Saturday, July 27, 2019

TANZIA - Agnes Kabigi

Wadau, Agnes Kabigi alikuwa rafiki yangu pamoja na mwandishi wa habari mwenzangu.   kweli nina huzuni leo.  Mungu ailiaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

HABARI KUTOKA https://www.habarimtaa.com/2019/07/picha-mwili-wa-agnes-kabigi-waagwa.html
Mwili wa Meneja Mawasiliano wa asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Agnes Kabigi umeagwa leo Jumamosi Mjini Kahama na kusafirishwa kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazishi.

Agnes Kabigi alifariki dunia aliyefariki dunia jana mchana Ijumaa Julai 26,2019 baada kuanguka ghafla wakati akitekeleza majukumu yake akiwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Agnes Kabigi ni mwandishi Mwandamizi aliyewahi kufanya kazi katika Magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Nipashe na mpaka umauti unamkuta alikuwa anafanya kazi katika shirika la AGPAHI linalojihusisha na mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ambalo linafanya kazi zake katika mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Simiyu na Mara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa shirika la AGPAHI,wakati wa kuaga mwili wa marehemu,Mfanyakazi wa AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Kasablankhahr Herman amesema mwili wa Agnes utasafirishwa kwa ndege majira ya saa 10 leo jioni kutoka Mwanza hadi Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazishi.

Agnes alizaliwa tarehe Julai 13,1967.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Agnes Kabigi . Amina

No comments: