Showing posts with label Rev. Christopher Mtikila. Show all posts
Showing posts with label Rev. Christopher Mtikila. Show all posts

Saturday, October 08, 2016

Christopher Mtikila, Bado Hajapatikana Mbadala Wako

 
The Late Reverend Christopher Mtikila
CHRISTOPHER MTIKILA BADO HAJAPATIKANA MBADALA WAKO
 
Na Happiness Katabazi

LEO Oktoba 4 Mwaka 2016 , naadhimisha  Mwaka mmoja kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic ( DP) , Mchungaji Christopher Mtikila  tangu alipofariki  kwa ajali ya gari Katika Kijiji cha Msolwa ,Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani ,Barabara Kuu ya Morogoro ,saa 11 alfajiri ya kuamkia Oktoba 4 Mwaka 2015 akitokea Mkoani Njombe Kwenye shughuli za siasa akirejea Dar Es Salaam.

Binafsi urafiki wangu na marehemu Mtikila ulianzia alipoanza kusoma makala na habari zinazohusu habari za mahakamani,siasa nilizokuwa naziandika NA kuchapishwa Katika magazeti Kadhaa nchini.

Mtikila ,Mkewe Georgia na viongozi wa Chama Chake DP, walinipenda sana na Mtikila na Mkewe walinigeuza Kuwa kama binti Yao. 

 Muda  wowote nilikuwa nakwenda nyumbani Kwa Mtikila Enzi zile akiishi lla la Mchikini na hadi alipoamia Katika nyumba Yao Mikocheni nilikuwa nikifika hapo kwake naenda kupiga story na Mtikila na Mkewe tunacheka na Mtikila alipachika jina la ' Mpambanaji' .

Nakumbuka Mtikila yeye alikuwa aogopi mtu Akiamua kuandika Waraka wa kumkosoa,kiongozi yoyote Yule anaingia ofisini kwake ambapo Mikocheni na Ilala alipokuwa akiishi alitenga chumba kimoja kama ofisi ya nyumbani kwake na akawema kompyuta kwaajili ya kufanya kazi zake awapo nyumbani kwake  anaandika waraka mrefu Una maneno makali sana ananiiita niusambaze nami nilikuwa nafanya hivyo .Nilimpenda sana Mzee wangu Mtikila ambaye bado pengo lake halijazibwa  na uenda itatuchukua Miaka Mingi kama  Taifa kumpata mtu wa aina ya Mtikila .

Nikiupeleka waraka wa Mtikila kwa Mhariri ,hataki kuchapisha eti Waraka huo Una matusi hivyo hawezi kuchapa Kwani Gazeti litashitakiwa.Na kweli Mtikila alikuwa aliandika maneno makali Katika Waraka alizokuwa akiziandika.

Kesho yake Mtikila  akiona hakuna gazeti halijachapisha habari yake ,Mtikila ananipigia simu na alikuwa akianza kwa kunisalimia hivi ( Saa ya Ukombozi) minamjibu ni ( Sasa), ananiuliza Hao " wahariri Njaa" kwanini wamekataa kuchapa Habari yake  namweleza Sababu .Mtikila ananiombia  wahariri Hao ni weu wanaho gwa hela na CCM wasitoe Habari zake Kwani eti yeye Mtikila ni Kiboko ya CCM,CCM ina muogopa sana.


Mtikila alikuwa ni mwanasiasa wa aina yake kwani licha ya Kuwa mwanasiasaia alikuwa ni kiongozi wa Kanisa na hakuwa Mwoga alikuwa akisimamia anachokiamini hadi mwisho na hata siku Moja hakuwahi na tabia kama za baadhi ya Vyanzo Vya Habari vingine ambavyo vinakupa  taarifa Fulani ukaandike Kwenye magazeti ,halafu akiona taarifa hiyo amebanwa ,Chanzo hicho kinaibuka na kumkana Mwandishi wa Habari Kuwa hakumpa hiyo Mwandishi wa Habari.Nilimpenda sasa .

Mtikila alikuwa akishavamiwa na polisi nyumbani kwake Ilala mchikichini, Mikocheni  alikuwa akimtaka Mkewe ( GORGIA )  anipigie simu haraka mimi ( Happiness ) ili nifikie eneo la tukio niandike Habari.Na kweli nilikuwa nikifika haraka na kushuhudia Polisi wakiwa wamezingira nyumba yake na Kisha kumkamata kwenda naye Kituo Cha Polisi Kati.

Ndiyo maana nililia sana Mtikila alivyofariki  na ninavyoandika makala hii nakumbuka  vile  vituko vyake,harakati alizokuwa akizifanya za kukuza Utawala wa Sheria ikiwa ni kwa yeye  Kufungua mahakamani Kesi mbalimbali alizoana Haki na Sheria za nchi zimevunjwa ,kufanya mikutano na waandishi wa Habari  kujadili mambo  mbalimbali ya Kitaifa Hali iliyosababisha umma nao kuacha woga nakuanza kuwakosoa viongozi bila woga.

Kama siyo Mtikila na baadhi ya wana mageuzi wengine  kama marehemu Dk.Sengondo Mvungi,James Mapalala, Augustine Mrema,  na wengine Leo hii sisi vijana Tusingekuwa na lakusimulia,au uenda Leo hii  tungekuwa na uwoga kwa Kudai Haki zetu kuikosoa serikali.

Hata hivyo Leo wakati tukiazimisha Mwaka mmoja wa kifo Chako ( Mtikila ) ,Yale maneno yako kuhusu baadhi ya viongozi wenzio Vya vya upinzani Kuwa siyo wapinzani wa kweli ,wanasalitiana na ndiyo maana hukutaka kabisa kujiunga na Umoja wa UKAWA kwasababu unafahamu vyema viongozi Hao wanaounda UKAWA ni wahuni na wasaliti umethibitika Kwani Tayari ndani ya CUF Hali Si shwari wanatimuana ovyo ovyo na hawaamini  tena baadhi ya viongozi kila mmoja anamuita mwenzio ni msaliti.Pia viongozi wa UKAWA wametangaza rasmi kumtenga Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye mara kadhaa ulikuwa ukimpinga Lipumba kuwa siyo mpinzani wa kweli.Hatari sana.

Kwa Sisi wasomi wa Sheria ,Wadau wa Utawala wa Sheria tutamkumbuka sana Mtikila na kuenzi na kuthamini mchango wake wa kushiriki kukuza Demokrasia na utawala wa sheria nchini ikiwa ni pamoja ya yeye Enzi za Baba waTaifa, Julias Nyerere yupo hai ,Mtikila alikuwa akitumia ujasiri wake kumkosoa Myerere,Rais Benjamin Mkapa,Jakaya Kikwete. Enzi walipokuwa madarakani.

Na wakati akiwakosoa,watawala walidai anatoa maneno ya uchochezi serikali ikawa ina mfungulia Kesi za uchochezi pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Kinondoni.

Enzi za Utawala wa Rais Mkapa, Serikali ilimfungulia kesi za kutoa maneno ya uchochezi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  mfano Kesi maarufu ambazo sisi waandishi wa Habari za mahakamani tuli zibatiza Kesi ya Nyerere. Katika Kesi hiyo Mtikila alipokuwa akihutubia mkutano wake Uwanja wa Jangwani Dar Es Salaam, alisema maneno yafutatayo ( Rais Nyerere ambaye hivi sasa ni marehemu ni Nyamafu na amekwenda Kuzimu).Mtikila alikuwa akitetewa na Marehemu Wakili maarufu Moses Maira. Hii Kesi mwisho wa siku Mtikila aliachiwa huru baada ya Mahakama kuamua kuifuata .

Kesi nyingine ni Mtikila alisema Rais Mkapa siyo Raia wa Tanzania ,Ana ushahidi Kuwa Mkapa ni Raia wa Msumbiji. Mwisho wa siku Mtikila alikuja Kuachiwa huru na Mahakama ya Kisutu.

Ila Kesi ya Kusema CCM ndiyo ilimua aliyekuwa Katibu wa Mkuu wa CCM'  iliyokuwa imefunguliwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Hakimu Gabriel Mirumbe ambaye Kwa sasa ni marehemu mwaka 1999 alimfunga Mtikila Kifungo cha Mwaka mmoja gerezani. Ni Kesi Moja tu Kati ya zote aliziwahi kushitakiwa ndiyo aliyofungwa gerezani Mwaka mmoja .


Enzi za Utawala wa Rais Kikwete ,Mtikila alishitakiwa Mahakama ya Kisutu kwa Kesi ya kumuita Rais Kikwete anagandamiza Ukristo anakumbatia ugaidi ' Kesi hii Mtikila alishinda na hivyo kuachiliwa huru na Mahakama.

Mtikila alifungua Kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, kuomba Mahakama hiyo I mpunguzie madaraka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ,aliyopewa katika Kifungu cha 91 ( 1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002. Ambapo Kifungu hicho kinampa mamlaka DPP Kufuta Kesi ya jinai na Hakuna mtu anayepaswa kumhoji.


Septemba 8 Mwaka 2011,  Mtikila, alifungua  kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ,akiomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia jengo la Mahakama ya Rufaa lililopo eneo la Kivukoni Front, lisiuzwe kwa mmiliki wa Hoteli ya Kempinski.

Kwa mujibu wa hati ya madai ambayo tayari imeshapewa namba 23 /2011 , Mtikila anamshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Katiba na Sheria na Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kuruhusu jengo hilo la mahakama ya juu nchini liuzwe.

Mtikila amefungua kesi hiyo chini ya ibara ya 27(1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayosomeka: “Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”

Anadai kuwa amefikia uamuzi wa kuwashtaki walalamikaji hao kwa sababu wadaiwa hao wana dhamana ya kulinda mali za umma zisifujwe lakini cha kushangaza ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kwa kushindwa kulinda jengo hilo ambalo ni mali ya umma na matokeo yake wameshiriki kuharibu mali hiyo ambayo ni jengo la kihistoria.

Hatua hiyo ya Mtikila kufungua kesi, imekuja ikiwa ni siku chache toka Waziri wa Katika na Sheria, Celina Kombani, kuueleza umma kuwa taratibu za kisheria zimefuatwa za kuliuza jengo hilo. Hadi sasa jengo Hilo la Mahakama ya Rufaa halijauzwa.

Mtikila alifungulia Kesi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  Aliyekuwa  Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ,Askofu Dk.Valentino Mokiwa kwa kumpapasa Makalio ,Kesi ambayo hadi umauti unamkuta ilikuwa bado haijamalizika.

Mtikila alifungua kesi ya Kikatiba Na.14/2015 Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, kupinga serikali isiwasilishe bungeni muswaada wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini.Hadi anafariki Dunia  Kesi ilikuwa haijamaliwa na serikali mwisho wa siku serikali ikafuta uamuzi wake wa  muswaada huo bungeni.


Mwaka  2011 , Mtikila  alifungua Kesi ya Kikatiba Katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu,Arusha kupinga hukumu Na.45/2009 iliyotolewa na Jopo la Majaji saba wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Katika rufaa hiyo iliyokuwa imekatwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza na Mpare Mpoki ambapo Mahakama hiyo ya juu kabisa nchini ilitengua hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya  Dar Es Salaam Na. 10/2005 iliyokuwa imeruhusu uwepo wa mgombea binafsi  Tanzania.

Hukumu hiyo ya kihistoria ilitolewa na Mahakama ya Haki za Binadamu ,Juni 2013 , Mahakama hiyo ilisema Tanzania inakiuka haki za binadamu kakuzuia uwepo wa mgombea binafsi.

Hakuna  ubishi kwamba hadi Leo tukiazimisha Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Mwanasiasa Mkongwe nchini Mtikila Hajapatikana Mbadala wa Mtikila.Mtikila alikuwa ni Mwanasiasa  wa vitendo yaani Anachukua Hatua za kisheria pindi anapoona au kudhani kuna Sheria na Haki zinavunjwa kwa kwenda Kufungua Kesi mahakamani siyo Kulalamika majukwaani.

Na jinsi Watanzania Wengi tulivyo wanafki tena wazandiki wakubwa Leo hii Mtikila akiwa anatimiza Mwaka mmoja tangu afariki,Hakuna hata Jukwaa Moja liwe la wasomi wa Sheria ,wanasiasa ,wapenda Mageuzi na hata Ofisi ya Vyama Vya Siasa vilivyoandaa hata mdahalo wa Kumbukumbu ya kifo cha Mtikila ambaye ameacha alama Katika siasa za nchi hii na Utawala wa Sheria .

Mtikila kasaulika utafikiri alifariki Miaka 300 iliyopita na wakati wa msiba wake kuna watu wakiwemo viongozi wa kiserikali walitoa Matamko wakisema ama kwa hakika hawatamsahau Mtikila, Na watambuenzi sana .Unafki mtupu.

Sina cha kukupa rafiki Mtikila zaidi ya mimi rafiki yako,mwanao kuendelea kukuenzi kupitia kalamu yangu kwa kuandika makala ili watu waelewe Kuwa pamoja na Vituko vyako ulivyokuwa ukififanya hapa Duniani Ulipokuwa kama mwanasiasa pia ulitoa mchango mkubwa Katika kukuza utawala wa Sheria kwa kutumia Haki yako ya Msingi iliyoainishwa Katika Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambayo  inasomeka hivi ;

"Kila mtu Ana Haki ,kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria,kuchukua Hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi zinalindwa".

Mtikila ni Mtanzania ambaye Tunaweza Kusema ni kama alikuwa ni kinara wa kuliko wa Watanzania wengi kuitumia haki hiyo ya Ibara ya 26(2) ya Katiba ya Nchi kwenda mahakama mbalimbali hapa nchini kufungua kesi .


Mwaka 1993 ,Mtikila alimfungulia kesi ya Kikatiba Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyekuwa akitetewa na Wakili wa Serikali Kipenka Mussa ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini ,Kesi  Namba 5 / 1993 ambapo Mtikila alikuwa akipinga uamuzi wa kuzuiwa mgombea urais ngazi ya mgombea urais, Ubunge Katika chaguzi za kisiasa ambalo zuio Hilo lilikuja baada ya kufanyika kwa Mabadiliko ya nane ya Sheria ya Katiba ya Mwaka 1992. 

Ambapo  Mabadiliko hayo yalifanyia marekebisho   Ibara ya 39 ya Katiba ya nchi Ambapo Kabla ya Mabadiliko hayo  Ibara ya 39 Ilikuwa ikimtaka mtu yoyote anayetaka Kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano ni lazima awe ametimiza umri wa Miaka 40 , pia atakawa na sifa ya Kuwa mbunge mjumbe wa Baraza la wawakilizi (Zanzibar).

Hitaji la kisheria la kutaka kila mgombea urais, Ubunge lazima apitishwe na Chama Chake cha siasa wakati wa uchaguzi  pia kimeanishwa katia Ibara ya 67 na 77 ya Katiba ya nchi pia Local council elections of the Local Authorities (Elections) Act, 1979, 
as amended by the Local Authorities (Elections) (Amendment) Act, _ 
(Act No 7 of 1992). 

Mtikila Mbele ya Jaji Lugakingira ambaye ni marehemu kwa sasa alidai Hitaji la linalotaka wagombea wadhaminiwe na vyama vinavunja Ibara ya 21(1) ya Katiba inatoa Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.

Akitoa hukumu yake Jaji Lugakingila alisema kwa mujibu wa Ibara ya 39,67,77 pamoja na Kifungu cha 39 Local Authorities (Elections) Act 1979,alisema ugombea binafsi siyo uvunjifu wa sheria  kwa ngazi ya rais .Hata hivyo Jaji Lugakingira Katika hukumu yake hiyo hakutamka Vifungo hivyo Vya Sheria ni Batili.

Katika rufaa iliyokatwa na Mtikila Na. 10 /2009, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam Mbele ya jopo la Majaji watatu Amir Manento ( Mstaafu ), Salum Massati ( Sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa) naThomas Mihayo (Mstaafu) .

Katika rufaa hiyo Na.10/2009 ,Mtikilia aliwasilisha maombi manne.  Mtikila alikuwa anapinga mabadiliko ya nane ya Katiba ya Katiba na akaomba Mahakama Kuu itamke kuwa marekebisho ya Ibara 39 na 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1979 yaliyoanzisha Sheria Na.34 ya 1994 inavunja Katiba .

Ombi la pili, Mahakama itamke Kuwa mlalamikaji anayo Haki kwa mujibu wa Ibara ya 21(1) ya Katiba ya nchi  Kugombea nafasi ya Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mgombea binafsi. Tatu, alipwe gharama za kuendesha rufaa hiyo na mjibu rufaa ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa serikali, Nne, anaomba alipwe nafuu nyingine  ambazo Mahakama itona itafaa.

Hata hivyo  jopo Hilo la Majaji watatu Manento,Massati, Mihayo wakitoa hukumu Yao Walikubali Maombi hayo  ya Mwomba rufaa ( Mtikila ) isipokuwa Mahakama hiyo imelikataa ombi Moja la kutaka alipwe gharama za uendeshwaji wa Kesi hiyo na badala yak e Mahakama ikaamuru kila upande Katika Kesi hiyo ibebe gharama zake.


Mwanasheria Mkuu wa serikali hakuridhishwa na hukumu hiyo alikataa rufaa Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam, na jopo la Majaji saba waliokuwa wakiongozwa na Jaji Mkuu ambaye kwa sasa ni Mstaafu Augustino Ramadhani , Eusebio  Munuo, January Msoffe ,Nataria Kimaro , Mbarouk Mbarouk, Bernad Luanda, Mjasiri  wasikiliza rufaa hiyo ya Madai 45/2009 dhidi ya Mtikila ambapo Mwanasheria Mkuu wa serikali aliwasilisha hoja Saba za kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyoruhusu uwepo wa mgombea binafsi Lakini baadae Akaamua kuzifuta Sababu mbili Kati ya Sababu Saba.

Aliyekuwa Mwanasheria wa serikali Katika Kesi hiyo alikuwa George Masaju  ambaye miongoni mwa hizo Sababu alidai  Mahakama Kuu ilikosea kisheria kwasababu ilishindwa kuanisha Yale yanayobishaniwa kwasababu amri ya 15 Kanuni ya 1(5) ya Sheria ya Madai ya Mwaka 2002 inataka  hivyo na kwamba Mahakama ilikosea kuruhusu mgombea binafsi kwasababu kuna mgawanyo wa mamlaka na kwamba Ibara ya 67 (1) (b)  ya Katiba ya nchi inataka mgombea Ubunge yoyote lazima awe ni Mwana Chama aliyependekezwa na Chama cha siasa, hivyo kuruhusu mgombea binafsi wakati Ibara hiyo bado ipo ni kuingilia Mhimili mwingine wa kutunga Sheria ambao ni Bunge.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Ramadhan alisema Mahakama ya rufaa inatengua hukumu ya Mahakama Kuu iliyoruhusu mgombea binafsi kwasababu Mahakama Kazi yake ni kutafsiri Sheria na siyo kutunga Sheria hivyo suala Bunge ndiyo lenye mamlaka ya kutunga Sheria ya kuruhusu mgombea binafsi na siyo mhimili wa Mahakama.

Nitaendelea kukukumbuka  Mzee wangu Mtikila na kuenzi mazuri uliyoyafanya hapa Duniani na Mabaya sitayafuata. 

Hakika Mtikila pengo Lako bado halijazibwa ,ulikuwa ni mwanasiasa wa vitendo wa kuzungumza unachokiamini  bila woga ,uliipenda Haki na kutetea Utawala wa Sheria ,hukuogopa kushitakiwa ,ukizungumza,ulishitakiwa hukuyumba.Wanafunzi wa Sheria vyuoni  Tunaposoma somo la Constitution Law, Human Rights, International Law basi ni lazima walimu watu take tusome Kesi ya Mtikila One, Mtikila Two na mwisho wa siku wanafunzi wa Sheria wanaishia Kusema Mtikila ameacha alama Katika tasnia ya Utawala Sheria
 

Mungu aiweke roho ya Mtikila Mahali panapostahili .

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
4/10/2016

 

Friday, January 04, 2013

Barua ya Wazi kwa WaTanzania Kuhusu Wanyrwanda Nchini

Imeandikwa na Mchungaji Christopher Mtikila

MAANGAMIZI YA KUTISHA YA WANANCHI WA BULIGI

(Wanyarwanda wahusika na unyama dhidi ya Wasukuma)

Hii ni Taarifa ya kuteketezwa zaidi ya nyumba 500 za wananchi wa kabila la Wasukuma kwa moto, pamoja na tani nyingi za mazao yao ambayo ni pamoja na mpunga, mahindi, maharagwe, mtama, dengu, uwele, serena, pamoja na mali zao zingine, katika eneo liitwalo Buligi, katika Wilaya ya Muleba. Unyama huu wahusika wamejaribu kuuficha kwa jina la ‘Opresheni Okoa mazingira’.

Ni lengo la Katiba ya Nchi yetu na Sheria pamoja na taarifa ifuatayo, kwamba wote waliohusika na maangamizi haya waadhibiwe vikali, na wananchi wote waliofanyiwa unyama huu ni lazima walipwe fidia za mali zao na mateso ya kutisha waliyopata. Baada ya kuchomewa nyumba zao na mali zao zote wananchi wengi wamelundikana makanisani, na wengi wako maporini wakikimbia unyama wa kutisha na kuporwa mali zao. Vijiji vilivyoteketezwa ni pamoja na Nyamiranda, Itunzi, Kasharara na Kiteme. Uharamia uliendelea mpaka maeneo ya Karagwe na Biharamulo kama alivyoeleza Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika vyombo vya habari, kama gazeti la Mtanzania Toleo nambari 7142 la tarehe 17/11/2012. Utetezi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Col. Fabian Masawe wa maangamizi ya kutisha ya Wasukuma, kama ulivyokuwa ule wa Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini, kwamba ilikuwa opresheni maalum iliyolenga kuondoa wahamiaji haramu wenye maelfu ya ng’ombe katika Hifadhi ya Taifa ya Buligiuna ukweli. Lakini Wasukuma si wahamiaji haramu, kwa sababu ni wazawa katika nchi yao, na hayo maelfu ya ng’ombe katika hifadhi si ya Wasukuma bali ni ya Watusi wa Rwanda.

KIINI CHA MATATIZO YA WATUSI DUNIANI

Hakuna asiyejua kuwa malengo makuu ya kuanzishwa Umoja wa Mataifa ni pamoja na kulinda haki na usawa wa binadamu wote ulimwenguni, ili idumu amani na kuleta maendeleo katika kuboresha maisha ya binadamu. Ndiyo maana ile sera ya Makaburu ya udhalilishaji wa mtu mweusi au ubaguzi wa rangi waliyoiita apartheid ilipigwa vita na dunia yote, mpaka ikatokomezwa. Hata ushujaa wa Nelson Mandela unaopita umaarufu wa kiongozi mwingine yeyote duniani, aliupata kwa sababu ya uhanga wake katika kutetea usawa wa binadamu wa rangi zote duniani. Lakiniapartheid ya Makaburu haikuweza kuufikia ushetani wa Watusi, jinsi wanavyowadhalilisha Wahutu na Wabantu wengine, kwa imani yao chafu sana kwamba wao eti waliumbwa kwa ajili ya kutawala tu, na kwamba Wahutu waliumbwa kwa ajili ya kuwa watumwa wao! Ni makufuru yanayojulikana wazi ya Watusi kuwatema mate Wahutu au Wabantu wengine kwa kinyaa kama vile ni mavi mbele zao. Na imani yao hii ya kishetani ndilo chimbuko la mbinu na mikakati yao yote ya kutawala siyo tu Maziwa Makuu bali hatimaye hata Afrika yote ya ‘watumwa’ wao!Tabia ya Watusi ya kula wao kwanza, halafu kuwatupia makombo watumwa wao (Wahutu), tena baada ya kuyatemea mate na makohozi, ni historia inayojulikana na kila mzawa wa Maziwa Makuu. Hata maendeleo yalipozidi kutowesha giza hili, bado wanawake Watusi walilazimika kudumisha udhalili wa Wabantu kwa kuolewa na wale wenye mali lakini mimba wapate kwa Watusi wenzao, ikibidi hata kwa ndugu zao wa damu kama hakuna Watusi wengine karibu. Historia itamuenzi shujaa Gregory Kayibanda wa Rwanda kuliko inavyomuenzi Nelson Mandela wa Afrika Kusini, kwa kutokomeza ile apartheid chafu kupindukia ya Watusi nchini Rwanda mwaka 1959. Ukweli ni budi uheshimiwe na dunia kwamba Watusi wengi walikimbia kutoka Rwanda kufuatia mapindizi yale, kwa sababu ya kukwepa balaa ya kuwa chini ya watumwa wao!Watusiwalikimbilia Burundi na Tanganyika kwa baba yao Julius Nyerere, kujipanga kwa ajili ya “kurudisha ubwana wao juu ya watumwa wao” Rwanda. Kwa imani ya kishetani ya Watusi, Watanganyika kwao wao ni mataahira tu kama Wabantu wenzao yaani Wahutu. Hata bila kupayuka Watusi wanarithishana imani kwamba sisi tuliumbwa kwa ajili ya kuwa watumwa wao. Ubwana wa Watusi uliimarishwa kwa kupandikizwa utwana katika mioyo ya Watanganyika, wa kuwaona Watusi kuwa bora kuliko Wahutu pamoja na hata sisi wenyewe! Hali hii ndiyo iliyowezesha Watusi kujipenyeza katika sehemu zote nyeti za utawala wa Nchi yetu, pamoja na uhodari wao katika matumizi ya rushwa ya mapesa na chambo cha wanawake zao (the Tutsi sexual diplomacy). Ndivyo Watusi walivyofanikiwa hata kuiteka kifikra jumuiya ya kimataifa, ikabariki na kuwasaidia kuangamiza Wahutu zaidi ya milioni sita, na hata kugeuza kibao kuhusu genocide ya Rwanda kwamba Wahutu ndio walioangamiza Watusi! Ndiyo maana nchi yetu ilipokuwa na wakimbizi wa Kitusi na wa Kihutu, Watusi walipendelewa kwa kuhudumiwa kama wafalme na kuandaliwa kurudi “kuikomboa” Rwanda. Kwani ingawa Rwanda ilikuwa na utawala wa kidemokrasi wa Wahutu walio wengi kwa asilimia 85%Watusi wakiwa asilimia 14% tu, ni haramu Watusi kuwa chini ya Wahutu kwavile eti ni watumwa wao! Ni kweli kwamba matokeo ya ufisadi nautwana wa watawala wetu wanaoamini katika ubwana wa Watusi, ni pamoja na kufurahisha Watusi na baba yao Nyerere kwa kuhusika kwa serikali yetu katika yafuatayo:

1. Maangamizi ya Wahutu zaidi ya 6,000,000,

2. Uvamizi wa Jamhuri ya Rwanda kupitia Uganda na Burundi, ambapo maandalizi kwa sehemu kubwa yalifanyikia nchini mwetu kwa mkono wa Serikali ya CCM. 3. Kuhusika kikamilifu na mauaji ya kinyama ya marais watatu Wahutu wa Burundi na Rwanda yaani Melchior Ndadaye, Juvenal Habyarimana na Cyprien Ntaryamira pamoja na ujumbe wao wote, na ushetani mwingine wa kutisha.

4. Kujiuza utumwani kwa Watusi, na kutumika kuliingiza eneo la Maziwa Makuu katika Himaya yao, kwa kuwasaidia kuingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati hawana sifa kabisa kulingana na Mkataba wa Uundaji wa Jumuiya(EAC), kwa unyama wa ‘apartheid’ na genocide yao.

5. Kusaidia uvamizi wa DRC uliofanywa na Kagame na Mseveni, watawala wetu wakaivika aibu kubwa Nchi yetu kwa kukataa kushiriki katika Jeshi la SADC (SADC Alliance) la kusaidia ndugu zetu dhidi ya maharamia, Nchi yetu ikaongopea dunia bila aibu kwamba eti haiko upande wowote kati ya wavamizi na mnyonge aliyevamiwa!

6. Kuwarudishia RPF Wahutu takriban milioni moja kwa unyama usiosemeka, waliokuwa wameyakimbia mauaji ya kinyama ya RPF baada ya kuvamia nchi yao, RPF wakawapokea na kuwaangamiza wote, na kumwaga maiti zao kwa maelfu katika mto Kagera, zikawa zinafunika Ziwa Victoria mpaka General Mboma alipotoa Tamko la kuvamia Rwanda kukomesha ushetani huu wa RPF, kama wasingeacha unyama huo mara moja.

Nchi yetu inakabiliwa na kisasi cha Mwenyezi Mungu! Na ishara tayari zinaonekana! Kuna kuacha upumbavu na kutengeneza na Mwenyezi Mungu, ama mapigo makali kuliko yaliyoipiga Misri, yatakayosimuliwa vizazi vyote! Kwa ufisadi na utwana wa watawala wa nchi yetu kwa Watusi, bila chembe ya aibu wala hofu kwa Mwenyezi Mungu waliikaribisha katika ardhi yetu ICTR, ikiwa nyenzo maalum ya kuwasaidia Watusi kuangamiza Wahutu wote wenye uwezo kiuchumi na kifikra duniani! Kenya iliikataa ICTR katika ardhi yake, kwa kumwogopa Mungu kwa sababu ni nyenzo ya genocideiliyoangamiza mamilioni ya Wahutu, ikawafuata mpaka na wale milioni 2.5 waliokuwa wamekimbizia uhai wao Mashariki ya Congo, na kuwateketeza kinyama! Kupenyezwa kwa Watusi katika ngazi zote nyeti za utawala wa nchi yetu kumewezesha Utusi kuteka nyara sera za nchi yetu zitumikie maslahi ya Watusi, kwa gharama ya heshima ya utaifa wetu na maslahi ya nchi yetu. Na siyo siri kwamba msingi wa laana hii yote iliyoonywa na Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu la Torati, ulijengwa na dikteta Julius Nyerere, ambaye leo anawekwa mahali pa Mwenyezi Mungu na kufanyiwa ibada ya ‘ubaba’ wa Taifa! Utekelezaji wa ndoto ya Nyerere ya kuweka eneo lote la Maziwa Makuu chini ya Himaya ya Watusi unasimamiwa na vijana wake, madikteta Yoweri Museveni na Paul Kagame aliyeangamiza mamilioni mengi ya binadamu duniani kuliko Adolf Hitler.

Propaganda za ‘Jumuiya au Shirikisho la Afrika Mashariki’ zinazopigiwa debe kwa nguvu na hawa Watusi, ni katika ujenzi wa hiyo Himaya yao. Dikteta Yoweri Museveni ametangaza mara kadhaa haki yake ya kustahili kuwa Rais wa kwanza wa shirikisho la Maziwa Makuu (Himaya ya Watusi), na anacho kikosi cha majasusi zaidi ya 400 ndani ya Nchi yetu, yanaoiyeyusha nchi yetu kwa ajili ya kumezwa katika Himaya hiyo, na mafanikio yanaonekana kwa jinsi utawala wetu wa CCM unavyonyenyekea Watusi na kujidhalilisha kwao.

