Friday, July 28, 2017

Tigo Imechangia Kisima kwa wakaazi wa Mji Mpya mkoani Morogoro



Mkuu wa wilaya ya Morogoro mjini, Regina Chonjo (katikati) akikata utepe kuzindua kisima kilichotolewa msaada na kampuni ya Tigo chenye thamani ya shilingi milioni 17/- kwa hospitali ya Mji mpya jana mjini Morogoro. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Meneja wa huduma za jamii Tigo, Halima Okash, Ofisa Mkuu wa Ufundi na Taarifa wa Tigo (CTIO) Jérôme Albou,  na  Diwani wa mji mpya Wence Kalogelezi

Mkazi wa Mji mpya akiwa kabeba ndoo ya maji mara baada ya uzinduzi wa kisima kilichotolewa msaada na kampuni ya Tigo chenye thamani ya shilingi milioni 17/- kwa hospitali ya Mji mpya jana mjini Morogoro.




Mkuu wa wilaya ya Morogoro mjini, Regina Chonjo (katikati) akihutubia wakazi wa Mji mpya mara baada ya  kuzindua kisima kilichotolewa msaada na kampuni ya Tigo chenye thamani ya shilingi milioni 17/- kwa hospitali ya Mji mpya jana mjini Morogoro.



Mkuu wa wilaya ya Morogoro mjini, Regina Chonjo akiwa katika picha ya pamoja  na Wakazi wa Mji Mpya Mkoani Morogoro mara baada ya uzinduzi w kisima hicho.

 kisima kilichotolewa msaada na kampuni ya Tigo chenye thamani ya shilingi milioni 17/- kwa hospitali ya Mji mpya jana mjini Morogoro.


·        Uchangiaji huu ni ishara ya shukurani kwa wakaazi hao kwa kuzima moto katika kituo cha data cha Tigo.

Tarehe 27 Julai 2017 – Tigo Tanzania imechangia kisima chenye thamani ya TZS milioni 17 kwa hosipitali ya Mji Mpya na maeneo yanayoizunguka katika mkoa wa Morogoro kama mkono wa shukurani kwa wakaazi kwa kuhatarisha maisha yao wakati wakipambana na moto ambao ulilipuka katika kituo cha data cha kampuni katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa Tigo, uchimbaji wa kisima hicho pia ulikuwa sambamba na nia ya kampuni hiyo kusaidia ustawi wa jamii ambako Tigo inaendesha  shughuli zake.
Akizungumza katika sherehe za makabidhiano zilizofanyika katika hospitali ya mji mpya katika manispaa ya mji wa Morogoro Afisa Ufundi na Taarifa wa Tigo (CTIO) Jerome Albou alielezea matarajio yake kwamba kisima hicho kitawafikisha mbali sana katika kuondoa suala la upungufu wa maji katika hospitali na pia kutoa maji safi na salama ya uhakika kwa jamii inayokizunguka.
“Tunawashukuru sana watu wa Mji Mpya kwa kuonesha kujali na kujitoa wakati wa kupambana na moto ambao karibu uteketeze kabisa kituo cha Data mapema mwaka huu. Kweli Tigo ina deni kwa wanajamii, serikali ya mtaa na viongozi wa ulinzi na usalama wa manispaa kwa kuitika  kwa wakati kuhakikisha kuwa hakuna uharibifu mkubwa unasababishwa wakati wa moto,” alisema Albou.   
“Kwa hiyo msaada huu, unakuja kutimiza ahadi walioiweka Tigo kwa wakazi wa Mji mwema wa kuwapatia maji safi na salama kama namna ya kutambua juhudi zao katika kulinda mali za kituo hicho cha data.”
Albou alibainisha kwamba uchangiaji huo unakamilisha idadi ya vijiji 20 ambavyo vimenufaika kutokana na jitihada za Tigo za kutoa maji safi na salama nchi nzima, ikiwa inawasaidia zaidi ya watu 187,000.
Mwaka huu, Tigo ina mpango wa kuchimba visima zaidi katika maeneo yanayohitaji ambayo zaidi ya watu 350,000 wanatarajiwa kunufaika katika jitihada zetu za kusaidia juhudi za serikali za kuondoa upungufu wa maji safi na salama nchini.
Makabidhiano yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Stephen Kebwa ambaye aliishukuru Tigo kwa kufikiria kutoa msaada huo. Alisema kwamba kisima hicho kitasaidia utoaji wa huduma bora za kiafya katika hospitali ya Mji Mwema na kusaidia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aliwaomba wasamaria wema wengine kujitokeza na kuunga mkono juhudi za kuondoa upungufu wa maji katika mkoa huo.
Tunapenda kuishukuru Tigo kwa kutusaidia katika juhudi zetu za kutoa huduma za kiafya za uhakika katika eneo hili kwa kutatua tatizo lililokuwepo la upungufu wa maji. Tunaamini kwamba upatikanaji wa maji safi na salama karibu na wakaazi pia itaongeza uzalishaji wa kiuchumi hasa kwa wasichana na wanawake ambao hawatakuwa wanapoteza muda mwingi wa kutafuta maji safi na salama sehemu zingine. Hii itawapatia wasichana fursa ya kuhudhuria masomo kwa uhuru na kuipa jamii fursa ya kuhudhuria kwa ufanisi katika shughuli zao za maendeleo ya Taifa,  Alisema Dr Kebwe. 

No comments: