika
Mtikila pengo Lako bado halijazibwa ,ulikuwa ni mwanasiasa wa vitendo
wa kuzungumza unachokiamini bila woga ,uliipenda Haki na kutetea
Utawala wa Sheria ,hukuogopa kushitakiwa ,ukizungumza,ulishitakiwa
hukuyumba.Wanafunzi wa Sheria vyuoni Tunaposoma somo la Constitution
Law, Human Rights, International Law basi ni lazima walimu watu take
tusome Kesi ya Mtikila One, Mtikila Two na mwisho wa siku wanafunzi wa
Sheria wanaishia Kusema Mtikila ameacha alama Katika tasnia ya Utawala
Sheria
Mungu aiweke roho ya Mtikila Mahali panapostahili .
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
4/10/2016
No comments:
Post a Comment