KUMEZWA KWA DRC KATIKA HIMAYA YA WATUSI

Mwuaji wa kutisha Paul Kagame alikwishaikamata DRC baada ya kufanikiwa kumwua Rais Laurent Kabila, akampenyeza madarakani Mnyarwanda Hypolite Adrien Christophe Kanambe kwa jina bandia la ‘Joseph Kabila’. Wauaji wa Rais Laurent Kabila baada ya kutoroshewa Rwanda walikimbiziwa hapa, ambapo walihamishiwa Norway kimya kimya. Mnyarwanda “Joseph Kabila” anayetawala Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kama Gavana wa dikteta Paul Kagame, ni ndugu wa damu wa Mkuu wa Majeshi ya Kagame, yaani James Kabarebe, ambaye pamoja na Kayumba Nyamwasa ndio waliosimamia yale mauaji ya kutisha ya wale Wahutu milioni 2.5 waliokuwa wamekimbilia DRC, ilipovamiwa nchi yao na wauaji wa RPF. Ni sera ya Rwanda kuhakikisha kuwa DRC haiwi na Jeshi imara, mpaka hapo mkakati wa Himaya yao utakapokamilika. Ndiyo sababu maafisa wa juu 7,000 wa Jeshi la DRC ni Wanyarwanda. Hypolite Kanambe (Joseph Kabila) anatumikia maslahi ya Rwanda kwa uzalendo wa hali ya juu, na Rwanda inapovamia DRC pilika za Hypolite A. C. Kanambe huwa ni usanii tu wa kuhadaa ulimwengu. Vinginevyo lazima DRC ingewapa silaha askari Wahutu waliojichimbia Congo, ambao wana uwezo mkubwa sana wa kuutokomeza unyama wa Watusi. Hata uvamizi wa Rwanda wa RPF ulifanikiwa kwa kutanguliza vikwazo vikali sana, vilivyohakikisha kuwa majeshi ya Hayati Rais Habyarimana hayawi na silaha.Historia ni budi iwe sahihi, kwamba vijana wa Nyerere yaani Museveni na Kagame walivamia Zaire kwa maelekezo ya baba yao, bila hayati Laurent Kabila, kwa malengo ya kupanua Himaya yao na kuteka tani za dhahabu na madini mengine mengi ya thamani Gbadolite, Kilomoto, Kinshasa, Kisangani na kwingine, kwa ajili ya kujipatia mabavu ya kiuchumi ya kupanulia Himaya yao, na kugharamia propaganda kali inayohadaa jumuiya ya kimataifa. Dunia ilipoanza kupigia kelele uvamizi huo, ndipo Nyerere alipomtafuta Laurent Kabila haraka, zikiwa zimepita wiki mbili baada ya uvamizi kuanza, na kumtanguliza yeye mbele katika kuhadaa ulimwengu, kwamba ni Wakongo wenyewe walikuwa wanaikomboa nchi yao kutoka kwa dikteta Mobutu! Uvamizi ulipoingia Kinshasa Kabila aliwageuka Watusi kizalendo, na kuwaambia sasa warudi kwao wawaachie Wakongo nchi yao. Kwani aliyekusudiwa na Watusi kuwa gavana wa Rwanda wa koloni hilo ni Bizimana Karahamheto au ‘Bizima Karaha’ kwa jina la hadaa. Uporaji wa kutisha wa utajiri wa DRC ndio mtaji wa jeuri yote ya Kagame leo, ya kuchezea amani ya Maziwa Makuu, na kusambaza maelfu ya majasusi katika nchi za kusini mwa Afrika, kuzifanyia kazi chafu ili hatimaye zimezwe katika Himaya yao, mbali ya kugharamia kikosi chake cha Escadron de la mort kinachoua wapinzani wake popote walipo duniani. Siri ya mkakati wa Nyerere wa Himaya ya Watusi ilionekana tangu alipotaka kuchelewesha uhuru wa Tanganyika, eti mpaka majirani wapate wao ili mkakati ufanikiwe, uhuni ambao ulishindwa kuuhadaa ushujaa kama wa Jomo Kenyatta. Mzee Jomo Kenyatta alipogundua jinsi Nyerere anavyochezea uhuru wa wana wa Tanganyika, hatimaye akaunajisi kwa ‘Muungano’ kwa ajili ya maslahi ya Wamarekani katika vita baridi, alilaani kwamba “Hakika Nyerere anatawala maiti” Ndiyo maana ni Watanganyika peke yao duniani wasiojali uhuru wao, wala hatima yao na vizazi vyao vijavyo, wala maslahi ya Nchi yao! Hii ni baada ya kupigika vizuri vichwani mwao ili wawe kama makondoo ya mtawala, waweze kuvikwa kwa ulaini kongwa la utumwa kwa Watusi, kwa maslahi ya kifisadi ya watumwa walio madarakani, wanaouza utu wao na hatima ya Nchi yao kwa utamu wa tende na halua, zinazomung’unyika mara moja na kupotea! Saa ya ukombozi ni sasa! Ndivyo utaahira wetu unavyoonekana kwa dunia yote ya wenye akili kuhusu kongwa la utumwa la Watanganyika liitwalo “Muungano”, lenye maslahi ya kifisadi ya watwana wachache sana wanaotawala, kama si mmoja tu, lakini kwa gharama ya Uhuru wa Watanganyika, heshima yao na utambulisho wao kama Taifa takatifu la heshima tangu katika Unabii wa Mwenyezi Mungu, tena kwa gharama ya raslimali za Watanganyika na matrilioni ya fedha ya damu yao! Utaahira wetu sisi Watanganyika unaonekana zaidi baada ya Zanzibar kujitoa rasmi katika huo ‘muungano’ kikatiba, ambapo kwa ajili ya maslahi ya kifisadi watawala wetu wanafumbia macho ukweli kwamba muungano umebatilika! Na kwa ujinga kama wa kuku anapodhani haonekani kwavile amefunika macho yake kwa bawa lake, hawa nao wamekazana kuudanganya ulimwengu kwamba muungano bado upo, na hata kulazimisha raia waukiri kiwendawazimu usanii huo! Lakini ukweli ni kwamba baada ya Zanzibar kujitoa rasmi yaani kikatiba katika muungano, Wazanzibari ni wachache sana mafisadi na wasaliti waliohongwa madaraka watetee bila haya usanii wa muungano batili, kwa maslahi yao ya kibinafsi, huku wakisingizia maslahi ya ukupe wa Taifa lao (parasitic advantages) katika damu ya Watanganyika.. Kama chatu anavyomvunjavunja mnyama ili awe rahisi kumezeka, ndivyo Nyerere alivyowahasi kifikra Watanganyika na kuwafisha ari ya ukombozi wao na utaifa wao, mpaka kwa kafara yamwenge, ili wawe rahisi kuvishwa kongwa la utumwa la Watusi. Upofushaji wa jinsi hii huua kabisa uzalendo ndani ya dhamiri ya kila raia katika nchi, na kuwaacha wananchi katika minyororo ya woga tu akilini mwao, badala ya uhanga kwa ajili ya Taifa lao.

KAGAME NA MUSEVENI - HATARI SANA KWA TAIFA LETU!

Uharamia anaoufanya Kagame kule Mashariki ya Congo hapa kwetu alifanikiwa siku nyingi. Tofauti ya DRC Mashariki na mikoa yetu ya Kagera na Kigoma ni kwamba wenzetu wanayo hata majeshi ya mgambo ya uzalendo wao yanayotetea ardhi yao na uhuru wao, kama vile Mai Mai. Lakini sisi tuliuawa kabisa uhanga wetu kwa ajili ya Nchi yetu. Tumebaki kuwasujudia wageni wanaoteka na kuipora nchi yetu, na kututia utumwani katika nchi yetu wenyewe. Hii ndiyo raha ambayo Nyerere aliwaandalia Kagame na Mseveni kwa Watanganyika. Kagame tayari ameingiza katika Nchi yetu Wanyarwandazaidi ya 35,000 wenye silaha, wengi wakiwa katika mapori ya Hifadhi ya Taifa ya Buligi na maelfu ya ng’ombe waliowaingiza kutoka kwao Rwanda na Uganda. Kwani kule kwao wamejiwekea sheria kali ya kuokoa mazingira yao, kwamba ni marufuku mtu kumiliki zaidi ya ng’ombe tano (5). Kwahiyo mamia ya maelfu ya ng’ombe zao wameziingiza katika ardhi yetu kwa njia za porini, na wapo Wanyarwanda wenye ng’ombe mpaka 10,000 mtu mmoja ndani ya Nchi yetu. Maelfu mengi ya ng’ombe hao wa Wanyarwanda wanajulikana kuwa mali ya dikteta Paul Kagame mwenyewe na mawaziri wake, na wengine ni mali ya dikteta Yoweri Mseveni, wengi wakiwa hata na mihuri ya NRA! Mbali ya Hifadhi ya Taifa ya Buligi, maelfu mengi ya ng’ombe wao wamewaswagia katika mapori yetu ya Kasindaga, Katete, Kinesi (Karagwe), Nyakerera, Kyobuheke na Misambya na kwingineko, ambako Wanyarwanda wamejikatia mabuloku makubwa sana (Blocks) ambayo wazawa hawaruhusiwi kukanyaga, na wakithubutu ni kuuawa. Kitendo cha Kagame na Museveni cha kuifanya Nchi yetu kwamba haina Utaifa na heshima ya mipaka yake (sovereignty and territorial integrity) kama zilivyo nchi zao, ni Tangazo la Vita! Ni lazima tujibu mapigo kwa nguvu kuliko tulivyomjibu dikteta Idd Amin Dadah. Majeshi yetu yaanze mazoezi makali ya vita, na raia waanze upya mafunzo ya mgambo kwa ajili ya Nchi yetu. Kama lilivyoanza tatizo la uvamizi wa Kagame DRC Mashariki, maelfu ya Wanyarwanda tayari wamekamata ardhi yetu kubwa sana, kwa kutumia vibali bandia vya kuishi nchini, na makaratasi ya uraia bandia wa Nchi yetu. Jasusi la Kagame liitwalo Athanas Kafurama mara nyingi hudhalilisha wazawa wa nchi yetu kwamba hawana kitu vichwani, na kwamba Tanzania inamjali mtu mwenye pesa yaani kama wao, na siyo raia wake walalahoi! Kagame amefanikiwa kwa sehemu kubwa kuiteka kimya kimya mikoa yetu ya Kagera na Kigoma! Hata Mkuu wa Mkoa wa Kagera Col. Fabian Masawe unamwuma moyo, jinsi Kagame na Mseveni walivyopenyeza askari zaidi ya 35,000, waliojichimbia na maelfu ya ng’ombe, hasa katika Hifadhi ya Taifa ya Buligi. Wanyarwanda wamekamata ardhi yetu kubwa sana, bila kuwa hata na vibali vya kuwepo nchini mwetu. Kabla ya kueleza zaidi juu ya uvamizi wa Buligi mkoani Kagera, tunapenda ifahamike kwamba Mkoa wa Kigoma umeingiliwa na Wanyarwanda na Warundi zaidi ya 100,000, ambao tayari wameteka sehemu kubwa ya ardhi ya Taifa letu, katika upanuzi wa Himaya yao. Tena wanajipenyeza kupitia katika makanisa maalum yanayoeleweka. Tayari wameanza kufanikiwa kukamata utawala wa Nchi yetu, kama vile Mnyarwanda aitwaye Peter Serugamba alivyoteka Jimbo la Kigoma Mjini, au Diwani John wa Kata ya Gungu. Watusi wamegundulika kuwamwagia rushwa viongozi wa vijiji na vitongoji ambao wanawatumia kuiteka ardhi yetu, na nafasi hizo wamepanga kuzichukua wao katika kuijenga Himaya yao. Vikao vya Watusi vya mikakati yao ya kuitwaa Nchi yetu katika Himaya yao mjini Kigoma hufanyikia katika hoteli ya Coast View, iliyojengwa kwa mtaji uliotoka Rwanda, ambao ni utajiri ulioporwa Congo.Watusi hawafichi katika majigambo yao, kwamba wanaweza wasilazimike kutumia nguvu za kijeshi kuitwaa ardhi ya Tanzania, kwa sababu eti wanaweza kutumia rushwa tu na akili kuichukua yote bila shida! Wanaujua udhaifu wetu kwa sababu walijipenyeza katika ngazi zote za utawala wa Nchi yetu, katika majeshi yetu, Uhamiaji, Taasisi zetu za fedha, Usalama wa Taifa n.k. Ndiyo maana Nchi yetu takatifu imetumika katika unyama wa kutisha kwa maslahi ya Watusi. Ni kweli pia kwamba nchi yetu inao watawala wanaoweza kununuliwa kirahisi kwa mapesa ya Wanyarwanda, ng’ombe zao na au mabinti wa Kitusi. Ndiyo maana wanampigia debe na kumwinamia mwuaji wa kutisha Paul Kagame, wakati wanajua kabisa kwamba:

1. Kagame amemwaga kinyama sana damu ya mamilioni ya Wahutu, ambao bado anaendelea kuwaua usiku na mchana, kuliko Adolf Hitler alivyowaua Wayahudi.

