Showing posts with label Journalists. Show all posts
Showing posts with label Journalists. Show all posts

Saturday, July 27, 2019

TANZIA - Agnes Kabigi

Wadau, Agnes Kabigi alikuwa rafiki yangu pamoja na mwandishi wa habari mwenzangu.   kweli nina huzuni leo.  Mungu ailiaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

HABARI KUTOKA https://www.habarimtaa.com/2019/07/picha-mwili-wa-agnes-kabigi-waagwa.html
Mwili wa Meneja Mawasiliano wa asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Agnes Kabigi umeagwa leo Jumamosi Mjini Kahama na kusafirishwa kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazishi.

Agnes Kabigi alifariki dunia aliyefariki dunia jana mchana Ijumaa Julai 26,2019 baada kuanguka ghafla wakati akitekeleza majukumu yake akiwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Agnes Kabigi ni mwandishi Mwandamizi aliyewahi kufanya kazi katika Magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Nipashe na mpaka umauti unamkuta alikuwa anafanya kazi katika shirika la AGPAHI linalojihusisha na mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ambalo linafanya kazi zake katika mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Simiyu na Mara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa shirika la AGPAHI,wakati wa kuaga mwili wa marehemu,Mfanyakazi wa AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Kasablankhahr Herman amesema mwili wa Agnes utasafirishwa kwa ndege majira ya saa 10 leo jioni kutoka Mwanza hadi Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazishi.

Agnes alizaliwa tarehe Julai 13,1967.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Agnes Kabigi . Amina

Saturday, March 18, 2017

Dk. Ryoba Awaona Waanidshi wa Habari wa Uhuru Leo

DK. AYUB RIOBA AWANOA KWA SEMINA YA WELEDI WAANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA UHURU, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO
 Mwandishi wa habari nguli wa siku nyingi,Dk. Ayub Ryoba, akiendesha semina ya kunoa weledi wa taaluma ya uandishi wa habari kwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, leo katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Dk. Ryoba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ana shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika Sayansi ya Jamii aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Mwandishi wa habari nguli wa siku nyingi,Dk. Ayub Ryoba, akiendelea kutoa 'nondoz' kwa wafanyakazi hao wa UPL, huku wafanyakazi hao wakimsikiliza kwa makini sana
 Mwandishi wa habari nguli wa siku nyingi,Dk. Ayub Ryoba, akifafanua mada zake kwenye semina hiyo ya kunoa weledi wa kitaaluma
 Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini
 Dk. Ayub Ryoba, akiendelea kutoa mada kwenye semina hiyo
 Washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Dk. Ryoba
 Yassin Kayombo (aliyesimama) akijitambulisha kwa Ryoba (kulia) na kwa washiriki wengie wa semina hiyo
 Mgaga akijitambulisha
 Jongo akijitambulisha
 Mnkondo akijitambulisha
 Ally akijitambulisha
 Furaha Omari akijitambulisha 
 Gailanga akijitambulisha
 Utambulisho ukiedelea
 Utambulisho ukiendelea
 Washiriki wakiwa ukumbini
 Dk. Ryoba akiendelea na semina hiyo
 Washiriki wakiwa katika kundi la kwanza kujadili mada
 Washiriki katika kundi la pili kujadili mada
 Washiriki katika kundi la tatu kujadili mada
 Washiriki kundi la nne wakijadili mada
 Dk Ryoba akipitiapitia mada zake wakati akisubiri mrejesho wa maswali aliyowapa washiriki 
 Dk. Ryoba akijadiliana jambo na baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakati wa mapumziko. Kulia ni Furaha Omar na Bashir Nkoromo
 Dk. Ryoba akijadiliana jambo na baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakati wa mapumziko. Kulia ni Furaha Omar na Bashir Nkoromo
(PICHA ZOTE NA KAMERA YA BASHIR NKOROMO)

Saturday, May 03, 2014

Waandishi wa Habari Msikubali Kutumiwa

DSC_0017

Baadhi ya waandishi wa habari na wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wakifanya usajili kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.(Picha na Zainul Mzige).

Na Waandishi Wetu, Arusha

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari na kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.

Kibanda aliyasema hayo jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuongeza kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti zao na kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.

“Baadhi ya wahariri huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari na kuyapa uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa hayawahusu moja kwa moja,” alisema Kibanda.

Aliongeza kwa kusema kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa vidole na kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama kuvitetea kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii.

DSC_0053

Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.

“Kwa sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.

Kibanda aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha tatizo kwa kupata ufumbuzi.

Kwa upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.

“Kuwe na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kasongo.