2. Kagame anaendesha mauaji dunia nzima, kwa kutumia kikosi chake maalum cha Escadron de la mort, ambacho ndicho alichotumia hata kumwangamiza Bingwa wetu wa Sheria, Hayati Profesa Jwani Mwaikusa, kwa kosa la kuweka wazi katika ICTR kwamba mtuhumiwa mkuu wa genocide katika Maziwa Makuu ni dikteta Paul Kagame. Kagame alihofia kwamba kutokana na majumuisho ya mwisho ya Mwanasheria huyo, lazima Ulimwengu ungelazimisha kukamatwa kwake na kufikishwa mbele ya Sheria.

3. Kagame akiwa na cheo cha Meja alikuwa mstari wa mbele kumwua Rais Thomas Sankara wa Burkina Faso, kule Uagadougou.

4. Kagame alikuwa Burundi kwa ushirikiano wake muhimu na Jean Bikomagu, katika mauaji ya kikatili sana ya marehemu Rais Melchior Ndadaye.

5. Kagame ndiye aliyehusika kikamilifu na utunguaji wa ndege iliyomchukua Rais Juvenal Habyarimana wa Rwanda pamoja na Rais Cyprien Ntaryamira wa Burundi.

6. Kagame analaaniwa na dunia nzima kwa kumfanyia unyama wa kutisha mwanasiasa mwanamke, shujaa Victoire Ingabire, ambaye amemtupa gerezani kwa kosa la kugombea Urais wa Rwanda akiwa Mhutu, na kosa la kuwa na kibali kwa wananchi wa Rwanda kuliko yeye aliyeloa damu ya mamilioni ya binadamu aliowaua kinyama.

7. Kagame amemwaga majasusi zaidi ya 1,000 katika Nchi yetu, wanaotumia ufisadi wa mapesa, ngono n.k katika kutengeneza mazingira ya kutekwa utawala wa nchi yetu na Watusi na hatimaye nchi yetu kuwa mkoa wa Himaya yao. Kama ilivyoelezwa juu, maelfu yao wamefanikiwa kujipenyeza katika taasisi zote nyeti za dola ya Nchi yetu. Walipoishika Uhamiaji waliitumia kujipa uraia na kukamata nafasi nyeti na ardhi yetu pia.

8. Maelfu ya majasusi wa Kagame wanajifanya wanashughulikia mizigo ya Rwanda na Uganda, wengine wanajifanya wafanyabiashara au wanatafuta kuwekeza, wengine wanajifanya wanafunzi. Lakini ukweli ni kwamba Taifa letu liko uchi kwa Kagame, kwa sababu kila tunachokifanya katika Nchi yetu kinaripotiwa Rwanda masaa 24. Katika Jiji la Dar es Salaam, Mikocheni ndiko walikojaa Wanyarwanda hao kama kwao.

ANGALIZO: Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka 1977 kwa sababu moja tu kwamba ilishindikana viongozi wa nchi tatu wananchama yaani Tanzania, Kenya na Uganda kukutana pamoja, kwa ajili ya kupitisha maamuzi yote muhimu ya uendeshaji wa shughuli zote za Jumuiya.

Kwa sababu Rais Julius Nyerere alikataa kukaa meza moja na Rais Idd Amin Dadah wa Uganda, kwa sababu Amin alikuwa mwuaji. “Siwezi kuchangia meza moja na mwuaji aliyeloa damu” alitamka Rais Nyerere, ulimwengu wote ukamuunga mkono hata mgomo wake uliposababisha kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki! SWALI: Ikiwa Nyerere alikataa kukaa meza moja na dikteta Idd Amin kwavile aliua binadamu takriban 350,000, Jumuiya ya Afrika Mashariki ikavunjika kwa sababu ya kuthamini uhai wa binadamu kuliko vitu vingine vyote, hawa watawala wetu wa leo wa CCM ni binadamu wa jinsi gani, ikiwa wanaweza kulikumbatia na kulipigia debe na hata magoti liuaji la kutisha kama Paul Kagame, lililoua kinyama binadamu zaidi ya 6,000,000 Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Kenya, na kuwapelekea wengine kifo kule kule Ulaya walikokuwa wamekimbizia uhai wao? Watu wa hatari kuliko wote kuhusu amani katika Maziwa Makuu ni hawa madikteta, Paul Kagame na Yoweri Museveni, walioangamiza mamilioni ya raia wa Maziwa Makuu, wakavamia Jamhuri dada za Rwanda na Zaire (DRC) na kuangusha tawala za mataifa hayo huru, na kuipora Congo mpaka dunia nzima inawapigia mayowe kama majambazi ya hatari! Watawala wetu wanakuwa katika akili za namna gani wanapokwenda Kampala na Kigali, na kukaa na Kagame na Museveni na kuzungumzia eti amani katika eneo la Maziwa Makuu, wakati hao ndio wavunjaji makatili wa hiyo amani? Hivi ni kweli akina Kikwete hawana hofu kwa Mwenyezi Mungu, kiasi cha kuamua kumsaliti jirani mwema aliyevamiwa na kuangamiziwa mamilioni ya raia wake kwa kosa tu la kuwa Wahutu, na kuwasaidia maharamia waliomvamia? Ni aibu kubwa zaidi kwamba watawala wetu waliishia kukubali umamluki, wa kuwasaidia Kagame na Museveni majeshi eti yakawasaidie kuangamizia Wahutu waliopokonywa nchi yao ya Rwanda, na mashujaa wanaopinga udikteta wa damu wa Yoweri Museveni nchini Uganda! Huku ndiko kuhimiza kisasi cha Mwenyezi Mungu juu ya nchi yetu!



UHARAMIA ULIOFANYWA NA WANYARWANDA BULIGI

Kwanza kabisa, Wanyarwanda hawatasahaulika walivyotikisa Mkoa wa Kagera walipoingia kule kwa uharamia wa kutumia silaha, wakajulikana kwa ufupisho kama Wanyaru. Wanyarwanda waliteka magari, walipora fedha na mali zingine za wananchi, na zaidi waliteka ng’ombe za wananchi na kuzikimbizia Uganda, ambako walizibadilisha na kuleta nchini wale ng’ombe wa kwao, ambao wako tofauti na wetu kimaumbile. Huu ni ujanja wa kawaida wa kijambazi. Uharamia wa Wanyarwanda ulishamiri mno mkoani Kagera, hapo Buligi pakawa kama makao yao makuu ya kutisha, ndiyo maana palipewa jina la Kosovo. Pori lote mpaka Kyamyorwa lilikuwa halipitiki kwa sababu ya hatari ya Wanyaru., ambao walikuja kutokomezwa na ulinzi wa jadi wa Wasukuma na ushirikiano wa dhati wa Kamanda mzalendo wa Polisi, Inspekta Samson ambaye hivi sasa yuko Wilayani Chato Mkoa wa Geita. Kutokana na umahiri wa Wasukuma katika kupambana na uharamia kwa ulinzi wao wa jadi au Sungusungu, Mheshimiwa Wilson Masilingi akiwa Waziri katika Ofisi ya Rais na Mbunge wa Muleba Kusini, alipopita mikoa ya Ukanda wa Ziwa aliwahamasisha Wasukuma kwamba wahamie maeneo ya Kyamyorwa na Kasindaga na kwingine mkoani Kagera, na kwamba wapewe na mashamba kwa sababu ni kweli kwamba Wasukuma kwa asili ni wazalishaji hodari. Wasukuma waliitika mwito huo na kuhamia huko, na ni kweli kwamba waligeuza eneo lile kuwa kitovu cha uzalishaji usio kawaida wa mazao ya mpunga, mahindi, dengu, mtama, ulezi, serena na mengine mengi, mbali ya ufugaji wao. Baadaye Wasukuma hao walihamishiwa Buligi kutoka hapo Kyamyorwa, kwa maombi ya Waziri wa sasa wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, kwa msingi kwamba eneo hilo ni la kampuni ya Itente ambayo yeye ni mhusika. Profesa Anna Tibaijuka aliandika hata katika kitabu chake cha kampeni yake ya Ubunge wa Muleba Kusini, kuwa Wasukuma wengi walikuwa wamepewa eneo la Kyamyorwa kwa makosa, kwavile eneo hilo lilikuwa la Kampuni hiyo. Waziri Anna Tibaijuka anakiri kwamba aliwaombea Wasukuma Serikalini wakapewa uhamisho kwenda Buligi, na kwamba yeye mwenyewe aliwasaidia hata usafiri wa kuhamia Buligi. Wazalishaji wa Kisukuma waliongezeka huko Buligi, baada ya ndugu zao waliokuwa wamewaacha nyuma kuvutiwa na ushuhuda mwema wa uzalishaji wa wenzao waliotangulia huko, baada ya mageuzi ya eneo lililokuwa ‘Kosovo’ kuwa paradiso ya amani na maendeleo. Ni kweli kwamba Wasukuma walipofika uhamishoni Buligi, kwa uhodari wao katika uzalishaji na umahiri wao katika ulinzi wao wa jadi, waliigeuza‘Kosovo’, ikawa kihenge cha chakula cha Mkoa wa Kagera, wakizalisha mpunga, mahindi, maharagwe, dengu, mtama, ngano, uwele, mihogo, migomba, viazi ulaya, vitunguu, nyanya, mboga na hata miti kwa ajili ya hifadhi ya mazingira, kwa kadri walivyoshauriwa kitaalamu. KWAHIYO ukweli hauwezi kukwepeka kwamba :

1. Uchomaji wa nyumba zaidi ya 500 za wananchi wa kabila la Wasukuma katika maeneo ya Buligi na mengineyo kwa kisingizio cha ‘Operation Okoa Mazingira’ ulilenga kuwaangamiza Wasukuma pamoja na mazao yao tele waliyokuwa nayo majumbani mwao pamoja na mali zao zingine zote.

2. Huko Buligi na maeneo mengine ambako Wasukuma wanazalisha kwa wingi mazao hayo yote, Wasukuma waliletwa na Serikali, si wavamizi.

3. Wasukuma hawakuvamia mapori ya Wanyarwanda au ya mtu mwingine yeyote. Kwani Vijiji vyote wanavyoishi vinawatambua, hata kwa mchango wao mkubwa sana katika uzalishaji.

4. Wasukuma hawajaingia katika Hifadhi ya Taifa, wala hawana ng’ombe hata mmoja katika Hifadhi, bali Wanyarwanda ndio wenye mamia ya maelfu ya ng’ombe katika Hifadhi, ambamo hata wanyamapori wetu Wanyarwanda wamewamaliza. Wanyarwanda huhonga mamilioni ya fedha na ng’ombe kwa maafisa wa wanyamapori na watumishi wengine wa umma.

5. “Operation Okoa Mazingira” haikulenga wahamiaji haramu ambao ni Wanyarwanda, wala mamia ya maelfu ya ng’ombe zao kutoka Rwanda na Uganda hususan katika Hifadhi ya Taifa, kwa sabau Wanyarwanda hawakuguswa kabisa, bali walikuwa wakishangilia wanavyofanyiwa unyama Wasukuma, ambao wala hawana ng’ombe katika Hifadhi kunakoharibiwa mazingira!

6. Nyumba za Wasukuma zilizoteketezwa hazikuwa katika Hifadhi, bali katika vijiji na vitongoji rasmi vyenye serikali halali za Vijiji na Vitongoji. Mfano ni nyumba 105 za Kishonga B Barabara ya 9, katika Kijiji cha Nyamilanda Kitongoji cha Nyakabingo, na Kijiji cha Itunzi Kitongoji cha Miziro. Wenyeviti wa Vijiji vya Nyamilanda na Itunzi ni mashahidi, na wanalalamikia unyama wa kuchomewa nyumba wananchi wao.

7. Uteketezaji wa nyumba za Wasukuma uliambatana na unyang’anyi wa pesa zao, kuanzia shs 100,000/- hadi shs 4,000,000/- kwa Msukuma mmoja, na kuwapa stakabadhi feki zilizoandikwa “WAZABUNI WA MASOKO/ MIALO/VIVUKO. Eti ADHABU kwa ajili ya hatia zilizobuniwa zikiwa ni pamoja nauharibifu wa mazingira, kufyeka misitu ovyo, zingine ziliandikwa ‘Kusafirisha mifugo bila kibali’ Tunaambatanisha vivuli vya stakabadhi feki zilizotumika (Nambari 135559, 135519, 135562, 135356, 135520,135367). Tena walipora mapesa mengi sana kuliko waliyoandika katika stakabadhi, na walio wengi hawakepewa hizo karatasi! Huu ni unyang’anyi na ujambazi wa wazi kabisa! Tunawaachia kazi DCI na Takukuru.

8. Maelfu ya wananchi waliofanyiwa unyama huu walilundikana makanisani, kwa ndugu zao na marafiki zao, na wengi walilazimika kuishi maporini, ambako wanawake wapatao watatu walijifungua kama wanyamapori.

9. Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Lemberis Kipuyo, ambaye alikuwa ameonwa na Mnyarwanda aitwaye Athanas Habamungu Kafurama, na kibaraka wa Wanyarwanda ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana aitwaye Julius Rwechungura, baada ya kuchangwa shilingi milioni 100 katika kikao cha Wanyarwanda katika kanisa lao la Butera tareke 31/10/2012, kulingana na majigambo ya Wanyarwanda na Kafurama mwenyewe, ndiye aliyeonekana kusimamia unyama huo, ingawa yeye ndiye mwangalizi wa amani na usalama katika Wilaya!

10. Mkuu wa Wilaya Lemberis Kipuyo alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu unyama huu wa kutisha, alikiri kwamba wamechoma moto nyumba eti zilizokuwa katika Hifadhi, eti kwa ajili ya kulinda mazingira ya Mkoa wa Kagera na kuhamisha wahamiaji haramu wanaoingia na makundi makubwa ya ng’ombe katika Hifadhi.

11. Kama alivyoeleza Lemberis Kipuyo, unyama huo wa kutisha uliosukwa na Wanyarwanda na kutekelezwa kwa usimamizi wake yeye mwenyewe Mkuu wa Wilaya, ulianza tarehe 3/11/2012 saa 3 asubuhi katika eneo la Buligi. Na kama alivyosema hata yeye Mkuu wa Wilaya, maharamia waliowafanyia wananchi wa kabila la Wasukuma unyama huu ni: Askari wa Jeshi la Polisi Usalama wa Taifa Takukuru Wafanyakazi wa Idara ya Misitu Wafanyakazi wa Idara ya Uvuvi, ambao baadhi yao walitambulika. Askari wa Wanyamapori, ambao baadhi yao walitambulika. Askari wa Jeshi la Ulinzi, waliotambulika kwa sare zao. Maharamia waliovaa sare za Mgambo. Lemberis Kipuyo alisema walikuwemo pia Wanasheria katika unyama huu.

12. Wananchi waathirika walipokusanyika Kituo cha Polisi Miziro, Mkuu wa Wilaya Lemberis Kipuyo alifika hapo. Lakini alipoombwa afike ajionee makazi ya wananchi wake yalivyoteketezwa, aliwapuuza isivyo kawaida hata kibinadamu, ingawa umbali haufiki hata kilometa!

13. Kwa kuhofia makusanyiko ya vilio vya Wasukuma, jasusi Mnyarwanda Athanas Kafurama alikwenda kumchochea Mkuu wa Wilaya azidishe unyama kwa madai kwamba eti Wasukuma wamejiandaa kuvamia Kituo cha Polisi Miziro. Ndipo unyama ulipozidishwa maradufu kuwaangamiza Wasukuma, na kuwawinda wale wote wanaoogopwa kama waelewa, na wengi ikawabidi kukimbilia maporini na kuishi huko kama wanyamapori licha ya mvua nzito.

WANYARWANDA WALIVYOIPINDUA OPRESHENI DHIDI YAO

(Kwa kuwageuzia kibao hicho Wasukuma)

Wanyarwanda walipoijua ‘Opresheni Okoa Mazingira’ kwamba imeandaliwa rasmi kwa ajili ya kuwatokomeza wahamiaji haramu yaani wao, na kwavile waliwashika mkononi viongozi wote kuanzia Mkuu wa Wilaya kama walivyokuwa wanajigamba, na kama walivyokuwa wanajihami kwa rushwa kwa uharamia wao wote wanaoifanyia Nchi yetu, ndivyo walivyojipanga kuwatoa kafara Wasukuma Serikali yetu ilikuwa na taarifa zote za mikakati ya dikteta Kagame na Museveni juu ya Nchi yetu, yaani uvamizi wenye lengo la kuiteka ardhi yetu kama vile wanavyofanya Congo Mashariki, uporaji wa raslimali zetu, na walivyohamishia mamia ya maelfu ya ng’ombe zao katika Hifadhi za Taifa letu na utekaji wa ardhi ya wananchi, na hata kulisha mifugo yao katika mazao ya wananchi, wakitetewa na vibaraka wao ambao ni viongozi wetu wala rushwa.

Wamiliki halisi wa haya mamia ya maelfu ya ng’ombe ni marais na mawaziri wa Rwanda na Uganda, ambao wanayo mahusiano ya kifisadi na viongozi wetu mafisadi au Watusi kama wao. Ndiyo maana azma ya Serikali yetu ya ‘Opresheni Okoa Mazingira’ imekuwa ikipozwa kwa ufisadi kwa muda mrefu, huku maadui wakizidi kujichimbia na kuangamiza mazingira. Lakini kwa nguvu ya wale viongozi wetu waliobaki na uzalendo, Serikali yetu ilikazana na mpango kabambe wa OPERATION ‘OKOA MAZINGIRA’, kwa ajili ya kutokomeza kabisa uvamizi wa Watusi katika Nchi yetu (wahamiaji haramu), na kutowesha ng’ombe zote zilizoingizwa katika Nchi yetu, zenye kuhatarisha uhai wa vizazi vyetu vijavyo kwa kuharibu vibaya sana mazingira. Kilio cha wananchi juu ya uvamizi wa ardhi yetu na kuingizwa maelfu ya ng’ombe katika Nchi yetu kutoka Rwanda na Uganda kilianza mwaka 2009. Wanyarwandawalipopata taarifa juu ya ‘Opresheni Okoa Mazingira’ dhidi yao, walifanya mikutano kadhaa mizito katika kanisa lao la Butera, linaloongozwa na Mtusi wa hatari aitwaye Augens.