DSC_0060

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw. James Jesse, akitoa mada kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya uhuru wa kujieleza kwa kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yanayofikia kilele leo jijini Arusha.

Mwanahabari mwingine mkongwe Dokta Samwilu Mwaffisi aliyetoa mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari alisema kuwa kuna haja ya waandishi kuzingatia uhuru wa habari walionao kwa kuzingatia maadili yanayowaongoza ili kuboresha heshima waliyonayo katika jamii kwa kuandika ukweli na uhakika, bila upendeleo, kutoa fursa ya kujitetea na kukubali kuomba radhi pale unapokosea.

“Kuandika habari zenye kuzingatia maadili kunapunguza manung’uniko, mashauri na kuongeza heshima ya chombo cha habari na mwanahabari mwenyewe,”

Akizungumzia suala la ufanisi, Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari, Kenneth Simbaya, aliwaasa waandishi wa habari kusimamia ukweli katika kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo litakawaweka huru zaidi katika utekelezaji wa shughuli zao za uandishi wa habari.

Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na umoja wa asasi mbalimbali chini ya uenyekiti wa MISA TANZANIA unafikia kilele chake tarehe 3 Mei kwa kuzindua majarida mbalimbali, matamko kutoka asasi mbalimbali na kuhitimishwa kwa tafrija ya chakula cha jioni chini ya mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mheshimiwa Mark Bomani.

DSC_0341

Mwanahabari Mkongwe kutoka Chuo Kikuu Huria, Dokta Samwilu Mwaffisi (kulia) akiwasilisha mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Simon Berege.

DSC_0311

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akitoa maoni yake wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.

DSC_0079

Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakongwe, mabalozi na wanahabari washiriki katika kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.

DSC_0028

DSC_0283

DSC_0371

Mwandishi wa Habari Chokonozi, Bw. Fredrick Katulanda, akielezea madhila mbalimbali yaliyomsibu katika utekelezaji wake wa kuandika habari za uchambuzi.

DSC_0119

Mwanahabari Mkongwe Bi. Leila Sheikh akichangia mada ya Mchango wa Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Katika Utawala Bora, Kukuza Uwezo Na Kupunguza Umaskini wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.

DSC_0348

Mmiliki wa Gazeti tando la Mjengwa na Kituo cha Redio Kwanza Jamii, Bw. Maggid Mjengwa akielezea jinsi Intaneti inavyoweza kuunganisha mtandao wa Redio.

DSC_0339

Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) na Mkurugenzi wa kituo cha mawasiliano Sengerema, Bw. Felician Ncheye akichangia mada.

DSC_0386

Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamamo hilo.

DSC_0310

Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.

DSC_0281

Picha juu na chini Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.

DSC_0322

DSC_0214

Kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 likiendelea.

DSC_0164

Mwanakamati wa maandilizi ya maadhimisho ya Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda nje ya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.

Wednesday, December 05, 2012

Warsha Kwa Vyombo Vya Habari London 6/12/12

WARSHA FUPI YA VYOMBO VYA HABARI KESHO ALHAMISI LONDON


Na Michael Zetulla

Jumuiya ya Urafiki kati ya UIngereza na Tanzania (Britain –Tanzania Society) itaendesha warsha juu ya vyombo vya habari Tanzania, kesho Alhamisi.

Semina hiyo itafanyika chumba namba 4421 katika chuo kikuu cha lugha SOAS (School of Oriental and African Studies) kilichoko Russell Square, katikati ya London, saa kumi na moja hadi saa moja jioni.

Mtu yeyote anaweza kuhudhuria na hakuna malipo yeyote yanayotakiwa.

Mzungumzaji mkuu atakuwa Ben Taylor wa Daraja ambalo linasimamia magazeti kadhaa mjini Njombe na Iringa ikiwemo Kwanza Jamii. Mwenyekiti wa warsha atakuwa Freddy Macha mwandishi na mwanasafu mkazi London.

Kufuatana maelezo yaliyotolea na jumuiya ya BTS, mada ya warsha itakuwa : “Habari na demokrasia Tanzania”. Shughuli hii ni sehemu ya warsha mbalimbali zilizofanywa na jumuiya ya BTS toka mwezi Oktoba kuzungumzia na kuangalia mada mbalimbali za Tanzania. Mwezi jana Waziri wa Uchukuzi , Dk Harrison Mwakyembe alialikwa kuzungumzia suala la katiba na usafiri katika ukumbi wa Central Hall, mjini London.

Habari zaidi tembelea:

http://www.btsociety.org/events-and-announcements

Au piga simu

+44-20-7727-1755
+44-7721-869-215