Tawi la kanisa hilo liko Chanyamisa, Karagwe, ambako pia linatumika kwa mikakati hii ya Kagame. Opresheni Okoa Mazingira iliyokusudiwa kutokomeza wavamizi wa Nchi yetu na maelfu ya mang’ombe yao yanayoharibu mazingira ya Nchi yetu, iligeuzwa na walengwa, Wanyarwanda, kuwa unyama wa kutisha wa kutowesha katika eneo hilo wananchi wa kabila la Wasukuma, na kuwapora mali na ardhi wanayozalishia mavuno yaliyotia fora katika mkoa wa Kagera. Katika kuwatwika Wasukuma dhoruba ya ‘Operation Okoa Mazingira’ ambayo iliwalenga wao, Wanyarwanda walianza kwa kuwachonganisha kirahisi kabisa Wasukuma na ndugu zao Wahaya; Kwavile Mhaya mwenye kulima ekari nne au tano ndiye aliyeonekana kuwa mkulima stadi, lakini Wasukuma wakawa wanalima ekari mpaka 50 mkulima mmoja, Wanyarwanda walitumia kwa ufundi wao kigezo hicho kupandikiza mbegu ya kijicho miongoni mwa Wahaya, ambao wamekuwa wepesi kukabidhi kwa Wanyarwanda ardhi yetu. Hatimaye baadhi ya Wahaya walianza kuwanyoshea kidole Wasukuma kwamba eti wanakamata ardhi kubwa kuliko wao, ingawa mapori hayo yalikuwa yanakaa bure tangu uumbaji mpaka Wasukuma walipoyavamia kwa uzalishaji wa nguvu, hata wakawa wakivuna magunia ya mpunga mpaka 700 mkulima mmoja.Kwa hila za Wanyarwanda, Wahaya wa Muleba na sehemu zingine zilizofanyiwa kazi ya ufitini na Watusi, walianza kujikusanya vikundi vikundi kuandika barua za kuomba ardhi hiyo wanayozalishia Wasukuma, ili mashamba ya Wasukuma yamegwe na kupewa wao, kusudi Wanyarwanda wajipatie kutoka mikononi mwa Wahaya, ambao Watusi wanawachukulia kuwa wepesi zaidi wa kuwapasia wao. Kwa kuwatumia vibaraka wao kama Julius Rwechungura ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana, Wanyarwanda siyo tu wameteka mamia ya ekari za ardhi yetu, bali wamekuwa wanapiga vita siku zote ya kuwafukuza Wasukuma ili wakamate wao maeneo yote. Uharamia huu ndio uliopelekea Mkurugenzi wa Wilaya kumwamuru Afisa Mtendaji Kata ya Kyebitembe kuitisha mkutano wa tarehe 27/3/2012 kuhusu malalamiko ya Wasukuma dhidi ya Wanyarwanda. Mkutano huo ulipiga marufuku kumega ardhi yoyote inayotumiwa na wananchi wa kabila la Wasukuma, kwa ajili ya mapinduzi ya uzalishaji waliyofanikisha katika mkoa, walioingia katika maeneo hayo tangu mwaka 2007 hadi 2011. Mkutano uliamuru pia kufutwa mashitaka ya kihaini yaliyofunguliwa na kibaraka wa Wanyarwanda Julius Rwechungura, akitaka Wasukuma wanyang’anywe mashamba yao ili wapewe Wanyarwanda. Kisha Wanyarwanda walifanya kikao muhimu tarehe 31/10/2012 katika kanisa hilo la Butera, chini ya uongozi wa Jasusi la Kagame liitwalo Innocent Mchunku Kapilipili. Agenda kuu ilikuwa kuchangisha shilingi milioni mia moja kwa ajili ya kujihami nahiyoOpreshenidhidi yao, kwa kuwanunua viongozi wote wa hiyo opresheni. Taarifa za uchunguzi wetu ni kwamba kweli mapesa hayo yalichangwa na kuwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya Lemberis Kipuyo na timu yake iliyoendesha unyama wa kutisha dhidi ya Wasukuma, badala ya wahamiaji haramu. Uchunguzi umethibitisha kuwa Mnyarwanda Innocent Mchunku Kapilipilialikuwa jambazi, katika lile genge la hatari la maharamia kutoka Rwanda waliojulikana kama “Wanyaru” chini ya kamanda wao aliyeitwa ‘Kamanda Dogo’. Mnyaru huyu ameteka zaidi ya ekari 400 za ardhi yetu katika Kijiji cha Nyamilanda, Kitongoji cha Nyakabingo, na Kijiji cha Kisana Kitongoji cha Butera. Mtusi huyu anamiliki zaidi ya ng’ombe 500. Mnyarwanda mwingine muhimu katika kikao cha kanisani Butera ni Francis Magege, ambaye amekamata ekari zaidi ya 400 katika Kijiji cha Nyamilanda, Kitongoji cha Nyakabingo. Kikao hicho kilishirikisha pia Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kisana, msaliti aitwayeJohanson Shumuni, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana, msaliti aitwaye Julius Rwechungura, na Mwenyekiti wa Kitongoji cha NyamtunduAbdon Krophas. Msaliti Johanson Shumuni ametoka katika kifungo cha nje cha mwaka mmoja, kwa kosa la kung’oa mazao ya mwananchi wa Kijiji cha Nyamilanda, kusudi Wanyarwanda wapitishe ng’ombe zao. Kibaraka huyu wa Wanyarwanda alilipishwa pia fidia ya shilingi 70,000/- kwa ajili ya mazao ya wananchi. Wasaliti Johanson Shumuni, Julius Rwechungura na Abdon Krophas kwa pamoja wana kashfa ya kukitapeli Kikotongoji cha Butera msitu wa asili wa mitundu, wakivunga kwamba ni ‘Hifadhi ya Kijiji’ lakini wakawa wanapasua wao mbao na kuzitoroshea nje ya nchi, mpaka moja ya malori ya mbao hizo lilipokamatwa mwaloni Katunguru na kifikishwa Polisi Muleba, mwezi Mei 2010. Lakini watuhumiwa hawajawahi kufikishwa mahakamani mpaka leo, Vibaraka hawa wa Wanyarwanda ndio wahusika wakuu katika kuwauzia ardhi yetu wahamiaji haramu. Mhusika mwingine katika uuzaji wa ardhi kwa Wanyarwanda ni Diwani wa Kata ya Karambi, Ngote, aitwaye Hamudi Abdalla, ambaye hivi sasa anamiliki zaidi ya ng’ombe mia mbili (200) kutokana na rushwa ya Wanyarwanda. Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana, msaliti Julius Rwechungura alidiriki hata kuwafungulia mashitaka mahakamani wananchi wa kabila la Wasukuma, kwamba eti wamevamia ardhi ya machungio ya Wanyarwanda! Kisha aliwawekea dhamana yeye mwenyewe na kuwatoza shilingi 10,000/- kila mmoja. Lakini kibaraka huyo alilazimishwa na kikao cha tarehe 27/3/2012 kilichoamriwa na Mkurugenzi wa Wilaya kufuta kesi hiyo, kwa sababu haiwezi kuwepo ardhi ya Wanyarwanda ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Tanzania!

USHAHIDI WA UKATILI WA WANYARWANDA KWA RAIA WETU

Kwanza kabisa turejee mapokeo ya ile imani chafu sana ya Watusi, kwamba wao wana utu wa hali ya juu zaidi (superior race) kuliko Wabantu. Unyama wa Wanyarwanda ni pamoja na kuwateka nyara raia wetu, na kuwatumia kama watumwa wa kuswaga mifugo yetu waliyotupora.Mateka hawa huvuliwa nguo na kuvikwa vipande vya matambara vya kitumwa, na kubadilishwa majina. Mfano ni vijana wetu Opecatus Filipowa Nsheshe, Kijiji cha Nyamilanda, Kata ya Kyebitembe ambaye aligeuzwa jina na kuitwa Peter, na Antelius wa Kabanga Kijiji cha Kasharara, Kata ya Karambi, aliyegeuzwa jina na kuitwa Rutashambya. Wanyarwanda waliishi porini na hawa ‘watumwa’ kwa miaka miwili. Mmoja wao hatimaye alifanikiwa kuwatoroka, akatoa taarifa Kituo cha Polisi Kyebitembe, ambapo Mkuu wa Kituo hicho shujaa Inspekta Samson alifuatilia kwa uhodari mpaka akafanikiwa kumwokoa yule kijana wetu wa pili. Wale watekaji walikimbia msako huo baada ya kutonywa na msaliti Afisa Mtendaji wa Rwabera, Karagwe, mwanamke aitwaye Alfredina. Raia wetu hao waliokombolewa wana ushuhuda wa kutisha wa unyama uliokuwa ukifanywa na Wanyarwanda. Wanaeleza njia za porini walizokuwa wakipitishia mifugo yetu, mawasiliano ya Wanyarwanda kwa redio na simu dhidi ya mipango yote ya serikali yetu ya kuwafuatilia na mifugo yetu waliyopora. Vijana wanaeleza jinsi walivyotumika kuficha hayo makundi ya ng’ombe zetu, na jinsi walivyoishi kama wanyamapori katika mvua kali na jua na mateso mengi yasiyosemeka. Vijana hawa wanashuhudia jinsi Wanyarwanda walivyomchoma raia wetu kwa upanga wa moto mwilini, kwa kuthubutu kudai ujira wa kutumiwa kikatili kutorosha ng’ombe waliopora katika nchi yetu mpaka huko maporini. Vijana wanashuhudia jinsi wenzao walivyouawa na Wanyarwanda kama wanyama. Zaidi ya yote, anaalaniwa vikali msaliti Johanson Shumuni ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kisana, kwa kumfichia siri mwuaji katili wa Kinyarwanda,‘Mchungaji’ Augens mwenye hilo kanisa la Butera, alipomwua kinyama mfanyakazi wake aliyekuwa anasimamia boti yake iliyokuwa ikifanya kazi za magendo katika Ziwa Buligi, baada ya kumtuhumu kwa wizi wa injini ya hilo boti lake. Shahidi mmojawapo wa mauaji haya ni Benedicto Damian ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji hicho cha Butera. ‘Mchungaji’ hatari Augens pia anashughulika na uvuvi haramu wa kutumia makokoro, unaoangamiza mpaka mbegu ya samaki kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo, Mtusi mwingine aliyeua kinyama raia wetu ni Mchungaji wa kanisa la Mnyarwanda Francis Magege. Huyu alimwua aliyekuwa mchungaji wa ng’ombe zake, baada ya siku tatu akaenda kutoa taarifa ya uongo Polisi kwamba marehemu ameuawa na nyoka. Baada ya kugundulika mwili wa huyo marehemu machakani na kuchunguzwa na Dr. Mtumbi, iliripotiwa kwamba aliuawa kikatili sana kwa kitu kizito chenye ncha kali. NdipoMnyarwanda huyo ‘Mchungaji’ aligeuza kibao na kusema marehemu ameuawa na Msukuma eti aliyekuwa amegombana naye kwa sababu ya kulisha ng’ombe mazao yake. Lakini uchunguzi unaonyesha kuwa marehemu aliuawa baada ya kudaiana na huyo mwajiri wake ‘Mchungaji’. Mashahidi muhimu ni pamoja na huyo Daktari aliyefanya uchunguzi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Butera, na kijana aliyekuwa anachunga pamoja na marehemu, ambaye alikimbilia Ngara. KWAHIYOkwa ajili ya usalama wa Nchi yetu, na heshima na Uhuru wa kweli wa Taifa letu, na sifa ya Taifa letu ya kupigania HAKI na utu wa mwanadamu, tunasisitiza kwamba:

1. Watu wote waliohusika na unyama wa kutisha dhidi ya wananchi wa kabila la Wasukuma Mkoani Kagera, pamoja na Wanyarwanda wote waliohusika na unyama huu wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria. Watuhumiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Lemberis Kipuyo .

2. Wananchi wote waliofanyiwa ukatili huu walipwe fidia ya mateso yote na hasara zote walizosababishiwa na unyama huu.

3. Mamia ya maelfu ya ng’ombe zilizoingizwa nchini mwetu kutoka Uganda na Rwanda zikamatwe na kupigwa mnada, ili fedha hiyo itumike kuboresha Hifadhi zetu na mazingira ya Nchi yetu.


KUHUSU GENOCIDE MAZIWA MAKUU

4. Taifa letu lisimame kinyume kabisa na uharamia wa kuvamia Nchi yoyote huru duniani, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa Jamhuri ya Rwanda na uvamizi na uporaji wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, uliofanywa na Watusi wa RPF na Uganda.

5. Taifa letu lilaani imani chafu ya Watusi(apartheid nyeusi) kwamba wenzao eti waliumbwa kuwa watumwa wao, hivyo kudai usawa wa kibinadamu eti ni uasi wa kuangamizwa kama wanavyofanywa Wahutu.

6. Taifa letu liusaidie ulimwengu kujua ukweli kwamba Watusi ndio walioendesha genocide ya kutisha duniani, kwa kuangamiza Wahutu zaidi ya 6,000,000, zaidi ni mauaji yaliyofanywa na dikteta Paul Kagame wa Rwanda, ambaye ndiye mtuhumiwa Mkuu wa genocide ya Maziwa Makuu.

7. Taifa letu lihakikishe pia kwamba mwuaji Paul Kagame na wenzake wote wanafikishwa mbele ya Sheria kujibumashitaka ya genocide.

8. Taifa letu lifanye TOBA kwa mwenyezi Mungu kwa kudhamini unyama wote uliofanywa na Watusi, ukiwa ni pamoja na mauaji ya marais watatu wa Kihutu wa mataifa ya Rwanda na Burundi, marehemu Rais Melchior Ndadaye, marehemu Rais Juvenal Habyarimana na marehemu Rais Cyprien Ntaryamira.

9. Taifa letu lifanye TOBA kwa kuikaribisha ICTR Arusha, na kuifukuza katika Nchi yetu mara moja, kwa sababu siyo siri kwamba ICTR ni nyenzo ya kusaidia genocide ya dikteta Paul Kagame ya kuwamaliza Wahutu.

10. Taifa letu lipige vita ukatili wa kuendelea kuwashikilia kifungoni Wahutu waliotamkwa na hiyo ICTR kwamba hawana hatia, na kuwatetea kwamba walipwe fidia kwa unyama wote waliotendewa na Kagame pamoja na ICTR na/au UNO.

11. Taifa letu lihakikishe kuwa Rwanda, Burundi na Uganda zinafutwa uanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kwa sababu sharti kuu la uanachama ni Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala wa Sheria, lakini hizi ni tawala za Udikteta wa kikatili na Umwagaji damu.

12. Taifa letu lihakikishe kwamba Dikteta Paul Kagame anamwachia huru mara moja mwanamke mpinzani wake, shujaa Victoire Ingabire, ili akakataliwe na wananchi wenyewe wa Rwanda au wampe uongozi kama wanaona atawafaa. Kutoona haya mbele ya dunia kwa unyama huu, kunadhihirisha Kagame kuwa si binadamu wa kawaida!

Liberty International Foundation

Reverend Christopher Mtikila
(0766 053081, 0713 435016 )
EXECUTIVE CHAIRMAN

Friday, September 26, 2008

Mchungaji Christopher Mtikila alazwa baada ya kupigwa Mawe Tarime


Nimesikitika sana kusikia kuwa Mchungungaji Christopher Mtikila, kapigwa huko Tarime leo. Sisi waTanzania si tulikuwa tunajivunia ni watu wa amani? Sioni sababu ya mtu yeyote hata awe mwanasiasa kutoka chama gani kupigwa.
*******************************************************************

Kutoka Lukwangule Blog (Beda Msimbe):


Mtikila apigwa mawe Tarime

MCHUNGAJI Christopher Mtikila amelazwa katika Zahanati ya Tarime mjini hapa baada ya kupigwa jiwe la kichwani wakati akihutubia kumnadi mgombea wake.

Kwa mujibu wa maelezo ya daktari anayemtibu Mchungaji Mtikila, Philemon Hungiro, kiongozi huyo ameumizwa vibaya na jiwe hilo kisogoni kiasi cha kushonwa nyuzi tatu.

Mtikila alisema alipigwa jiwe hilo na mtu asiyemfahamu wakati akimnadi mgombea ubunge kupitia chama chake cha DP, Denson Makanya, kwenye Uwanja wa Shule ya Sabasaba mjini Tarime.

Jiwe hilo alipigwa majira ya saa 11 jioni leo wakati akitoa ufafanuzi wa taarifa zake kuhusu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.

Wakati akiishambulia Chadema kuhusika na kupanga mauaji hayo, ndipo mtu huyo alipochoropoka kutoka nyuma na kumpiga jiwe la kisogoni.

Hata hivyo, Mchungaji Mtikila alidai kipigo alichokipata ni matokeo ya ahadi ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, kwamba damu itamwagika na kwamba kiongozi huyo akifika Tarime atapigwa mawe.

Awali akihutubia mamia ya wananchi waliofurika katika uwanja huo wa mkutano, Mchungaji aliwataka wananchi kumchagua mbunge anayemnadi kwani yeye hana ufisadi wala mipango ya mauaji.


*****************************************************

Kutoka ippmedia.com

Tarime ni soo!

2008-09-26 16:35:51
Na Mwandishi Wetu, Tarime

Wakati siku za kuelekea uchaguzi mdogo wa kumsaka mbunge wa Jimbo la Tarime zikizidi kukaribia, hali ya kisiasa mjini hapa imeanza kuwa tete baada ya wafuasi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kuendelea kufanyiana visa mfululizo, vikiwemo vile vya kumwagiana pilipili na kuwatwangana mawe mikutanoni.

Uchaguzi huo mdogo, unatarajiwa kufanyika Oktoba 12, ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Marehemu Chacha Wangwe, aliyefariki mjini Dodoma Julai 28 mwaka huu baada ya kupata ajali ya gari.

Jana, muendelezo wa visa vya baadhi ya wafuasi wa vyama hivyo vya CCM, CHADEMA, NCCR-Mageuzi na DP ulifikia pabaya baada ya Mwenyekiti wa UDP, mchungaji Christopher Mtikila kupigwa jiwe la kichwa wakati akiwa kwenye mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya Sabasaba.

Mtikila alijeruhiwa vibaya na kukukimbiziwa hospitali mjini hapa ambako inadaiwa alishonwa nyuzi saba.

Kutokana na vibweka vinavyoendelea katika kampeni za kuelekea siku ya uchaguzi huo, , viongozi mbalimbali wa vyama vilivyosimamisha wagombea wamekuwa wakitoa kauli tofauti kuhusiana na yanayojiri.

Dk. Sengondo Mvungi (NCCR-Mageuzi)
Yeye aliripotiwa kuwa kiongozi wa kwanza kufanyiwa vurugu wakati wa kampeni jimboni humo.

Mvungi alikumbana na kadhia ya kutimuliwa kwa mawe wakati akimnadi mgombea wa chama chake cha NCCR.

Baada ya hapo, Dk. Mvungi ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alilaani tukio hilo na kueleza kuwa ni la hatari, kwani hakuna chama chenye hakimiliki ya jimbo hilo.

Pius Msekwa (CCM)
Makamu huyu Mwenyekiti wa CCM, naye alionja ya joto ya jiwe ya kufanyiwa vituko vya kampeni hizo wakati alipokuwa akimnadi mgombea wa chama chake, Bw. Ryoba Kangoba.

Msekwa alifanyiwa fujo na kuzomewa na watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa vyama pinzani.

Aidha, wafuasi wawili wa chama chake wameripotiwa kuumizwa baada ya mmoja kupigwa jiwe na mwingine kumwagiwa pilipili.

Kutokana na hali hiyo, bosi huyo namba mbili wa CCM akailalamikia hali hiyo na kuripotiwa akitishia kulifikisha suala hilo kwa Rais Jakaya Kikwete ili hatimaye zifanyike taratibu za kudhibiti hali ya namna hiyo ambayo ni ya hatari.

Christopher Mtikila (DP)
Baada ya kasheshe la jana la kupigwa mawe kwenye uwanja wa Sabasaba, amekaririwa akilalamikia hali hiyo aliyodai kuwa imetokana na njama za wapinzani wake.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mtikila amekaririwa leo asubuhi akisema: ``Nilitoa taarifa mapema kwa Msimamizi wa Uchaguzi na OCD.. niliwaeleza juu ya agizo la mimi kupigwa mawe...``

Freeman Mbowe (CHADEMA):Mbowe na chama chake cha CHADEMA wamekuwa nao wakilalama kuonewa na askari polisi walio katika operesheni kali ya kulinda amani katika jimbo hili.

Aidha, kwa nyakati tofauti, yeye, Katibu Mkuu wake Dk. Wilbroad Slaa na Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Halima Mdee, wamekuwa wakitoa madai ya kuonewa kwa kunyimwa viwanja vya kufanyia kampeni za mgombea ubunge wa chama chao, Bw. Charles Mwera.
Prof. Ibrahim Lipumba (CUF)

Baada ya kutosimamisha mgombea jimboni humo ili kuwapa fursa wenzao wa upinzani jimboni humo, Prof. Lipumba na chama chake wamekuwa katika wakati mgumu wa kuamua wamuunge mkono mgombea yupi baada ya wenzao kuwasaliti kwa kusimamisha mgombea zaidi ya mmoja, kinyume cha makubaliano.

Mkanganyiko huo unadaiwa kutokea baada ya vyama vinavyoungana nacho katika umoja wao wa vyama vikiwemo vya CHADEMA, TLP na NCCR-Mageuzi kushindwa kumsimamaisha mgombea mmoja, hasa baada ya NCCR na CHADEMA kusimamisha wagombea wawili tofauti.

Hata hivyo, ingawa CUF Tarime wameamua kumuunga mkono Bw. Charles Mwera wa CHADEMA, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Wilfred Lwakatare, amekaririwa asubuhi ya leo akisema kuwa wamemtuma jimboni humo kiongozi wao Mustafa Wandwi ili kuangalia ni mgombea yupi anayeelekea kukubalika zaidi ili hatimaye wamuunge mkono.

Wakati huohuo, Jeshi la Polisi jimboni humo limesema liko makini katika kudhibiti vitendo vyote vinavyoashiria kuvunja amani.

Akizungumza na Alasiri juzi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Liberatus Barlow, amesema FFU na polisi wengine kibao waliomwagwa jimboni humo wamejipanga vilivyo katika kuhakikisha kuwa uvunjifu wa amani unadhibitiwa ipasavyo.

Wakati huohuo, katika kuthibitisha kuwa Polisi wako makini, tayari wameshawanasa watu wanne wanaotuhumiwa kumvurumishia mawe Mchungahji Mtikila jana na kuwawezesha kuburuzwa kortini.

Walionaswa na polisi katika tukio hilo la jana na ambao leo wamepandishwa kizimbani ili kujibu mashtaka.

Kamanda Barlow amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mussa Peter, Mwita Chacha, Hafidh Stanslaus na Mwita Kilongo.

Amesema watuhumumiwa hao, mmoja alikamatwa wakati wa tukio la kupigwa kwa Bw. Mtikila na wengine watatu walikamatwa jana katika msako wa Polisi uliofuatia kujiri kwa tukio hilo la kupigwa kwa Mtikila.

SOURCE: Alasiri